Laki Si Pesa
JF-Expert Member
- Dec 20, 2018
- 5,085
- 9,022
Laki...mi nawalaumu sana akina Sykes na wapigania uhuru wengine kwa kushindwa kupigania haki zao baada ya uhuru enzi za Nyerere, hawa walipigana vita ya pili ya dunia, walipata wapi uoga wa kumuogopa Nyerere na kuacha historia kupindishwa makusudi? kwangu mimi Abdul Sykes ni looser badala ya kupigania haki yake akasusa
Wachana na OIC na porojo nyingine,nyinyi waislam wa Tanganyika mmefanya nini mpaka leo kujenga chuo?,wewe umebaki kuzurura tu kupiga soga kuliko kuja na mbinu mbadala.Magnifico,
Katika miaka ya 1970 mwishoni Organization of Islamic Countries (OIC)ilitaka kujenga chuo Tanzania.
Serikali ilikataa kutoa kibali.
OIC wakauhamisha ule mradi chuo kikajengwa Mbale, Uganda.
Katika miaka ya 1990s mwishoni Darul Imaan kutoka Saudi Arabia walitaka kujenga shule ya ufundi Kibaha.
Mradi huu ulipigwa vita na vyombo vya habari kuwa na mradi wa "Waarabu uliokuja kupora ardhi."
Darul Imaan walipoona uadui huu wakasimamisha kazi na ndiyo ukawa mwisho wa hiyo shule.
Aboud Jumbe akailalamikia Darul Imaan kwa hoja kuwa kama Tanzania Bara kuna uadui dhidi ya mradi huo mradi uhamishiwe Zanzibar na akaihakikishia Darul Imaan ushirikiano na serikali.
Mradi ukapelekwa Zanzibar na Zanzibar wakaomba wajenge Chuo Kikuu badala ya shule ya ufundi.
Darul Imaan wakajenga Zanzibar University.
Mwaka wa 2004 nikaalikwa chuoni hapo kutoa mhadhara wa maisha ya Sheikh Hassan bin Ameir.
MUFTI SHEIKH HASSAN BIN AMEIR (1880 - 1979)
Seminar on The Role of Educated Youth to Muslim Society 27 th February – 4 th March 2004 ORGANISED BY ZANZIBAR UNIVERS...mohamedsaidsalum.blogspot.com
Laki...
Nimekuwekea hapa siku chache zilizopita orodha ya vyuo vikuu nilivyopata kualikwa Ulaya, Marekani na Afrika.
Mimi sijui fedha zao zinakotoka.
Laki...kama akina Sykes wangepigania haki zao, leo Mohamed Said usingepata shida ya kutuhadithia mchango wao kwenye uhuru.
Nanren,
Mimi ninaweza nikakujibu kwa yale yaliyotokea Tanzania mwaka wa 1968 ya Kenya siyafamu.
Makao Makuu yalihamia Tanzania kwa ajili ya wingi wa Waislam ukilinganisha na Kenya na Uganda.
Nanren,EAMWS ilianzishwa na nani, kwa malengo gani na kwa nini ilipigwa marufuku Tanzania mwaka 1968.
Wanajamvi nadhani kuna haja kubwa ya kuijadili kwa kina iliyoitwa EAMWS (East African Muslim Welfare Society) iliyoanzishwa na jumuia ya Isma'ili Khoja mjini Mombasa, Kenya mwaka 1945 na baadaye tawi lake kufunguliwa Tanganyika...je ni kitu gani kilisababisha ipigwe marufuku Tanzania mwaka 1968...www.jamiiforums.com
Cpt,Kama lengo lilikua kujenga taasisi mbalimbali za afya na elimu ili kusaidia maendeleo ya jamii ya waislamu Tanganyika, ilikuaje wakasitisha lengo hilo wakati hiyo BAKWATA iliundwa na waislamu wenzao!? Labda utuambie shida ilikua serikali na sio kuundwa kwa BAKWATA.
Unataka kutuambia katika uongozi wa BAKWATA kulikua na wasio waislamu!?Cpt,
BAKWATA haikuundwa na Waislam.
Ikiwa unataka kusoma historia ya BAKWATA itakubidi usome kitabu cha Abdul Sykes.
Ni historia ndefu inayojumuisha watu wengi katika historia ya uhuru wa Tanganyika.
Cpt,Unataka kutuambia katika uongozi wa BAKWATA kulikua na wasio waislamu!?
Cpt,
Viongozi wote walikuwa Waislam lakini vyombo vya dola kama Polisi na Usalama wa Taifa vilitumika katika kuwasha moto wa chokochoko na propaganda ikawa inaenezwa na gazeti la TANU The Nationalist na Sauti ya Tanzania Dar es Salaam (RTD)dhidi ya EAMWS na viongozi wake.
Geoffrey Sawaya aliyekuwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai ndiye aliyetumika katika kuwahonga baadhi ya masheikh wampige vita Sheikh Hassan bin Ameir, Rashid Kayugwa wa Usalam wa Taifa yeye ndiye alikuwa mpanga mipango ya farka na Martin Kiama Mkurugenzi RTD na Benjamin Mkapa Mhariri wa The Nationalist wakawa ndiyo waenezaji wa propaganda dhidi ya EAMWS.
Hii ilipelekea viongozi wa EAMWS Tewa Said Tewa na Titi Mohamed kwenda kuonana na Julius Nyerere.
Kama nilivyokueleza historia nzima nimeieleza katika kitabu cha Abdul Sykes.
Katika viongozi wa EAMWS waliokabiliana na vita hivi aliye hai ni Bilal Rehani Waikela yuko Tabora na katika Kamati iliyoundwa kutatua mgogoro huu aliye hai ni Wakili Mussa Kwikima.
Nyaraka za Bilal Waikela za mgogoro ule ndizo zilizonisaidia kuweza kuandika historia hii pamoja na mahojiano niliyofanya na yeye nyumbani kwake Tabora mwaka wa 1987.
Nyaraka hizi zimehifadhiwa katika Maktaba ya Muslim Students Association of the University of Dar es Salaam (MSAUD).
Rashid Kayugwa baada ya miaka mingi alijuta na kuomba Allah amsamehe kwa yale aliyofanya na baadhi ya masheikh waliohusika katika kuivunja EAMWS walisafiri hadi Zanzibar kumwangukia Sheikh Hassan bin Ameir mbele ya Sheikh Ameir Tajo.
Yapo mengi.
Bilal Waikela anasema kama si EAMWS kutaka kujenga Chuo Kikuu isingelipigwa marufuku na ingekuwapo hadi leo.
Leo kuna watu wanaeneza propaganda kuwa Waislam hatupendi elimu.
Labda wanayasema haya kwa kukosa kujua historia ya Waislam.
Nimekueleza haya kudhihirisha ukweli wa niyajuayo.
Laki...siku waislam wakianzisha mgogoro na BAKWATA, chanzo kitakuwa ni Mohamed Said, maneno yako hayatawafurahisha BAKWATA
Bado kuna idadi kubwa tu ya wale ambao hadi leo hawatambui Baraza.mkuu, hiyo EAMWS imeshavunjwa siku nyingi, sasa hivi iko BAKWATA, huoni maneno yako yanachochea chuki kwa waislamu dhidi ya BAKWATA?
Hiyo ni kashfa kubwa tu.Waislam kama wanawake, wanapenda kujiona kundi maalum linaloonewa
Rommy...Historia hii kwa kua hawajaindika kwenye vitabu vyao vya kisekula sie tutawafundisha vijana wetu madrasa ili wapate kujua tu nini kilitokea mpk hali ikawa hivi. Povu ruksa.
Abunuwasi,Hiyo ni kashfa kubwa tu.
Mtu yeyote aliyestarabika hapaswi kutoa kauli ambayo inatuhumu jamii nzima. Mimi ni mwislamu na nimeishi na wakristu kwa miaka mingi na sijawahi kuwasikia wakitoa kauli za kipuuzi kama yako. Mungu ametupa midomo na mikono na mwisho wa siku vipao hivyo hivyo tulivyopewa vinaweza kutupeleka pabaya kutokana na matumizi ambayo hayampendezi mola.