Ukweli usemwe: Aliyeharibu nchi hii ni Mwalimu Nyerere kwa kushindwa kuwapa Watanzania Elimu

Nadhani hustahili lawama kwa Sababu ya Umri pengine!

Unajua au kusikia ajira ya waalimu wa UPE?

UNAJUA UPE NININI?

Unajua kwa nini Mwalimu alifanya hivo?

Mwalimu alifanya kila aliloweza!

Sema tu neno UJAMAA NI JINAMIZI HATA LEO!!
 
Sababu za Nyerere kufeli ni external factors za kubadilika kwa Sera za kisiasa na kiuchumi za kidunia.Sera zilizopelekea mataifa ya kiafrika kuletewa ukoloni mambolea.
Kwa Tanzania hakuna kiaongozi kama Nyerere ukiwajumuisha Mwinyi,Mkapa,Kikwete,Magufuli &Samia ukiwajumuisha wote hawafikii hata robo ya uwezo wa Nyerere kiouongozi.

Matatizo ya Tanzania yamesababishwa na viongozi wasio na vision baada ya Nyerere,ni Mara 100 angeendelea Nyerere kuongoza.
 
Kila siku nasema h
Kila mara nasema humu Nyerere na mashoga zake walikua na tamaa ya uongozi tu hatukua tayar kujitawala hivi unaenda kudai Uhuru nchi nzima haina hata watu waliotayar kua viongozi unaenda kudai Uhuru wa nini kisa shobo za kijinga
Nyerere katuingiza kwenye zahma kubwa sanaa tena hasa baada ya kutuachia hawa CCM chama cha mambuzi ndio maana wale vijana kina hanspope walitaka kukapindua kwasababu waliona kabisa huyu atakuja kua ndio chanzo cha umaskini wa watanzania
Miaka ya baadae kuna vijana wataenda kulichapa bakora kaburi lake hawa kina Nyerere nashangaa tunawaenzi Kwa upuuzi waliotuletea
#Mchonga meno katuweka kwenye matatizo mengi zaidi ya faida#
 
Kwa hayo nyerere hayumo, waliofuata mpaka sasa hawajafanya kazi yao kutuvusha sawasawa.
 
Umemaliza yote.
Bila ya kusahau pia Mwalimu Nyerere alikuwa na msemo wake kwamba "Ikulu ni sehemu ya lawama,ikulu sio sehemu ya kuikimbilia"lakini hawa viongozi wa sasa wako tayari kutumia nguvu yoyote ili mradi wabaki ikulu na kuendelea kuitawala nchi ikiwemo na kuandaa watoto wao waje kuendeleza kuitawala nchi na hata wanaostaafu bado wanataka kuishikilia nchi kuwa mali yao.
Ni aibu kubwa sana kumfananisha nyerere na viongozi wa kisasa wenye tamaa ya kujilimbikizia utajiri wa nchi.
Leo hii aje kusifiwa mtu aliyefanya ufisadi wa kufuru kwa kujenga majengo tupu ya shule yasiokuwa na walimu ambayo yanalea watoto kisha wanarudi mtaani kuwa Panyaroad,je hiyo ndiyo elimu inayokusudiwa Watanzania waipate?
 
Mwl alifeli pia kwa kukitukuza kiswahili na kukipromote kuwa lugha ya taifa .
Tunetengeneza taifa ambalo lipo isolated sana na dunia. Watu wanahitaji akina mkandara kutafsiriwa cnn english news.
Huwezi kuendelea ki technolojia kwa kutumia lugha ya mwenzio,mataifa yote yanayoongoza katika technology mbalimbali Duniani wanajifunza kwa lugha zao.
Leo Hui Putin ugomvi wake mkubwa ni kuhusu west Ku destroy culture ya Russia. Alicho kosea Nyerere ni kutobalisha masomo yawe kwa lugha ya Kiswahili kuanzia darasa LA kwanza hadi university
 
Huu sio muda wa kumlaumu marehemu...huu ni muda wa kuanza kuleta mabadiliko unayotaka kuyaona.
It begins with you.
Watu wanaoifisidi Nchi ni lazima wamtafute mtu wa kumwangushia gari bovu !!
Sisi tunashikilia kwamba yeye Mwalimu hakuwa fisadi na hiyo inatosha kuamini kwamba alikuwa ana nia njema sana na Taifa lake !
Mengine aliyokosea ni kwa mapungufu ya kila binadamu aliyonayo !
Hakuna binadamu aliye mkamilifu !!
 
Hivi unafikiri kina mhongo walisomeshwa kipindi gani, tatizo letu kubwa ni ubinafsi.
Ukiangalia wakuu was usalama wengi kipindi chake walikuwa PhD holder.
Aliondoa mfumo was watoto wa machifu kuwa wapewe kipaumbele kusoma, alitaifisha shule za dini Ila Kila mtu asome.Alianzisha vyuo vingi vya Kati ili watu wapate ujuzi Leo hii tuna vyuo na wasomi wengi wanasaidia Nini taifa, PhD wa uchumi anaweka tozo benki?
 
Enzi za Nyerere huduma za elimu, hadi anangatuka zilikuwa nzuri sana! Tatizo baada ya hapo, serikali ilianza kutumia hela za umma kulia Bata! Kuanzia Mwingi, safari za nje za anasa! (Rejea safari ya RioDejeneiro ktk mkutano wa mazingira mwaka 1992).
Kama warithi wake Wangwe seleza jitihada zake, tatizo la elimu halingekuwa!
Ila katika katiba, mimi simtetei Nyerere, alituuza, ndiyo chanzo cha ubovu wa Tz ya leo!
 


Huyu mzee unamuonea Tu

Kwa miaka Ile hata chakula cha kulisha wanainchi wake ilikuwa ishu

Hata dawa hospital zilikuwa hamna

Do you think angewekeza Kwa watu kupata Elimu kuliko kula?
 
Nadhani hustahili lawama kwa Sababu ya Umri pengine!

Unajua au kusikia ajira ya waalimu wa UPE?

UNAJUA UPE NININI?

Unajua kwa nini Mwalimu alifanya hivo?

Mwalimu alifanya kila aliloweza!

Sema tu neno UJAMAA NI JINAMIZI HATA LEO!!
UALIMU PASIPO ELIMU
Hiki ndicho kituko kingine alichokifanya mwalimu.

Utawafundishaje watu wewe huna elimu? Nyerere alikuwa nataka ku reinvent the wheel.

Ukweli ni kwamba alikuwa na kila namna ya kujenga nchi ya wasomi. Kulikuwa na nchi nyingi tu zilizokuwa zina mu support. Angeweza hata kupeleka watu wake wakajifunzo huko namna ya kufundisha.

Just imagine kama angeweza kupeleka watu watu 10 kila kijiji wakaenda kusomea ualimu kwa miaka miwili miwili. Maana yake kipindi cha miaka miwili angekuwa na walimu 200,000.

Sasa unakuja na sera ya UPE what a failure.
 
Ukweli mchungu ,pro ujamaa watakuja kukuambia eti mwalimu aliacha Mali nyingi za umma.
Nyerere ameacha nchi ikiwa bikra kabisa bila kuiba chochote.

  • Ameacha madini
  • Ameacha misitu
  • Ameacha mashirika yaumma zaidi ya 400

- Ameacha viwanda lukuki, vingunguti ilikuwa imechangamka.

- ameacha nchi moja.

Waluofuata wamefanya nini, zaidi ya kugawana keki ya taifa, kugawia watoto wao na machawa??!!
 
Huyu ndio rais aliyeweza kulinda rasilimali zanchi kama leo hii rais ndani ya miaka 2 tu kashauza kila kila kitu tukimpa miaka 20 hii nchi itakuwa sio yetu tena tutarudi kwenye ukoloni
Na huyo huyo ndie alietuwachia hii katiba wanayoitumia hao viongozi kufanya wanavotaka inawapa mpaka kinga ya kutoshitakiwa

Sent from my ATU-L31 using JamiiForums mobile app
 
Hao wachache walisomeshwa na mwalimu, zaidi ya kuwa mafisadi wameifanyia nini nchi? Aliiacha nchi ikiwa unexploited, lakini wameuza kila kitu, walipoona raslimali zote zimekwisha, wameamua kuuza hata Bandari kwa style ya santakalawe.

Kufika 2030 hata chama chao kilichoanzishwa na nyerere na wenzake watakipiga mnada.
 
alichokosea ni kuwa alijua hii katiba siyo ila akatuachia hivyo hivyo hayo mengine unamuonea!
angebadili katiba na kuweka sheria kali kwa viongozi wa umma wala tusingekuwa hapa!
 
Kwenye Katiba hapo ndipo alipobugi stepu na alikuja kuliona hilo na akaonya when it was too late !
 
Asante tena kwa uchambuzi mzuri...

Msingi wa watu wanaojiamini,msingi wa watu wenye elimu nzuri...nadhani hapa hauongelei tena idadi,bali aina ya elimu ya hao wachache waliyoipata.

Ni kipindi hicho cha Nyerere mtu akipata elimu,unaiona elimu yake wazi wazi,kuliko elimu hii ya sasa ambayo wengi wanaingia shule wakiwa wajinga,wanatoka wakiwa wajinga vile vile..wanafaulu div 1 za kutosha lakini unapomsikiliza unamuona elimu hajaipata sawasawa.

Elimu ya kipindi hicho,serikali iliibeba elimu kama wajibu wake wa msingi,mtu atapata huduma zote za elimu bure hadi chuo kikuu,leo hii elimu inaendeshwaje? ,hatushudii wanafunzi wanashinda na njaa shuleni kutwa nzima,huku serikali ikilazimisha wazazi wachangie chakula,wazazi wasipo changia chakula hicho wanafunzi wanashinda na njaa kutwa nzima...

Rungwe mzee wa ubwabwa amekuwa akiishangaa serikali inapelekaje mtoto shule bila kumhakikishia kuwa atakula?

Hoja yako kubwa naiona ni kuihamasisha serikali iboreshe elimu na siyo kukazania kuongeza idadi ya vituo vya watoto kwenda kukua huku wakiviita vituo hivyo shule
 
Ndio maana nasema kipindi chake elimu ilikuwa bahati mzee. Haikuwa haki ya watanzania wote.

How many people like mhongo wapo. Na hawa wamekuwa machawa tu, kutokana na kuishi katika nchi isiyo na misingi bora ya elimu.

Kila mwaka sera za elimu zinabadirika. Hakuna msimamo wowote kwenye elimu ya mtanzania. Hii nikutokana na muweka maono ya nchi kukosa dira ya elimu katika nchi yake.


Kwa hili la elimu Nyerere ali fail.
 
Nyerere aliogopa wasomi ili kuzuia ukosoaji dhidi ya sera zake za kijamaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…