Ulichoma mtaji mara ngapi mpaka kuja kutoboa kibiashara?

Ulichoma mtaji mara ngapi mpaka kuja kutoboa kibiashara?

Mwezi wa 8 nimenunua mashine ya kubirigua magogo nikaingia chimbo kilichonikuta huko porini... Zaidi ya mil6 zilizama najionea, nimekaa miezi miwili porini narudi mjini sina kitu na mtaji wangu nimechoma. sitousahau mwaka huu
Pole kiongozi. Watu ambao hawajawahi kufanya biashara ukiwaambia 6m inateketea na hupati hata mia hawaamini!
 
Nakumbuka kuna center moja nilikamata sehemu. Kila mtu ananiambia daah hapa mwanangu umeula kwa eneo hili utapiga business mpaka uchoke. Weee..! [emoji3] Mbata! Mbata! Kofi! Teke! Mtamaa..! Kichwa chini miguu juu hata miezi 6 haikuisha dadek[emoji1]
,[emoji23][emoji23][emoji23]
 
".... Na kukimbia biashara kabla hujaizoea.
Mkuu hatukimbii kwa kupenda, unalazimika kutoka nduki! We imagine mimi kuna wakati nilikua na mgahawa, asubuhi mnanunua kila kitu kwa 200,000 ikifika jioni kufunga mahesabu unakuta kila kitu kimeisha na mmepata 150,000. Hapo una vijana kama wanne wanasubiria ujira na kesho kunatakiwa hela ya sokoni kufuata mahitaji! Kwanini usivizie watu wakiondoka unakunja majiko yako unatia mfukoni na kutoka nduki kali...???😄😄
 
Acha tu mkuu. Mimi hua nawaangalia watu wanaosema hii hela kuliko ufanyie kitu fulani bora uweke kwenye biashara chap uzungushe ukipata faida ndio ufanye. Nasema hiiii...[emoji3]
Si ndo hapo sasa! Eti kuna aliyeleta uzi humu eti wenye nyumba wengi ni masikini eti badala wafanye biashara kwanza ndo wajenge eti wanajenga kwanza pesa zinaisha wanabaki masikini.
 
Acha kabisa mkuu. Nimechoma milioni 80 kwenye dhahabu. Imeniacha mbendembende. Daah...! Bahati mbaya napoteza hela na umri ndio umeenda 40+.

Nimegundua ndio maana wakinga wakishika biashara moja ya duka ni hiyo hiyo hawabadiriki.

Hivi najitafuta kwa upya. Duka nililipukutisha kuingiza kwenye dhahabu. Hivi ndio napambania kulirudishia. Bidhaa sina japo biashara ipo. Hapa ili nirudi sawa natakiwa angalau milioni 40 kwa uchache 20 mpya niitupie humo.

Ila unajua nini? Lazima niyarudie madini yanipe hela.
Halafu mara nyingi hela ikishaisha ndio hua unaanza kupata akili ya mambo ambayo kama ungeyafanya ungepiga hatua
 
Mtu akikuona leo hii unavyokula bata, maisha mazuri, usafiri mkali na biashara kubwa mjini, anaweza kudhani umefika hapo ulipo kirahisi rahisi tuu. Mimi mwenyewe nilikua nadhani hivyo!

Cha ajabu ni kwamba kila ninapojaribu kutia mguu kwenye biashara nachezea za uso mbaya kabisa najikuta natoka kapa. Mpaka muda huu nimeshajaribu zaidi ya aina 5 tofauti za biashara kuanzia bar, stationary, usafirishaji, kilimo, ufugaji nk na zote hakuna hata moja iliyofanikiwa walau hata kurudisha mtaji!

Nimebaki najiuliza nyie wenzetu mliofanikiwa kutoboa kibiashara je na nyie mwanzo mlichoma mitaji kama sisi? Hebu tupeni akili na sisi tutoboe.

NB: Usije na hoja za "fanya kazi kwa bidii".
Ulikuwa unabadili biashara kila baada ya miaka mingapi?
 
Mkuu hatukimbii kwa kupenda, unalazimika kutoka nduki! We imagine mimi kuna wakati nilikua na mgahawa, asubuhi mnanunua kila kitu kwa 200,000 ikifika jioni kufunga mahesabu unakuta kila kitu kimeisha na mmepata 150,000. Hapo una vijana kama wanne wanasubiria ujira na kesho kunatakiwa hela ya sokoni kufuata mahitaji! Kwanini usivizie watu wakiondoka unakunja majiko yako unatia mfukoni na kutoka nduki kali...???😄😄
Itakuwa ulikuwa unakosea padogo
 
Acha kabisa mkuu. Nimechoma milioni 80 kwenye dhahabu. Imeniacha mbendembende. Daah...! Bahati mbaya napoteza hela na umri ndio umeenda 40+.

Nimegundua ndio maana wakinga wakishika biashara moja ya duka ni hiyo hiyo hawabadiriki.

Hivi najitafuta kwa upya. Duka nililipukutisha kuingiza kwenye dhahabu. Hivi ndio napambania kulirudishia. Bidhaa sina japo biashara ipo. Hapa ili nirudi sawa natakiwa angalau milioni 40 kwa uchache 20 mpya niitupie humo.

Ila unajua nini? Lazima niyarudie madini yanipe hela.
Mzee una moyo....utafanikiwa.....mzgo wte huo na bdo unataka kurudi tena hukohuko???? Ww kiboko, nadhani mahustla wadogo tunachakujfunza kwako hapo mkuu....hongera snaa kwa hilo
 
Back
Top Bottom