Ukweli unaoogopwa kusemwa kuhusu bwawa la umeme la Nyerere

Kama swala ni upatikanaji wa hewa safi. Bahari ipo na ndio inatoa 80% ya oksijeni tunayovuta.

Umetoa wazo zuri sana mkuu. Tupande miti kufidia iliyokatwa problem solved.
Nashangaa hizi kelele, tukitaka kupanda miti mipya hata milioni 3 igawanye kwa mikoa hata wanafunzi wa shule ya msingi wanafanya. Watu walihamisha bahari ili wapate ardhi itakuwa kujenga bwawa la umeme?

Tumeruhusu makuwadi wakae viti vya mbele na sasa wanatuona wajinga!
 
Swala la gesi kilitokea nini Mtwara hadi vipigo vilitembea? Hiyo gesi mbona nayo imejaa mitego mingi tu! Ukiangalia ndio maana JPM aliona bwawa la umeme ndio litatuweka huru kwenye energy na akahakikisha linajengwa kwa fedha za ndani! Acheni kuwasikiliza wanasiasa corrupt.
 
Kuna watu watalaaniwa kwa kuwa upande wa shetani kupinga huu mradi. Huu mradi utatukwamua na kuwa huru kwenye energy!

Hiyo gesi itafanya biashara nyingine lakini umeme wa bwawa la Nyerere utakuwa wa Watanzania asilimia 100 na hakuna atayetupangia bei! Tumejenga kwa fedha zetu wenyewe! Ukiwa huru kwenye energy utakuwa huru kwenye mengi pia.

Gesi iendelee na PPP ifanye biashara, tena wenzetu Kenya wameomba tupeleke gesi kwao! Tuanzie hapo.
 
Hilo bwawa sio center ya mambo yote, ni porojo tu kama zile za Muhongo na gesi.
 
Hilo bwawa sio center ya mambo yote, ni porojo tu kama zile za Muhongo na gesi.
Inaweza isiwe centre ya mambo yote (kwa jinsi mambo yanavyokwenda) ila likitumika vema litakuwa centre ya mambo yote - kama tunataka energy mix ya upepo na jua unadhani tutatunza vipi hio energy ili itumike baadae...

 
Unajua wewe ni mjinga ila hujui tu kama ni mjinga, ndiomanaa unaadika upupu kama huu kwa kujiamini kabisa.
 
Wewe jamaa hujui kitu unabwabwaja tu au umetumwa kuja kuangalia hali ya hewa,unajua hiyo gesi ya Mtwara inaenda na Wazungu?
Sisi kukata miti milioni tatu si kitu hao wazungu wamekata miti milioni ngapi kufanya hayo maendeleleo yaliopo huko kwao leo? Unadhan kuna maendeleo yanayokuja bila athari?
 
Misri lile bwawa lao la kufua umeme katika mto Nile walijenga juu ya miti?. Ghana na zimbabwe yale mabwa makubwa walijenga kwenye hewa bila kukata miti?

Ulaya miradk mikubwa ya nyukri hewani? Acha kushikiwa akili we dogo
Mueleweni huyu Bwana vizuri.Nadhani yeye anachohoji ni miti millioni tatu ilipokwenda.He is not concerned about cutting of trees.He believes kwamba hiyo miti imeuzwa,sasa pesa iko wapi?
 
Acheni uchambuzi wa kichawa. Vipi miti inayokatwa kwa kilimo, mkaa na kusafirisha magogo nje? Mbona haya haujayaandikia aya.

Acheni kupumbazwa eti mazingira ni mkawa wapumbavu kweli kweli
 
Una uhakika gani umeme wa maji hautakuwa bei juu? Unajua terms za mkopo wa ujenzi wa hilo bwawa? Mbona ndege ni zetu, lakini nauli ni bei gali kulinganisha na fastjet? Acheni utapeli wa kijinga.
Watu wengi hawajui kuwa bei muafaka lazima ihusishe kiasi cha “roc” - return on capital invested. Ikipigwa bei ya uhakika kulingana na matarajio ya urejeshaji wa mitaji uliowekezwa, si ajabu hicho kinachoitwa “umeme wa bei rahisi” kikaonekana enzi za wajukuu. Hapo pia itategemea kama mafisadi wajao hawatachezea miundombinu.
 
Luqman maloto huwa anamuandama sana hayati JPM mwamba wa chato sijui alimfanya nini
 
Unataka kujenga nchi sio kubomoa nchi,LAKINI ujenzi wa nchi unahitaji maamuzi sahihi na salama kwa maslahi mapana ya nchi yetu.
Haya mambo ya one man show ni usiku wa giza.
 
La Nyerere.. usikie ghalama harisi na na sio unaleta mbwembwe za 11 tl badala ya 6.5 tln.. mweupe sana wewe jamaa.

Kadirio mwanzo kabisa wa huo mradi ilikuwa ni $3.5b. sasa piga hiyo bei kwa sasa baada ya vifaa na dola kupanda na +VAT kisha uje uendelee na mjadala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…