Ukweli unaoogopwa kusemwa kuhusu bwawa la umeme la Nyerere

Kadirio mwanzo kabisa wa huo mradi ilikuwa ni $3.5b. sasa piga hiyo bei kwa sasa baada ya vifaa na dola kupanda na +VAT kisha uje uendelee na mjadala.
Unaongelea kadilio wakati mradi uanelekea kuisha? Sasa hivi ongelea actual.

Ushakuwa mweupe kabisa wewe.
 
Unataka kujenga nchi sio kubomoa nchi,LAKINI ujenzi wa nchi unahitaji maamuzi sahihi na salama kwa maslahi mapana ya nchi yetu.
Haya mambo ya one man show ni usiku wa giza.
JNHPP, SGR ni miradi ya nchi siyo ya mtu. Ni miradi iliyoanza tangu zama za Mwalimu. Kila awamu ya uongozi wa nchi yetu ilitimiza wajibu wake kwa kadri ya uwezo wake.

Mzee JPM na Serikali yake ambayo Mhe. Rais Dk. Samia alikuwa ni Makamu wa Rais, ikaamua kufanya kweli ibaki lawama. Mradi ukaanza. Mhe. Rais Samia kaukuta na 37 asilimia. Kakimbiza kwa kasi leo ni 78+asilimia. #JNHPP na SGR ndiyo miradi ya kuleta mapinduzi ya maendeleo. Tupongeze kasi ya Rais.πŸ™πŸ™πŸ™
 
Unaongelea kadilio wakati mradi uanelekea kuisha? Sasa hivi ongelea actual.

Ushakuwa mweupe kabisa wewe.

Kwahiyo kadirio la mwanzo liko chini kuliko uhalisia? Unataka kusema ni mradi wa $2b?
 
Toka tunapata uhuru mafisadi wamekuwa wakitupiga sana kwenye nishati.

Hivyo huu mradi ni pigo kwao. Zitatafutwa kila sababu tu ionekane haufai.
 
Gesi nayo non-renewable na kivyovyote lazima ilete mabadiliko ya tabianchi lkn maji ni renewable jambo la msingi kuendelea kuhamasishana kupanda miti mingi.lazma tuharibu pahali ndio tuweze kujenga nchi yetu.ni vema kuangalia nchi za wenzetu hasa waafrika wanafanya nini katka sekta hii ya umeme wa Gesi na Maji ambayo ni muhimu katka maendeleo ya viwonder
 
Una hoja lakini umeiwakilisha kisiasa zaidi kuliko kitaalamu. Kitaalamu ungeweka takwimu kwenye hoja zako badala ya blaablaa. Km gharama za kuendesha mitambo ya kufua umeme kwa gesi / maji au usalama (uzalishaji endelevu) kwa mitambo ya gesi / maji. Je, umefanya tathmini ya faida/hasara ya kimazingira ya ufuaji na usambazaji wa umeme wa gesi / maji?
 

hakuna real project ambayo haina athari za kimazingira. kitu cha muhimu ni kupunguza athari zake. pia gesi pia ni mharibifu wa mazingira. maana ikiungua inasababisha greenhouse gases ambazo ndiyo chanzo cha ongezeko la joto duniani.
 
Kukata miti million 3, kwenye square meters za maraba 1,500 huo ni uongo.
Pia bwawa Lina hifadhi maji , sio kila siku Lina pitisha maji .
Gas kama ikizalishwa in full capacity itadumu kwa miaka isio zidi 35, gas itakuwa imekwisha kabisa.
Lakini bwawa litakuwa bado lipo.
Chamsingi tutunze vyanzo vinavyo jaza bwawa la JNHPP.
 
Jifunze ku attach hizo picha vizuri.

Anyway watakuja na blaa blaa za kusema gas imeuzwa na umeme wa gas Ni ghali Sana πŸ˜‚πŸ˜‚.

Ila Hilo bwawa ni expensive Sana kuliko uhalisia wake.Til.11 Ni Pesa nyingi Sana aisee..
Baada ya wewe mwenyewe kufundishwa na kujua namna ya kuattach kule kwa wakenya naona ushakua mwl sasa πŸ˜€
 
Hili bwawa ni uamuzi mzuri tu,, ila baada ya miaka 10,, mahitaji ya umeme yata triple,, sababu maendeleo yanakuja kwa kasi, punde tutahitaji megawatt 10,000,hivyo tuharakishe miradi mingi ya kuzalisha umeme,, hakuna kupumzika, hadi tuzalishe Gigawatt 1000
 
Siasa, siasa,siasa. Mambo ya kitaalamu ukiingiza siasa bado kutakuwa na maneme meeeennnnggiiii.
 
Kwani ulikua wapi wakati Maghufuri anasema Gesi ya Kusini sio yetu tena!?
 
Maloto ni sehemu ya project au kiwanda maalum cha matusi kwa JPM. Hawa hata kwa mama Samia wanaishi nae kinafiki lakini wana ajenda zao.
Luqman maloto ni takataka tu inayolipwa vilaki laki kufanya propaganda za hovyo hovyo dhidi ya mwamba JPM.

Maloto ni pimbi
 
Mtoa mada samahn naomba nikutusi, ww ni pimbi na takataka.

Hivi mnalipwa kiasi gn kufanya upotoshaji?

Kwa taarifa yako tu eneo lililokatwa miti ni kama 2% tu ya eneo zima. Ww ni pimbi
 
Nimekusoma hadi hapo katikati, roho ikanichefuka na kutaka kutapika.

Ninachojua ni kwamba mradi huu wa umeme sasa utawapa kazi ngumu sana watu kama wewe mnaotafuta kuvuna kwa jasho la waTanzania. Hivyo vi-miradi vyenu vya pembeni vya kuwakamua waTanzania sasa italazimu mtoike jasho kuvijengea hoja ya ulazima wa uwepo wake.

Visababu vya kuwa na vyanzo tofauti vya uzalishaji isiwe ni vichochoro vya wizi wenu.

Mtakapolazimisha kuja hapa na kutumia jua letu, upepo wetu, ujoto ardhi wetu ili mtukamue zaidi, itabidi tuwaulize maswali magumu kwa nini mtuuzie kwa bei ya juu zaidi kuliko umeme tunaozalisha kwa maji yetu.
Kuna siku, waTanzania wataelewa mbinu zenu, na watazikomesha.
 
Huna gas ww? Kipindi kile bungeni uliambiwa umeme ukizalishwa kwa kutumia gas, bei zitashuka vip tokea waanze kuzalisha umeme wa gesi Cost per unit imeshuka?

Hapo ndipo utapata majibu gas ni ya nani na nani ana control bei ya hiyo gas.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…