Ulichoma mtaji mara ngapi mpaka kuja kutoboa kibiashara?

Mwezi wa 8 nimenunua mashine ya kubirigua magogo nikaingia chimbo kilichonikuta huko porini... Zaidi ya mil6 zilizama najionea, nimekaa miezi miwili porini narudi mjini sina kitu na mtaji wangu nimechoma. sitousahau mwaka huu
Pole kiongozi. Watu ambao hawajawahi kufanya biashara ukiwaambia 6m inateketea na hupati hata mia hawaamini!
 
Nakumbuka kuna center moja nilikamata sehemu. Kila mtu ananiambia daah hapa mwanangu umeula kwa eneo hili utapiga business mpaka uchoke. Weee..! [emoji3] Mbata! Mbata! Kofi! Teke! Mtamaa..! Kichwa chini miguu juu hata miezi 6 haikuisha dadek[emoji1]
,[emoji23][emoji23][emoji23]
 
".... Na kukimbia biashara kabla hujaizoea.
Mkuu hatukimbii kwa kupenda, unalazimika kutoka nduki! We imagine mimi kuna wakati nilikua na mgahawa, asubuhi mnanunua kila kitu kwa 200,000 ikifika jioni kufunga mahesabu unakuta kila kitu kimeisha na mmepata 150,000. Hapo una vijana kama wanne wanasubiria ujira na kesho kunatakiwa hela ya sokoni kufuata mahitaji! Kwanini usivizie watu wakiondoka unakunja majiko yako unatia mfukoni na kutoka nduki kali...???πŸ˜„πŸ˜„
 
Acha tu mkuu. Mimi hua nawaangalia watu wanaosema hii hela kuliko ufanyie kitu fulani bora uweke kwenye biashara chap uzungushe ukipata faida ndio ufanye. Nasema hiiii...[emoji3]
Si ndo hapo sasa! Eti kuna aliyeleta uzi humu eti wenye nyumba wengi ni masikini eti badala wafanye biashara kwanza ndo wajenge eti wanajenga kwanza pesa zinaisha wanabaki masikini.
 
Halafu mara nyingi hela ikishaisha ndio hua unaanza kupata akili ya mambo ambayo kama ungeyafanya ungepiga hatua
 
Ulikuwa unabadili biashara kila baada ya miaka mingapi?
 
Itakuwa ulikuwa unakosea padogo
 
Mzee una moyo....utafanikiwa.....mzgo wte huo na bdo unataka kurudi tena hukohuko???? Ww kiboko, nadhani mahustla wadogo tunachakujfunza kwako hapo mkuu....hongera snaa kwa hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…