Ulazima wa Kiingereza cha Rais Samia ziarani nchini Kenya

Haya, njooni muone huyu ndondocha wa mabeberu.
 
Nami ntamwona kama limbukeni, kama ataogopa kuzungumza Kiswahili.

Hiyo itakuwa dalili ya kwanza kabisa kwamba mama anayo matatizo ya kujiona kuwa yeye na watu wake ni duni mbele ya hao anaowatembelea.
Atajiaibisha sana na vizungu vyake vya kusoma.

Mtu unashindwa kujiamini na lugha yako unakimbilia kusoma lugha za kitumwa kwenye karatasi!

Ni upungufu wa akili tu!
 
Rais wao pia kila akitutembelea anatumia Kiswahili..ata msiban aliongea Kiswahili vizuri Sana kuliko baadhi ya mawaziri wetu
Uhuru Kenyatta hata akiwa Kenya anaongea Kiswahili vile vile!

Ni ajabu sana mwenyeji wake aongee Kiswahili halafu yeye mswahili aanze kutusomea vizungu vya kwenye makaratasi!

Ni kituko!
 
Hakika.

Itakuwa ni maajabu aanze kusoma viingereza vya kuandikiwa!

Kwa kweli atashangaza!
 
Kwanza umepotosha Mama Samia hana uwezo was kuhutubia kwa kizungu,hana na hata kuja kuwa nao.
Alisoma hutuba kwa kizungu,hakuhutubia.
 
Kwanza umepotosha Mama Samia hana uwezo was kuhutubia kwa kizungu,hana na hata kuja kuwa nao.
Alisoma hutuba kwa kizungu,hakuhutubia.
Aisee hii ni kweli.

Nimeangalia namna Obama alivyohutubia Bunge la Uingereza — Jamaa lina ufundi wa ajabu wa kuzungumza.

Huyu Bibi Sasha akianza kutusomea vizungu vya kwenye makaratasi, kwa tunaotambua nini maana ya kuhutubia, ni Kero kusikiliza.

Kwanini asihutubie Kwa Kiswahili?

Naamini yeye ni gwiji wa Kiswahili na ana uwezo wa kutupa ile ladha sahihi ya hotuba.
 
Kwanza umepotosha Mama Samia hana uwezo was kuhutubia kwa kizungu,hana na hata kuja kuwa nao.
Alisoma hutuba kwa kizungu,hakuhutubia.
Kusoma si shida as long as aliweza kujua right pronounciation ya maneno kwenye hotuba then she is good....aendelee hivohivo.....

kusoma hotuba ya kiingereza kwa ufasaha kuanzia muktadha body language, na utamkaji wa maneno sio rahisi haya kidogo....she deserve praise on that.
 
mm sina pressure,mama apige yeyote atakayejisikia, ila kwa ushauri wangu apige kiswahili kwa vile wakenya wanakijua kiswahili, Dunia ya kingereza ni kubwa tutapiga tukienda safari ya huko europe.
 
Kwanza umepotosha Mama Samia hana uwezo was kuhutubia kwa kizungu,hana na hata kuja kuwa nao.
Alisoma hutuba kwa kizungu,hakuhutubia.

..anatakiwa aandikiwe HOTUBA nzuri ya kuwasilisha mbele ya wenyeji wake.

..wasaidizi wanatakiwa wamuandae Raisi ili kuhakikisha hazungumzi jambo lolote nje ya ujumbe ambao umekusudiwa ktk ziara yake.

..Wazungu wanaita " staying on the message. " Yaani kuhakikisha kiongozi ana nidhamu ktk mazungumzo wakati wa ziara.

..mahali ambapo anaweza kuzungumza bila kutumia taarifa / notes / hotuba iliyoandaliwa ni ktk mkutano na waandishi wa habari.

..
 

..anatakiwa afanye practice / mazoezi.

..anatakiwa awe anaijua hotuba yake na siyo kukurupuka na kuisoma.

..hata viongozi wakubwa duniani hufanya mazoezi ya hotuba zao muhimu kabla ya kwenda kuhutubia ktk hadhira iliyokusudiwa.

..practice, practice, practice.

Cc Nguruvi3
 
Hii lugha ya kiswahili haina soko. Kwasabb ilipaswa kubeba teknolojia/maarifa ambayo ndiyo yangevutia watu kujifunza kiswahili
Fanya utafiti ujifunze,usipende kukalilishwa vitu visivyo na tija,kuna nchi nyingi hazitumii kiingereza,zinaumia lugha zao za ASILI,lkn ziko vzr,hivyo hoja yako ni mfu,
 
Kwanini mtu anaetumia kingereza anapigwa sana vita na watu wanatumia kiswahili? Ni dhambi kutumia kingereza? Kwanza asilimia kubwa ya watanzania wamehitimu kidato cha nne kwahiyo nina imani kingereza mnakijua vizuri. Mama ataamua mwenyewe kutumia lugha atakayoona inamfaa kwa mazingira atakayokuwepo.


Ushauri: huwezi kukuza kiswahili kwa kukichukia kingereza.
 
Siyo kizungu.Kiingereza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…