Ukweli usemwe: P Funk ndio mtu mnyonyaji zaidi kuwahi tokea kwenye historia ya Bongofleva

Ni wazi ndivyo ilivyo.
Kisheria kuna ile haki inaitwa exclusive right, kwamba kama msanii ameuza mpaka exclusive right basi anakuwa hana haki tena na hiyo kazi.

Mfano, nasikia Darassa aliuza album yake boomplay kwa milioni 140 hivi (na exclusive right), baadae wimbo wake wa I Like It ukatumika kwenye movie na boomplay wakalipwa milioni 600, akaanza kujilaumu.
 
Soggy hata juzi kama miezi miwili imepita alikuwa anaongea kuwa waliingia mgogoro na P Funk baada ya ngoma ya Darubini Kali ya Afande Sele, beat aliifanya Soggy ila credit hakupewa na vitu kama hivyo.
Soggy na Lamar si Sawa na Prof. Ludigo na Bizman. Hawa ni wanafunzi tu wa Majani huko studio. Walikuwa wameajiriwa hapo kama Producers!?
 
daah noma sana aisee😱😱 umaskini huu mbayaa
 
hivi mpaka beat inatumika inakuwa hao wanaogiza movie wameitaka au umejipigia promo??
 
hivi mpaka beat inatumika inakuwa hao wanaogiza movie wameitaka au umejipigia promo??
Wanakuwa wameipenda wenyewe. Ila wakati mwingine huwa wanatoa tangazo watu walete kazi zao ili zitumike kama soundtrack, wanatoa idea ya movie na kusema nyimbo ziwe na maudhui hayo, ila mara nyingi ni kwa wao kupenda nyimbo zilizotoka tayari.

Kwenye Sometimes in April movie, walitumia kinyemela wimbo wa Dataz ft Soggy Doggy; Soggy alipofuatilia walilipwa hela yeye na Dataz
 
Unajua nini Ndugu Mdau!? "Haki Haiombwi" Bali "Inapiganiwa". Kama Prof. Jay anaamini ana Haki yake imedhulumiwa, hakuna aliyemkataza kuipigania. Majani alisafiri mpaka Uganda kuipigania haki yake.
 
Unajua nini Ndugu Mdau!? "Haki Haiombwi" Bali "Inapiganiwa". Kama Prof. Jay anaamini ana Haki yake imedhulumiwa, hakuna aliyemkataza kuipigania. Majani alisafiri mpaka Uganda kuipigania haki yake.
Mkuu mimi sio msemaji wa Prof. Jay ila ni mdau tu wa kusikiliza habari kwenye media. Nimezungumza kile nilichokisikia

Ni imani yangu kuwa Professa anapitiaga mitandao ya kijamii, huenda ataona huu ushauri wako
 
Hivi huonΓ­ kuwa nimeuliza nieleweshwe?
 
So hapo producer hakulipwa kitu?? au walimmegea pia..
 
Statement ya akili Sana hiyo. Eti "sikujua kuwa sheria hairuhusu hii". Mahakama inakupiga nyundo tu.
 
Ukweli lazima usemwe.
 
Kama ile kesi ya MWANA FA NA AY mpaka wakalipwa BIL 2 sijui na tigo ina maana ukitumikaa wimbo bhasi ndo haki ya msanii kulipwa ila likitumiKA BEAT tu bhasi haki ya producer kulipwaa... ngoma ngumu snaa hii πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€
 
Ni kweli ni mgogoro mkubwa. Kwani kila mmoja ni wazi anaibeba kazi ya mwingine.
 
Sikiliza interview za wasanii wa zamani mfano Ferouz, anasema P. Funk aliwasaidia mawazo na kuwapeleka mpaka kuuuza albam kwa mdosi, maana walikuwa hawajui waanzie wap baada ya hapo wakawa wanaenda wenyewe
Skia, mtafute Feruzi mwambie mnataka kufanya biashara utumie wimbo wake wa starehe kwenye tangazo. Alafu utaskia atachokwambia
 
Ukishakuwa mfanyakazi ni kunyonywa tu πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…