MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,675
- 33,583
Siku moja nimetoka mwandege huko kufika Mbagala kuna mdaladala DCM ( umechoka mbaya) bila kujali ulipita na bampa kirahisi tu na uzuri kulikuwa na foleni na nipo upande wangu yeye ndio anachepuka!Tatizo la mbagala ni hapa nyuma mbele jalala[emoji445][emoji445]
Abiria wote wanaona niwaache waende tu bahati mbaya [emoji1787] , alitokea mama mmoja mwenye hekima akanifata akaninongoneza " kaka wasamehe tu, nakuelewa sana ila huku? " hapo nikakumbuka nipo maeneo gani.
Dereva alipiga honi nimpishè kama msafara alivyoona sijapisha akapita na bampa kibabe! Sasa huu ukanda wa bagamoyo road pamoja na changamoto za daladala hakuna akili hizi wala daladala zenye akili za namna hii.
Kwa ufupi kuna level ya utaratibu ukizoea ukaenda mitaa iliyojaa uswahili itakupa tabu sana. Ndio maana mtu akipata vijifedha kidogo anaenda kujibanza usawa wa bagamoyo road.