Ulichoma mtaji mara ngapi mpaka kuja kutoboa kibiashara?

Umeandika fasta fasta mnoo. Lakini unaonekana unapenda faida ionekane biashara inapoanza. Hapa lazima ulie sana, utalia mbaka ubadilike mwnyw
 
Ungekaza hapo kwenye "transportation /logistics" na kwenye "kilimo" ndipo sehemu sahihi zaidi kwa mazingira ya Tanzania
 
Na mm nipitisheni kwenye huo ulimwengu wa roho
 
Hapa la kujifunza ni kusimamia biashara yako mwenyewe...biashara zako zilikuwa kwa kuamin watu na kuwaachia waendeshe...pole
 
Waathirika wa biashara za kufanya muda mfupi na kudhani utapata faida kubwa ni Watumishi wa Serikali au Wafanyakazi wa Serikali hasa Wastaafu. Mtu hajawahi kufanya biashara akipata mafao anavamia kufanya biashara fulani au hata kilimo cha mazao fulani baada ya miaka 2 anaandika historia ya kufeli. Inatakiwa akiwa amebakiza miaka 5 kabla ya kustaafu inabidi aanze kufanya biashara au kilimo au kuuza mazao ya kilimo halafu atakuwa anajifunza pole pole maeneo anayokumbana na changamoto za shughuli husika. Akija kustaafu anakuwa tayari ana uhakika wa shughuli ya kufanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…