Ni kweli maneno yako siwezi kubadili historia lakini la kusikitisha historia tunaiona inajirudia kila baada ya miaka mitano . Tunawaona akina Mahita , Kikwete, Mwinyi nk.wanavyotufanyia . Sio wote lakini wengi wako hivyo . Wako wachache sana akina Ponda vitendo vyao tunaviona vya kupigania haki , na hao walipigwa risasi na kuwekwa jela na hao viongozi wa Kiislamu. Hayo mapenzi ni povu la mdomo na hapa kwenye kioo. ACTIONS SPEAK LOUDER THAN WORDS
Mimi nakuelewa sana, na tatizo naloliona hutaki kuwataja waznz ambao ndio sehemu ya uharibifu wa znz, hutaki kuwashutumu walevi wa kiunguja na kipemba ambao ni sehemu ya uharibifu wa znz. Kwa mfano chanzo wa kikamatwa mashekhe wa uamsho ni waislam wa znz.
Lkn unawajeshimu kwa sababu ya uznzr wao pamoja ni walevi baadhi yao na kuwakashifu waisalam wa Tanganyika kuwa si lolote zaidi ya utanganyika wao.
Kubwa pemgine una upofu wa kutoelewa chanzo cha tatizo na kuwa na uoni huo finyu.
Nirejee lengo la historia si kuisoma na kujitengenezea chuki. Laa, Bali lengo kubwa la historia ni kujua matatizo na mafanikio ya nyuma ili Mimi na wewe tuweze kuiandika historia mpya itakayosomwa na vizazi.
Sasa hiyo mifano ya majina ya kiislam uliyoitaja waliyoyafanya hatuwezi kuyabadili. Lkn wanayoyafanya sasa sisi tunaweza kuyabadili.
Na ili uweze kubadili kwanza tujue chanzo cha tatizo hadi kuwa wako tayari kushirikiana na waislam wenziwao ambao ni waznz kuwaletea mateso na ukatili kwa waznz wasio na hatia. Je tatizo ni utanganyika.?!?!
Binafsi kwa utafiti mdogo nilioufanya na naoendelea kuufanya naamini tatizo si utanganyika.
Bali Ujamaa. Mwalimu Nyerere ktk maono yake alipata kutamka kuwa ujamaa ni imani. Na kama tunavyojua dini ni imani na hivyo ujamaa ni dini.
Hivyo kauli ya mzee Nyereee hakukurupuka. Kwani asili ya ujamaa ni ukomunist. Na ukomonist ni imani isiyoamini uwepo wa Mungu. Na kwamba wanaamini dini zinatokana na ufinyu wa kufikiri wa mwanadamu. Hivyo kutokana na uanzishwaji na uwepo was imani hii ya ukomonist (ujamaa ). waislam pia waliathiriwa na wanaendelea kuathiriwa na imani hii.
Na ili kukata mzizi was fitna serikali ikapigilia msumari kuwa serikali ya ccm haiamini Mungu na hivyo haiamini dini.
Huu ndio msingi was imani ya Ujamaa.
Kwa hiyo ukiniuliza kwa nini waislam was Tanganyika na wa znz walishiriki uhalifu na bado wanaendelea kushiriki uhalifu kwa jimbo LA znz, nitasema tatizo ni imani ya ujamaa.
Iliyowalevya na kuutumikia ujamaa zaidi kuliko imani ya asili yao (uislam) na kuwaona wapinga ujamaa na wasioshiriki imani ya ujamaa ni maadui zaidi kuliko watu wengine.
Sasa kama nawe uko ktk chama. Na misingi ya chama hicho ni itikadi ya ujamaa. Wewe nawe utaendelea kuwaona waislam wa Tanganyika ni maadui kwenu.
Kinyume chake tunaweza kuandika historia mpya. Kwa kuikataa itikadi ya kijamaa.
Kama kuna maeneo ndani ya znz ambapo muislam mtanganyika hawezi kupewa mke kwasababu yeye ni mtamganyika wao pia wameathiriwa na itikadi ya ujamaa.
Kwa kifupi ujamaa umeshindwa na ni adui yetu namba 1 tunaepaswa tumuondoe.
Tunaweza kuishi bila ujamaa kama ndio msingi wa itikadi yetu, pia tunaweza kuishi bila ubepari kuwa ni msingi wa itikadi yetu pale watu wema watakapoamua kushiriki siasa. Na kuanchana na wahuni na wajamaa watuongoze.
Watu wema wapo tz bila kujali imani wetu. Kwani ktk ulimwengu huu ambapo kuna makundi ya watu wenye mchanganyiko wa utamaduni na imani huwezi kujifungia na kudhani utaweza kuishi na watu wenye imani yako pekee. Huku bara hata baadhi ya misikiti inaajiri walimzi wa viatu wa imani nyengine. Maadamu hatuwashinikizi waamini tunayoyaamini sisi, wala wao hawatulazimishi tuamini wanayoyaamini wao.
Nimalizie kwa maneno machache ya kimombo yanayitofautisha aina za watu hapa duniani.
1. Kundi la Whats happen
2. Lets happen
3. Makes happen.
Kundi no 1. Linakuhusu unapemda kufatilia nini kimetokea.
Kundi no 2 ndio watz wengi wengine na hasa waswahili wao ni hewawa wacha yatokee.
Kundi no 3 wako wachache, wao wanataka kutengeza historia mpya. Ndugu yangu napenda ubadili ubongo wako ufikiri kama wanavyofikir Kundi la 3.
Kinyume chake nitakuweka ktkt kundi lililotengenezwa hadi kuzuzuka.
Nini maoni yako.