Ukweli ni kwamba Mbagala ina ardhi nzuri kuliko Bunju, Tegeta na Msasani

Bei ya Viwanja huko Tegeta, Bunju na Boko ni kubwa mno ukilinganisha na Mbagala, lakini linapokuja suala la Mvua Mbagala haina mafuriko kabisa kulinganisha na Tegeta, Bunju na Boko.

Sasa kinachowafanya wengi kukimbilia huko ni nini?
Nakuelewa Mkuu, Ila demand and supply ndio inaamua thamani ya eneo. Miundombinu, Rasilimali chini ya ardhi, proximity to the CBD, logistics, Milima yenye ukijani na fukwe ni baadhi vichocheo vya demand. Na hii siyo Tanzania tu bali dunia nzima. Kuna miji ambayo ina maafa ya kila aina ikiwemo mafuriko na vimbunga lakini ndiyo yenye mvuto kwa watu kila mtu anataka kuishi huko: Amsterdam, London, Valencia, Lake Geneva coast, Santa Monica, Santa Barbara, San Diego, the Saigon City, Capetown n.k.
Sehemu ambayo huwa nashangaa imekuwaje kuwa squtter licha kubarikiwa ni Kigamboni, Rungwe hills, Kilwa beach, Bagamoyo na Kijichi
 
Lakini pia ni elimu yao imewafikisha hapo wana wataalamu wa uhakika
Sisi sehemu korofi ndio tunajenga kama pale waliweka mabasi ya mwendokasi unaniambia walikuwa hawajui kuwa maji ndio njia yake hapo
Mkuu pale wenye taaluma zao wanajenga bila kuvuruga mkondo wa maji chini sasa sisi tuna kauli ya kipuuzi eti maji yanakimbia watu ndio maana unaona watu wanajenga hata Viongozi kukemea wanashindwa mimi tu sio mtaalamu wa ujenzi nilishangaa kuona sehemu ya ma bus pale yaani magari yapo mtoni maana miaka yote tunaona mkondo wa maji ukiongezeka...
 
Nakupa hadithi fupi kidogo, siku zote wachaga huogopa sana kabila za Pwani kwa hofu ya uchawi, same to Chanika, kapo ka imani Chanika huwezi jifugia ngombe wakastawi, ni lazima atakufa kitu ambacho si cha kweli, in short watu hukimbia sehemu wanazohisi zina uchawi na vijicho.
 
Wabongo wajinga tu,hakuna sehemu ardhi ni nzuri kama kisemvule,nilikuwa na kiwanja bagamoyo nikakiuzilia mbali,baada ya kuona tabu wanayopata majirani zangu,uko job mvua ilianza tu,ni mashaka matupu,kisemvule nimetulia nainjoy mvua ,siiogopi tena,kama sasa hivi hapa naangalia mabata yangu yanaogelea
 
Kabali yenu ni Kisarawe ndie anayecheua hayo maji yote mnayoangaika nayo huko mjini.Suluhisho Kisarawe ichukuliwe na Ilala na Makao makuu ya wilaya ya Kisarawe yapelekwe Maneromango huko.
 
Bei ya Viwanja huko Tegeta, Bunju na Boko ni kubwa mno ukilinganisha na Mbagala, lakini linapokuja suala la Mvua Mbagala haina mafuriko kabisa kulinganisha na Tegeta, Bunju na Boko.

Sasa kinachowafanya wengi kukimbilia huko ni nini?
Hata huko mbagala wakianza kujenga mahekalu kama bunju mafuriiko hayaepukiki
 
Naishi Kijichi, karibuni very classic na tulivu!! Hakuna waswahili wala mafuriko...!!
 
Daah kwa hiyo kujenga tu kisemvule umewazidi akili waliojenga Bunju hii hatari sana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…