Nawasalimu wanaJF.
Leo nimeamua niseme ukweli kuhusu nchi yetu hii ya Tanzania.
Katika miaka 24 ya utawala wa Mwalimu Nyerere, alitangaza maadui wakubwa wa watatu wa watanzania:-
1. UJINGA
2. UMASKINI
3. MARADHI
Mwalimu Nyerere hakuwa visionary leader alikuwa mwanaharakati, badala ya kujenga nchi na kuwapatia elimu watanzania alikuwa na misemo tu, kuongea majukwaani tu bila vitendo.
Je, Mwalimu Nyerere kitu gani kilimshinda kujenga shule za msingi kila kijiji kwa miaka yote hiyo 24 badala yake akajenga ofsi za chama kila kijiji?
Je, kitu gani Mwalimu Nyerere kilimshinda kwa miaka 24 kujenga vyuo vya ufundi kila wilaya badala yake alijenga viwanja vya mpira wa miguu?
Lowassa aliweza kujenga shule za secondary kila kata. Je, Mwalimu Nyerere kitu gani kilimshinda kwa miaka 24 kujenga Shule hizo?
Tunaweza kutafuta mchawi wa taifa letu. But kusema kweli Nyerere alitukosea sana watanzania.
Nadhani Mwalimu Nyerere alikuwa na mentality za utawala wa kifalme ambao hauna malengo.
Tunaona mataifa mengi yaliyowekeza kwenye elimu alivyopiga hatua.
Yeye Mwalimu Nyerere hakuwa na nia kabisa ya watanzania wengi kupata elimu. Wakati wa Mwalimu Nyerere kusoma ilikuwa ni bahati na siyo haki ya Mtanzania.
Taifa lisilokuwa na elimu haliwezi kujiendesha vizuri, litabaki kuwa ombaomba tu.
Sisi kama Taifa ni lazima tujue tulipoangukia, tukainuke na kusonga mbele. Bado hatujachelewa.
Tanzania tupo na vijiji na mitaa isiyozidi 20,000. Kwani alishindwa nini kuchukua kila kijiji vijana 10 na kuwapeleka kusoma nchi za nje? Vijana 10 kila kijiji maana yake ni watanzania 200,000 tu.
Yaani angechukuwa wanawake 5 na wanaume 5.
But uwezo alikuwa nao wa kufanya hivyo.
Nitaendelea kueleza machungu yangu haya kwenye uzi huu ili tujue wapi tulipoangukia tukainuke na kusonga mbele...
Kama hujui legacy ya Nyerere bora ukae kimya. Hiki ndio kile kizazi ambacho hata Nyerere mwenyewe mmemsikia kwenye tv.
Unafahamu vyuo vikuu vya serikali isipokuwaUDOM tu alijenga yeye. UDSM, SUA, Mzumbe, CBE, vyuo vingi vya ufundi Moshi Tech, Dar Tech, ArushaTech n.k
Unafahamu vyuo na taasisi za utafiti nchi nzima Maruku(Kagera), Lyamungo (Moshi), Ukirguru(mwanza) Uyole (Mbeya), Naliendele, Katrini, selian, n.k
Unafahamu shule zote za secondary za serikali zilizokuwepo kabla ya mkapa kuanza kujenga alijenga Nyerere over 200,
Unajua shule za msingi zilizokuwepo kabla ya mkapa alijemga Nyerere.
Unafahamu wakati wa nyerere Darasa moja lilokua watotohawazidi 45 na hakuna mtoto aliyekaa chini
Unajua wakati wa nyerere hakukuwa na ada, watoto walisoma bure na walikula shule na vitabu na madaftari walipewa bure kila mtoto.
Unatambia literacy level ilifikia 82% kutoka less tha 10% wakati tunapata uhuru
Some literature, vyuo vikuu vyetu vilikua vinaongoza Africa kwa ubora wa elimu
Mapungufu yameanza baada ya kuingia warith wake.
Sijui kwa nini umeamua kumbagaza huyu mzee wakati ndio aliyepigania elimu kwa kiwango cha juu sana. Na ameandika maandiko mengi sana kuonyesha umuhimu wa kukuza elimu.
Kama hijamsoma nyerere uaipende kutoa lawama kwa usiolijua