Ukweli ni kwamba Maandamano ya CHADEMA yamefanikiwa kwa 100%

Ukweli ni kwamba Maandamano ya CHADEMA yamefanikiwa kwa 100%

Lengo Kuu la Maandamano haya lilikuwa ni kuijulisha Dunia yote na Taasisi zote za Kimataifa kwamba Serikali ya Tanzania ndio inayoteka na kuua Wakosoaji wake kwa kutumia vyombo vya Dola, Hili limethibitika Rasmi, kwa Ushahidi Mwanana, Kauli ya Rais ya Juzi na mnachokiona mitaani ni uthibitisho kwamba Wauaji ni Watu wa serikali na Wanalindwa kwa Udi na Uvumba.

Kujitokeza hadharani kwa Freeman Mbowe huko Magomeni, Huku akijua kwamba atapigwa risasi ili afe au atakamatwa, Kumekata Ngebe na kuwafunga mdomo waliodhani hili jambo ni Utani, Huu ni Ushindi Mkubwa sana.

- LIVE - Yanayojiri kwenye Maandamano ya CHADEMA 23/9/2024

Hata ukimuuliza leo IGP au hata RPC Murilo kwanini wanazuia Maandamano ya Chadema, hawatokuwa na Majibu yoyote zaidi watasema ni Amri kutoka Juu.

Bali Swali ni hili, Unateka mtoto kama Soka na kumuua ili upate nini, uokoe nini au ushinde kitu gani ambacho kijana huyo alikuzuia kukishinda? Kama mnataka kuimaliza CHADEMA kwanini msimuue Mbowe au Lissu ili mkate kabisa mzizi wa Fitna?

Bali ifahamike kwamba Mungu siyo fala, Na Kila Ubaya Utalipwa.
IMG-20240923-WA0050.jpg
 
Wasaliti wakubwa nyie.Mmejificha chumbani kwenu huko tena uvunguni ,halafu saizi ndio mnajifanya kutoa pua zenu hapa. Mlikuwa wapi wakati Mbowe anakamatwa peke yake kama kuku? Waandishi wa habari ndio wamebaki wanamtetea na kumuombea asikamatwe na polisi huku Ninyi mmejificha porini huko
Na wewe ulikuwa wapi, si Mbowe alitoa wito hata kwa wasiowanachadema kwamba waandamane? Kwa mantiki hiyo, kwa vile hukushiriki, basi na wewe msaliti au siyo?
 
Mhhh. Kweli makurukurutabu ni janga la taifa. Eti lengo kuu la maandamano ya maandamano ya chadema ilikuwa ni kuijulisha dunia yote na tasisi zote za dunia na kwamba leo lengo hilo limefanikiwa kwa 100%. Hii ni akili ya samaki.

Hamujui hata dunia ni kitu gani. Kwenu Amerika na Ulaya magharibi ndiyo dunia nzima. Kwa taarifa yenu huko China, India Ukraine, Palestina, Amerika ya kusini, UAE na kadhalika hawana habari of your existence in this planet called dunia.

Hao mnaowaita dunia (USA, Canada and UK) ujumbe wenu walishausikia mapema tu na ku react kwa kuielekeza kwa maandishi na kwa matamko serikali yetu inachotakiwa kufanya. Raisi wetu shupavu aliwakoromea sana hao unaowaita dunia. Koromeo lake liliungwa mkono na kukaziwa zaidi na Umoja Afrika (AU) na Umoja wa Mataifa (UN).

Hao mnaosingizia wametekwa na kuuliwa na polisi hamna hamna ushahidi wo wote. Wengi wao inawezekana wametekwa na kuuliwa na chadema yenyewe kwani historia yake inajulikana kwenye masuala haya kuanzia ya Chacha Wenge nk. Inawezekana wengine wameuawa kwa kutembea na wake za watu, au kuiba mali za watu, kudhurumu wenzao, imani za ushirikina na kadhalika.

Uchunguzi (Criminal investigation) ya masuala haya siyo nyepesi kama ambavyo akili yenu inawatuma. Yanahitaji utaalamu wa juu na infrastrure ya juu katika dunia ya leo. Hata huko kwenye nchi zilizoendelea, zenye makamera kila mahali, forensic laboratories za hali ya juu, drones, artificial intelligence ya hali ya juu, robots na setilites za kutosha bado changamoto zipo nyingi tu kwani wahalifu nao wana akili na wanaweza ku evade hizo systems.

Sasa sembuse sisi ambao tunatumia zaidi ushirikishwaji wa wananchi huko mitaani, vijijini na vitongojini katika criminal investigation zeu. Kwa akili yenu mnafikiri maandamano ndiyo criminal investigation technique madhubuti ya kuwapata hao wahalifu. Mmeambiwa hiyo ni akili ya samaki. Leo mtakuwa mmejifunza kutokana na maandamano mliyokuwa mmeyapanga ku fail vibaya sana kwa wananchi kuyapuuzia mbali. Hata wewe hukuonekana huko kwa kuogopa kuchapwa virungu na kumwagiwa maji ya washa washwa. Kama mna akili hamtarudia tena hiyo dhana yenu ya maandamano.
🗑🚮🗑🚮🗑🚮
Halafu unajiita Akili !!!
Mbogamboga kuna hazina kubwa ya majinga
 
Sisi waislam kila wakati tunatakiwa tuseme ukweli

Jana Chadema imefanikiwa

Kila mtu jana Tanzania na duniani kwa jumla walikuwa wanafatilia siasa za Tanzania.
walikuwa wanaulizana kuna nini na kwanini kuna maandamano?
Jawabu ni simple wanaelezana 1, 2 , 3
Jina la Mbowe linawezekana limetajwa zaidi mara bilioni 1 au mbili. Ikiwa kwa wema au kwa shari. huo ni ushindi kisiasa.
Jina la chadema limeandikwa mara bilioni 2 au zaidi duniani hio ni jana. huo ni ushindi wa 2 kisiasa

Swala la kutoandamana.
Ukiondoa wanafunzi wa vyuo vikuu au waislam hakuna maandamano mengine yaliofanyika Tanzania bara
1. Sio madaktari
2. Sio walimu
3. Sio wakulima
]4 . Sio wafugaji

hii tofauti kabisa na nchi nyengine duniani. Hii ni asili ya Mtanzania, wapo wanaosema uliotengenezwa awamu ya 1.
Chadema walijua hilo na naamini wanajua hilo maana wao ni watz,

Ushindi wa Chadema ni Upi?
Sio kuingia barabarani, Ushindi ni kwamba kwanza yameepushwa maafa ambapo leo Taifa lingalikuwa katika Hamkani, watu wenye chuki na wengine wangalikuwa wanacheka, wanatengeza kesi, wanazomea, wanapanga kufuta vyama, Propganda kila kona, majumba yanvamiwa, masokoni hakukaliki, watu wanafukuzwa kazi, Kesi kila kona, miripuko ya kweli na ya mchongo ingalitengenezwa.
Hongera za pekee zimwendee Rais wa Tanzania kwa jinsi alivyoweza kuzima maandamano kwa njia ya Amani

NITASEMA UKWELI DAIMA, PROPAGANDA KWANGU MWIKO
 
Back
Top Bottom