Mi nawalaumu sana akina Sykes na wapigania uhuru wengine kwa kushindwa kupigania haki zao baada ya uhuru enzi za Nyerere, hawa walipigana vita ya pili ya dunia, walipata wapi uoga wa kumuogopa Nyerere na kuacha historia kupindishwa makusudi? kwangu mimi Abdul Sykes ni looser badala ya kupigania haki yake akasusa.
mi nawalaumu sana akina Sykes na wapigania uhuru wengine kwa kushindwa kupigania haki zao baada ya uhuru enzi za Nyerere, hawa walipigana vita ya pili ya dunia, walipata wapi uoga wa kumuogopa Nyerere na kuacha historia kupindishwa makusudi? kwangu mimi Abdul Sykes ni looser badala ya kupigania haki yake akasusa
Laki...
Nakusihi usitumie neno ''kususa'' nilishakueleza huko nyuma inawezekana tatizo ni lugha uliyoyozoea.
Kikwetu mtu akibaki kimya huo ni uungwana.
Wala halikuwa jambo la kuogopa.
Mambo kama hayo subra na subra ni sifa kubwa ambayo anayoweza kuwa nayo mja.
Maana yake ustahamilivu.
Subra ya Abdul ndiyo hii leo tunaishuhudia kuwa jina lake limerudi katika historia kwa njia ya kiungwana kabisa kuliko hivyo ulivyotaka wewe iwe kwa watu kuharibu hisani walizotendeana.
Magnifico,
Katika miaka ya 1970 mwishoni Organization of Islamic Countries (OIC)ilitaka kujenga chuo Tanzania.
Serikali ilikataa kutoa kibali.
OIC wakauhamisha ule mradi chuo kikajengwa Mbale, Uganda.
Katika miaka ya 1990s mwishoni Darul Imaan kutoka Saudi Arabia walitaka kujenga shule ya ufundi Kibaha.
Mradi huu ulipigwa vita na vyombo vya habari kuwa na mradi wa "Waarabu uliokuja kupora ardhi."
Darul Imaan walipoona uadui huu wakasimamisha kazi na ndiyo ukawa mwisho wa hiyo shule.
Aboud Jumbe akailalamikia Darul Imaan kwa hoja kuwa kama Tanzania Bara kuna uadui dhidi ya mradi huo mradi uhamishiwe Zanzibar na akaihakikishia Darul Imaan ushirikiano na serikali.
Mradi ukapelekwa Zanzibar na Zanzibar wakaomba wajenge Chuo Kikuu badala ya shule ya ufundi.
Darul Imaan wakajenga Zanzibar University.
Mwaka wa 2004 nikaalikwa chuoni hapo kutoa mhadhara wa maisha ya Sheikh Hassan bin Ameir.
Wachana na OIC na porojo nyingine,nyinyi waislam wa Tanganyika mmefanya nini mpaka leo kujenga chuo?,wewe umebaki kuzurura tu kupiga soga kuliko kuja na mbinu mbadala.
Hao ndo waislam duniani kote wao wanalalamika wanaonewa.Hata mngebaki waislam tupu dunia nzima na marehemu mudi tu bado ungekuja hapa tena kujilalamisha unaonewa.
Wanajamvi nadhani kuna haja kubwa ya kuijadili kwa kina iliyoitwa EAMWS (East African Muslim Welfare Society) iliyoanzishwa na jumuia ya Isma'ili Khoja mjini Mombasa, Kenya mwaka 1945 na baadaye tawi lake kufunguliwa Tanganyika...je ni kitu gani kilisababisha ipigwe marufuku Tanzania mwaka 1968...

Kama lengo lilikua kujenga taasisi mbalimbali za afya na elimu ili kusaidia maendeleo ya jamii ya waislamu Tanganyika, ilikuaje wakasitisha lengo hilo wakati hiyo BAKWATA iliundwa na waislamu wenzao!? Labda utuambie shida ilikua serikali na sio kuundwa kwa BAKWATA.

Cpt,
Viongozi wote walikuwa Waislam lakini vyombo vya dola kama Polisi na Usalama wa Taifa vilitumika katika kuwasha moto wa chokochoko na propaganda ikawa inaenezwa na gazeti la TANU The Nationalist na Sauti ya Tanzania Dar es Salaam (RTD)dhidi ya EAMWS na viongozi wake.
Geoffrey Sawaya aliyekuwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai ndiye aliyetumika katika kuwahonga baadhi ya masheikh wampige vita Sheikh Hassan bin Ameir, Rashid Kayugwa wa Usalam wa Taifa yeye ndiye alikuwa mpanga mipango ya farka na Martin Kiama Mkurugenzi RTD na Benjamin Mkapa Mhariri wa The Nationalist wakawa ndiyo waenezaji wa propaganda dhidi ya EAMWS.
Hii ilipelekea viongozi wa EAMWS Tewa Said Tewa na Titi Mohamed kwenda kuonana na Julius Nyerere.
Kama nilivyokueleza historia nzima nimeieleza katika kitabu cha Abdul Sykes.
Katika viongozi wa EAMWS waliokabiliana na vita hivi aliye hai ni Bilal Rehani Waikela yuko Tabora na katika Kamati iliyoundwa kutatua mgogoro huu aliye hai ni Wakili Mussa Kwikima.
Nyaraka za Bilal Waikela za mgogoro ule ndizo zilizonisaidia kuweza kuandika historia hii pamoja na mahojiano niliyofanya na yeye nyumbani kwake Tabora mwaka wa 1987.
Nyaraka hizi zimehifadhiwa katika Maktaba ya Muslim Students Association of the University of Dar es Salaam (MSAUD).
Rashid Kayugwa baada ya miaka mingi alijuta na kuomba Allah amsamehe kwa yale aliyofanya na baadhi ya masheikh waliohusika katika kuivunja EAMWS walisafiri hadi Zanzibar kumwangukia Sheikh Hassan bin Ameir mbele ya Sheikh Ameir Tajo.
Yapo mengi.
Bilal Waikela anasema kama si EAMWS kutaka kujenga Chuo Kikuu isingelipigwa marufuku na ingekuwapo hadi leo.
Leo kuna watu wanaeneza propaganda kuwa Waislam hatupendi elimu.
Labda wanayasema haya kwa kukosa kujua historia ya Waislam.
Nimekueleza haya kudhihirisha ukweli wa niyajuayo.
Historia hii kwa kua hawajaindika kwenye vitabu vyao vya kisekula sie tutawafundisha vijana wetu madrasa ili wapate kujua tu nini kilitokea mpk hali ikawa hivi. Povu ruksa.

Kilikuwapo kipindi Waislam walikuwa wanapambana na BAKWATA kila uchao lakini ikafika mahali wakajiuliza kwani sheria ya nchi inakataza kusajili taasisi za kidini kwa maendeleo ya wanadini?
Hapo ndipo Waislam wakaanza kupeleka maombi kusajili taasisi zao na haikuwa kazi rahisi lakini kuwepo kwa Rais Mwinyi madarakani palisaidia pakubwa katika hili kwani yeye aliona ile migogoro dhidi ya BAKWATA isiyokwisha hivyo akaruhusu kusajili taasisi za Kiislam.
Baada ya hapa hapajakuwa tena na mgogoro wowote Waislam kupambana na BAKWATA na Waislam wameweza kufanya mengi sana ya maendeleo yao.
Wamejenga shule, zahanati, wamefungua vituo vya radio na televisheni na kuwa na magazeti yao nawanaendesha programu nyingi tu.
Tatizo lililokuwapo ni kutokeza kwa kauli kutoka BAKWATA wakidai kuwa wao ndiyo wasimamizi wa Waislam Tanzania.
Lakini Waswahii tuna msemo, ''Domo kaya maziwa kwa mwenye mbuzi.''
Waislam wanabakia kimya hawajibizani na BAKWATA.
Unaweza kuisoma historia hii ya BAKWATA na Waislam hapo chini:
The Founding of Baraza Kuu (The Supreme Council of Islamic Organisations and Institutions of Tanzania) Abdallah Mgambo, Abbas Kilima...
mohamedsaidsalum.blogspot.com
''...President Mwinyi told the BAKWATA leadership to stop complaining and advised them to convene a meeting of all Muslim organisations to discuss whatever differences BAKWATA might be having with Muslims.
This advice by the government was ignored by BAKWATA. What BAKWATA envisaged was for the government to use its powers to effect a crackdown of those independent Muslims organisations to enable BAKWATA enjoy centre stage in Muslims affairs.
Muslims had long decided that the only way forward was for each organisation in its locality to try and help Muslims in its own way.
As these Muslims became engaged in various activities from building simple madras to providing tuition to school children BAKWATA increasingly became redundant and hence the statement by BAKWATA that the government was allowing other Muslim organisations to “meddle” into their exclusive zone, that of preventing Muslims to have any influence in the political system. ..''
Hiyo ni kashfa kubwa tu.
Mtu yeyote aliyestarabika hapaswi kutoa kauli ambayo inatuhumu jamii nzima. Mimi ni mwislamu na nimeishi na wakristu kwa miaka mingi na sijawahi kuwasikia wakitoa kauli za kipuuzi kama yako. Mungu ametupa midomo na mikono na mwisho wa siku vipao hivyo hivyo tulivyopewa vinaweza kutupeleka pabaya kutokana na matumizi ambayo hayampendezi mola.
Historia hii kwa kua hawajaindika kwenye vitabu vyao vya kisekula sie tutawafundisha vijana wetu madrasa ili wapate kujua tu nini kilitokea mpk hali ikawa hivi. Povu ruksa.
Rommy...
Ni muhimu haya yakajulikana kwani huenda huko siku za baadae hata kama sisi tutakuwa hatupo yakasaidia katika katika kuleta haki na usawa katika jamii yetu na hivyo kuepusha shari.
Hiyo ni kashfa kubwa tu.
Mtu yeyote aliyestarabika hapaswi kutoa kauli ambayo inatuhumu jamii nzima. Mimi ni mwislamu na nimeishi na wakristu kwa miaka mingi na sijawahi kuwasikia wakitoa kauli za kipuuzi kama yako. Mungu ametupa midomo na mikono na mwisho wa siku vipao hivyo hivyo tulivyopewa vinaweza kutupeleka pabaya kutokana na matumizi ambayo hayampendezi mola.
Abunuwasi,
Mimi kauli kama hizo hunitia hamasa ya kusomesha historia yetu kwani nachukulia kuwa kasema hayo katika ujinga, hajui kwa nini hali imekuwa kama hivi ilivyo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.