Ukweli wasioupenda Watanganyika au Watanzania Bara

Sasa wewe unaeashindanisha waarabu wa Oman na watanganyika hujasema mzanzibar mweusi kaifanyia nini zanziba mfanya yeye ni wa kupokea tuMsimamo wangu kwenye hili ni kuwa system ya utawala wa ccm umekaa kimagumashi hawataki watoto wetu wajue baadhi ya historia our history has to make us strong lazima ifundishwe kama ilivyo bila kuchakachulia,kama wazaibar wanaudugu wa damu na Oman waachwe lakini pia wana udugu na tanganyika hata sultan akitaka kurudi awe mfalme kama uingereza shughuli za utawa awepo waziri
 
Ina maana yeye kaona wazanzibar ni watu wa kuekezwa tu, wao hawawezi kuwekeza
Anasifia waarabu kuwekeza Zanzibar na kusema watanganyika hawajawekeza Zanzibar, ila hasemi wazanzibar wamewekeza wapi?
Akili zimejaa urojo naacha kula huu mdebwedo.
 
nimezungumza ukweli ambao either utake au usitake, lini mirambo alitoka Tabora akaenda bagamoyo kuuza watumwa?? unaongelea kuhusu kunyoosha kidole kwani mleta mada kasema nini nami nimejibu nini?? Kaongelea kuhusu waarabu nami nimejibu kuhusu waarabu period!!!

sasa ukisoma kwa kukurupuka halafu ukajibu kwa kukurupuka utabaki hivyo hivyo, sina cha kuongeza.


hizo ngozi zote nyeupe hakuna ambae alikuwa na upendo kwa sisi watu weusi, japo kuna wengine ufedhuli wao ulikuwa wa kutisha, lakini yaliyopita si ndwele tusamehe lakini tusisahau na watoto na wajukuu zetu waambiwe ukweli.
 
Niliwahi kwenda stone town nikaona pale watumwa walipokuwa wakihifadhiwa.

Ama kweli waarabu ni watu wema sana.

Waje tu kuwachukua ndugu zao waende nao Oman.
Mleta mada ni Mwarabu wala usijisumbue
 
Mirambo alikwenda pwani kabla ya mwaka 1860 (kama Bagamoyo, sijui). Alipokuwa kijana alishiriki mwenyewe katika biashara ya misafara ya ndovu na watumwa. Baadaye akiwa mtema na kupanusha himaya yake alituma misafara.
Alikuwa na nguvu kwa sababu alikuwa na gobori nyingi kwa rugaruga zake. Hakutengeneza, alinunua. Hapa aliuza meno za ndovu na watumwa ili aweze kupata silaha za kushambulia majirani. Pia alilazimisha misafara kutoka pwani kumlipa ushuru mkali. Hakuweka watumwa huru waliopitishwa katika maeneo yake, aliwatumia kupata ushuru.
Je hii ya "rangi" unamaanisha kweli? Mirambo unamruhusu kuvinda na kuuza watumwa (kwa sababu ya rangi yake), lakini Mwarabu ni mbaya kupita kiasi? Vipi kama tutazame wote kama watendaji wa maovu walioendesha biashara hiyo, kama wauzaji na wanunuzi?
 
Ngoja na mimi nije niwekeze!
 
Utumwa ulikuwa ni mfumo kama ilivyokuwa Ukoloni nk. Watumwa waliuzwa kwanza na jamii au Tawala zao.

Historia ya watu weupe Zanzibar imeanza na Waajemi baadae Wareno na ndipo walipokuja Waarabu. Uwepo wa Waarabu wa Oman ulitokana na kitendo cha Seyyid Said bin Sultan kuhamishia Makao makuu ya Utawala wake Zanzibar.

Tangu hapo biashara kubwa waliofanya ilikuwa ni Kilimo na mauzo ya karafuu. Biashara ya Utumwa ilikuwepo ndiyo lakini haikuwa msingi Mkuu wa uchumi na ilisimamiwa na mawakala na wanufaika Wakuu walikuwa Wazungu waliokuwa na Mashamba makubwa. Oman kipindi hicho ilikuwa nchi maskini kiasi kwamba wakati Utawala wa Seyyid Majid bin Said ulipojitenga na Oman ilibidi Zanzibar iwe inaipa Ruzuku Oman.

Kwa hiyo kuwaona Waarabu wote kama wafanye biashara ya Utumwa si sahihi na ni mwendelezo wa siasa za chuki zisizo na maana.
 

Thanks
 
Tataizo la Zanzibar ni viongozi wao wa CCM, ulaji na maisha yao yanategemea kuwakwao ndani ya chama hicho. Na chama hichi nguvu yake ni bora.
Viongozi hao wamekuwa wakikitumia chama hiki kupata maisha huko Zanzibar, kikitoka tu madarakani nao maisha watakuwa hawana, hivyo kwao muungano ni maisha bila muungano watakufa.
Wapinzani wa kubwa wa kujitegemea kwa Zanzibar ni waba CCM waliopo Zanzibar.
Wazanzibar mtawazuru watanganyika buree, ilhali tatizo lenu ni CCM Zanzibar. Wao ndo uwaita wanajeshi toka bara ili wawasaidie kuwa madarakani huko.
Lijueni tatizo lilipo ili mpate suluhisho sahihi.
Adui yenu ni wana CCM Zanzibar hukohuko
 
Yaani unawatukuza Waarab makatili, na walio wageuza kuwa Watwana wao miaka nenda! Mpaka pale mlipokuja kukombolewa tarehe 12 January 1964 na yule Mgalatia John Okello, mwenye asili ya Uganda!

Wewe aleesha ni Mzanzibari au Muarabu?, tuanzie hapo kwanza...
 
Watanganyika tutakujaje kuwekeza zbar wakati,wanzanzbr wanatubagua!!?, Mtanganyika zbar haruhusiwi kumiliki ardhi , mtanganyika zbar haruhusiwi kuajiriwa ,ondoeni huo ubaguzi uone Kama watanganyika hawajaja kuijenga zbar kuliko hao arabu!
 
Swali gani? Je sio wako Wazanzibari Waafrika, Waarabu, Wahindi - na tangu karne mchanganyiko wa kila aina? Siyo hii ni Zanzibar hasa na sifa yake?
Nimeona ameongelea Wazanzibari na Waarabu, mimi najua ni wote ni Wazanzibari tu labda asili ndio kama ulivyosema.
 
Watanganyika tutakujaje kuwekeza zbar wakati,wanzanzbr wanatubagua!!?, Mtanganyika zbar haruhusiwi kumiliki ardhi , mtanganyika zbar haruhusiwi kuajiriwa ,ondoeni huo ubaguzi uone Kama watanganyika hawajaja kuijenga zbar kuliko hao arabu!

Yaani pori lote lililoko Tanganyika huwezi pata ardhi mpaka uje Zanzibar , punguza kula ugali

 
Waarabu ndio walioleta biashara ya utumwa Znz na Tanganyika hao wazanzibar weusi ndio waliokuepo ni watumwa kipindi cha utumwa.
 
Mimi nakuelewa sana, na tatizo naloliona hutaki kuwataja waznz ambao ndio sehemu ya uharibifu wa znz, hutaki kuwashutumu walevi wa kiunguja na kipemba ambao ni sehemu ya uharibifu wa znz. Kwa mfano chanzo wa kikamatwa mashekhe wa uamsho ni waislam wa znz.

Lkn unawajeshimu kwa sababu ya uznzr wao pamoja ni walevi baadhi yao na kuwakashifu waisalam wa Tanganyika kuwa si lolote zaidi ya utanganyika wao.

Kubwa pemgine una upofu wa kutoelewa chanzo cha tatizo na kuwa na uoni huo finyu.

Nirejee lengo la historia si kuisoma na kujitengenezea chuki. Laa, Bali lengo kubwa la historia ni kujua matatizo na mafanikio ya nyuma ili Mimi na wewe tuweze kuiandika historia mpya itakayosomwa na vizazi.

Sasa hiyo mifano ya majina ya kiislam uliyoitaja waliyoyafanya hatuwezi kuyabadili. Lkn wanayoyafanya sasa sisi tunaweza kuyabadili.

Na ili uweze kubadili kwanza tujue chanzo cha tatizo hadi kuwa wako tayari kushirikiana na waislam wenziwao ambao ni waznz kuwaletea mateso na ukatili kwa waznz wasio na hatia. Je tatizo ni utanganyika.?!?!

Binafsi kwa utafiti mdogo nilioufanya na naoendelea kuufanya naamini tatizo si utanganyika.

Bali Ujamaa. Mwalimu Nyerere ktk maono yake alipata kutamka kuwa ujamaa ni imani. Na kama tunavyojua dini ni imani na hivyo ujamaa ni dini.

Hivyo kauli ya mzee Nyereee hakukurupuka. Kwani asili ya ujamaa ni ukomunist. Na ukomonist ni imani isiyoamini uwepo wa Mungu. Na kwamba wanaamini dini zinatokana na ufinyu wa kufikiri wa mwanadamu. Hivyo kutokana na uanzishwaji na uwepo was imani hii ya ukomonist (ujamaa ). waislam pia waliathiriwa na wanaendelea kuathiriwa na imani hii.

Na ili kukata mzizi was fitna serikali ikapigilia msumari kuwa serikali ya ccm haiamini Mungu na hivyo haiamini dini.

Huu ndio msingi was imani ya Ujamaa.

Kwa hiyo ukiniuliza kwa nini waislam was Tanganyika na wa znz walishiriki uhalifu na bado wanaendelea kushiriki uhalifu kwa jimbo LA znz, nitasema tatizo ni imani ya ujamaa.

Iliyowalevya na kuutumikia ujamaa zaidi kuliko imani ya asili yao (uislam) na kuwaona wapinga ujamaa na wasioshiriki imani ya ujamaa ni maadui zaidi kuliko watu wengine.

Sasa kama nawe uko ktk chama. Na misingi ya chama hicho ni itikadi ya ujamaa. Wewe nawe utaendelea kuwaona waislam wa Tanganyika ni maadui kwenu.

Kinyume chake tunaweza kuandika historia mpya. Kwa kuikataa itikadi ya kijamaa.

Kama kuna maeneo ndani ya znz ambapo muislam mtanganyika hawezi kupewa mke kwasababu yeye ni mtamganyika wao pia wameathiriwa na itikadi ya ujamaa.

Kwa kifupi ujamaa umeshindwa na ni adui yetu namba 1 tunaepaswa tumuondoe.

Tunaweza kuishi bila ujamaa kama ndio msingi wa itikadi yetu, pia tunaweza kuishi bila ubepari kuwa ni msingi wa itikadi yetu pale watu wema watakapoamua kushiriki siasa. Na kuanchana na wahuni na wajamaa watuongoze.

Watu wema wapo tz bila kujali imani wetu. Kwani ktk ulimwengu huu ambapo kuna makundi ya watu wenye mchanganyiko wa utamaduni na imani huwezi kujifungia na kudhani utaweza kuishi na watu wenye imani yako pekee. Huku bara hata baadhi ya misikiti inaajiri walimzi wa viatu wa imani nyengine. Maadamu hatuwashinikizi waamini tunayoyaamini sisi, wala wao hawatulazimishi tuamini wanayoyaamini wao.

Nimalizie kwa maneno machache ya kimombo yanayitofautisha aina za watu hapa duniani.
1. Kundi la Whats happen
2. Lets happen
3. Makes happen.

Kundi no 1. Linakuhusu unapemda kufatilia nini kimetokea.

Kundi no 2 ndio watz wengi wengine na hasa waswahili wao ni hewawa wacha yatokee.

Kundi no 3 wako wachache, wao wanataka kutengeza historia mpya. Ndugu yangu napenda ubadili ubongo wako ufikiri kama wanavyofikir Kundi la 3.

Kinyume chake nitakuweka ktkt kundi lililotengenezwa hadi kuzuzuka.

Nini maoni yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…