Ulazima wa Kiingereza cha Rais Samia ziarani nchini Kenya

Ulazima wa Kiingereza cha Rais Samia ziarani nchini Kenya

Mkuu Chige , nadhani ziara ya SSH nchini Kenya haina lengo la kuongea na wakenya kama mleta mada anavyodhani. Mama ana nia na jukumu la kupata platform nzuri ya kuelezea ninsi alivyo tofati na mtangulizi wake katika nyanja za biashara, uchumi na uwekezaji. Bila shaka ziara hiyo ni platform tu ya mama kuongea na mabeberu kujaribu ku-restore sintofahamu ya miaka takribani 6 ya mtangulizi wake. Kenya ni spika nzuri kwa wanaoitwa investors aka Mabeberu as wengi wao wamepafanya kama base ya shughuli kwa East Africa.
Media za Kenya zinasomwa na jumuiya kubwa ya kimataifa ukilinganisha na TZ, hivyo kwa vyovyote vile ili kuleta message ya moja kwa moja, inampasa na naamini mama aongee kiingereza. Clear message inahitajika hapa. Kamwe tusidhani ziara ya Mama ni ya kuongea na watu wa kibere kama mtoa mada anavyodhani. Is purely strategic visit.
Haya, njooni muone huyu ndondocha wa mabeberu.
 
Nami ntamwona kama limbukeni, kama ataogopa kuzungumza Kiswahili.

Hiyo itakuwa dalili ya kwanza kabisa kwamba mama anayo matatizo ya kujiona kuwa yeye na watu wake ni duni mbele ya hao anaowatembelea.
Atajiaibisha sana na vizungu vyake vya kusoma.

Mtu unashindwa kujiamini na lugha yako unakimbilia kusoma lugha za kitumwa kwenye karatasi!

Ni upungufu wa akili tu!
 
Rais wao pia kila akitutembelea anatumia Kiswahili..ata msiban aliongea Kiswahili vizuri Sana kuliko baadhi ya mawaziri wetu
Uhuru Kenyatta hata akiwa Kenya anaongea Kiswahili vile vile!

Ni ajabu sana mwenyeji wake aongee Kiswahili halafu yeye mswahili aanze kutusomea vizungu vya kwenye makaratasi!

Ni kituko!
 
Asilia mia zaidi ya 80 ya mawasiliano Kenya ni kiswahili.Mfano mzuri ni mikutano yote ya siasa lugha inayotumika kiswahili ,mitaani ni kiswahili pia.Hii dhana Kenya ni Kiengereza tuu ni upotoshaji mkubwa. Mama ni vizuri kuongea kiswahili ziarani Kenya.
Hakika.

Itakuwa ni maajabu aanze kusoma viingereza vya kuandikiwa!

Kwa kweli atashangaza!
 
Kwanza umepotosha Mama Samia hana uwezo was kuhutubia kwa kizungu,hana na hata kuja kuwa nao.
Alisoma hutuba kwa kizungu,hakuhutubia.
 
Kwanza umepotosha Mama Samia hana uwezo was kuhutubia kwa kizungu,hana na hata kuja kuwa nao.
Alisoma hutuba kwa kizungu,hakuhutubia.
Aisee hii ni kweli.

Nimeangalia namna Obama alivyohutubia Bunge la Uingereza — Jamaa lina ufundi wa ajabu wa kuzungumza.

Huyu Bibi Sasha akianza kutusomea vizungu vya kwenye makaratasi, kwa tunaotambua nini maana ya kuhutubia, ni Kero kusikiliza.

Kwanini asihutubie Kwa Kiswahili?

Naamini yeye ni gwiji wa Kiswahili na ana uwezo wa kutupa ile ladha sahihi ya hotuba.
 
Kwanza umepotosha Mama Samia hana uwezo was kuhutubia kwa kizungu,hana na hata kuja kuwa nao.
Alisoma hutuba kwa kizungu,hakuhutubia.
Kusoma si shida as long as aliweza kujua right pronounciation ya maneno kwenye hotuba then she is good....aendelee hivohivo.....

kusoma hotuba ya kiingereza kwa ufasaha kuanzia muktadha body language, na utamkaji wa maneno sio rahisi haya kidogo....she deserve praise on that.
 
mm sina pressure,mama apige yeyote atakayejisikia, ila kwa ushauri wangu apige kiswahili kwa vile wakenya wanakijua kiswahili, Dunia ya kingereza ni kubwa tutapiga tukienda safari ya huko europe.
 
Kwanza umepotosha Mama Samia hana uwezo was kuhutubia kwa kizungu,hana na hata kuja kuwa nao.
Alisoma hutuba kwa kizungu,hakuhutubia.

..anatakiwa aandikiwe HOTUBA nzuri ya kuwasilisha mbele ya wenyeji wake.

..wasaidizi wanatakiwa wamuandae Raisi ili kuhakikisha hazungumzi jambo lolote nje ya ujumbe ambao umekusudiwa ktk ziara yake.

..Wazungu wanaita " staying on the message. " Yaani kuhakikisha kiongozi ana nidhamu ktk mazungumzo wakati wa ziara.

..mahali ambapo anaweza kuzungumza bila kutumia taarifa / notes / hotuba iliyoandaliwa ni ktk mkutano na waandishi wa habari.

..
 
Kusoma si shida as long as aliweza kujua right pronounciation ya maneno kwenye hotuba then she is good....aendelee hivohivo.....

kusoma hotuba ya kiingereza kwa ufasaha kuanzia muktadha body language, na utamkaji wa maneno sio rahisi haya kidogo....she deserve praise on that.

..anatakiwa afanye practice / mazoezi.

..anatakiwa awe anaijua hotuba yake na siyo kukurupuka na kuisoma.

..hata viongozi wakubwa duniani hufanya mazoezi ya hotuba zao muhimu kabla ya kwenda kuhutubia ktk hadhira iliyokusudiwa.

..practice, practice, practice.

Cc Nguruvi3
 
Hii lugha ya kiswahili haina soko. Kwasabb ilipaswa kubeba teknolojia/maarifa ambayo ndiyo yangevutia watu kujifunza kiswahili
Fanya utafiti ujifunze,usipende kukalilishwa vitu visivyo na tija,kuna nchi nyingi hazitumii kiingereza,zinaumia lugha zao za ASILI,lkn ziko vzr,hivyo hoja yako ni mfu,
 
Tumesikia Rais Samia anaenda Kenya kwa ziara ya kikazi mnamo hapo kesho.

Ni matumaini yangu na fahari yangu kwamba, atatumia Kiswahili katika shughuli zote atakazoalikwa kuzifanya.

Hivi majuzi tu alipoenda Uganda, tuliona anatumia kizungu kuhutubia.

Wengi wa wananchi wetu nina uhakika hawakuelewa hata anachozungumza.

Ifahamike kwamba, Kiswahili si lugha ngeni Afrika Mashariki. Tuachane na Viingereza pasipo na ulazima.

Sijui ni nani aliyewalaghai kwamba kuongea kizungu ni ufahari na usomi?

Hata katika mazingira yasiyohitaji kizungu, bado watu watajing'ang'aniza kuongea kizungu hata kama hawakiwezi na tunajua kwa hakika kwamba hawakiwezi.

Hebu tuachane na hizi "You Know You know ofcozi zea zea" mingi mingi. Tunajiaibisha na kujidunisha.

Tunayo lugha adhimu ya Kiswahili. Tuitumie hiyo.

Nasubiri kuona hiyo Kesho vile Bibi SASHA atakavyojitutumua na viingereza vyake uchwara.

Ashauriwe vyema. Maana shughuli za aina ile sio mahali pa kuonesha mbwembwe za kuzungumza kwa lafudhi bandia za kimalkia.

Tunahitaji kusikia "maswala" yakijadiliwa na kuzungumzwa. Hatuhitaji mikogo ya lafudhi bandia za Kizungu.
Kwanini mtu anaetumia kingereza anapigwa sana vita na watu wanatumia kiswahili? Ni dhambi kutumia kingereza? Kwanza asilimia kubwa ya watanzania wamehitimu kidato cha nne kwahiyo nina imani kingereza mnakijua vizuri. Mama ataamua mwenyewe kutumia lugha atakayoona inamfaa kwa mazingira atakayokuwepo.

Ushauri: huwezi kukuza kiswahili kwa kukichukia kingereza.
 
Tumesikia Rais Samia anaenda Kenya kwa ziara ya kikazi mnamo hapo kesho.

Ni matumaini yangu na fahari yangu kwamba, atatumia Kiswahili katika shughuli zote atakazoalikwa kuzifanya.

Hivi majuzi tu alipoenda Uganda, tuliona anatumia kizungu kuhutubia.

Wengi wa wananchi wetu nina uhakika hawakuelewa hata anachozungumza.

Ifahamike kwamba, Kiswahili si lugha ngeni Afrika Mashariki. Tuachane na Viingereza pasipo na ulazima.

Sijui ni nani aliyewalaghai kwamba kuongea kizungu ni ufahari na usomi?

Hata katika mazingira yasiyohitaji kizungu, bado watu watajing'ang'aniza kuongea kizungu hata kama hawakiwezi na tunajua kwa hakika kwamba hawakiwezi.

Hebu tuachane na hizi "You Know You know ofcozi zea zea" mingi mingi. Tunajiaibisha na kujidunisha.

Tunayo lugha adhimu ya Kiswahili. Tuitumie hiyo.

Nasubiri kuona hiyo Kesho vile Bibi SASHA atakavyojitutumua na viingereza vyake uchwara.

Ashauriwe vyema. Maana shughuli za aina ile sio mahali pa kuonesha mbwembwe za kuzungumza kwa lafudhi bandia za kimalkia.

Tunahitaji kusikia "maswala" yakijadiliwa na kuzungumzwa. Hatuhitaji mikogo ya lafudhi bandia za Kizungu.
Siyo kizungu.Kiingereza.
 
Back
Top Bottom