Ulichoma mtaji mara ngapi mpaka kuja kutoboa kibiashara?

Ulichoma mtaji mara ngapi mpaka kuja kutoboa kibiashara?

Kuna sehemu nilikuwa nafanya kazi nikapata kama million 8 baada ya kuchukua mafao yangu NSSF na akiba yangu nikanunua kiwanja nikajenga banda la mpira lilikuwa linaenda vizuri tu ila kutokana na majukumu nikamuachia mtu aendeshe likamshinda ikabidi nikubali matokeo nikaenda zanzibar kuchukua mzigo kama TV used fridge pasi heater nakadhalika kwasababu nilikuwa bize sana na kazi nikamwachia mtu aendeshe akaniibia nikamtimua nikafunga biashara kwa hyo ile million 8 ikapotea kwa style hyo nimeambulia kiwanja tu ila nimejifunza vitu vingi sana sasa hivi najipanga kuja kivingine nianze upya na projects mpya I hope I will succeed next time.
 
JF ninayoijua.

Well documented mkuu 👍🏾
Chukua muda kujifunza na pia uwe na uvumilivu.

Biashara yoyote mpya matarajio ya kupata faida iwe baada ya miaka 2, kwa maana ya kupata muda mzuri wa kulisoma soko na kujifunza changamoto mbalimbali na namna ya kukabiliana nazo.

Ukitaka mafanikio ya haraka hamna biashara ya namna hiyo labda wizi.

Lazima uanguke ili usimame imara.

Biashara umefanya kidogo huoni muelekeo unakimbilia nyingine, hayo unayokimbia unatakiwa uyakabili na ujifunze ili kuyashinda.

Kwaheri.
JF ninayoijua

Well documented mkuu
 
boss miti inadondoshwa zinachanwa mbao undersize... yan si za kuuza ni kwa ajiri ya kutengeneza mizinga ya nyuki. mwisho wa siku sikufikia malengo na pesa nimeshachoma
Ulimbia mchezon mapema sana, issue s ilikua kukata mti mwingine tu uchane size unayotaka ? Au

Lililo kupata ni sehem ya kujifunza , hujachoma pesa
 
Nimechoma hela kwenye biashara

1.Mtumba
2.pembe Za ng’ombe
3.Kilimo
4.forex
5.Chakula
6.Samaki&Kuku


Mpaka nimekuja kusettle kwenye cosmetics na hapa nimesettle in a very hard way.. Yaani nilichojifunza
Kwenye biashara kuna muda inabidi ujitahidi kuforce sana mambo na kusimamia biashara mwenyewe

Usiachie mtu biashara yako.
Usiweke mtaji wote kabla haujausoma mchezo.
Kubali kuwa mjinga jifunze kwa watangulizi.
Kuwa na nidhamu ya Pesa.

Kupitia haya angalau biashara inaweza kusimama na kukua.
Hii cosmetics mpewe maua yenu walai, nilijifunza kwenu , mwaka wa pili na kitu sasa , biashara imesimama mie niko porini natafuta shilingi kwenye kilimo na ufugaj, pesa inatoka kwenye cosmetics huko huko
 
Nina ndugu yangu analipa madeni (uzuri ni mfanyakazi wa serikali) sababu ya Hii biashara ya madini

Bahati mbaya yeye aliingizia na ushirikina, mganga akalamba hela na shimo likalamba pesa

Siyo mchezo..

Pole sana utainuka tu pambana.
Daaah...! Dhahabu hatari sana jamaa yangu. Hapa kichwa kimevurugika. Najikaza tu uanaume ila nina strees za kufa mtu. Nikivuka Salama mpaka mwaka 2025 nitamshukuru MUNGU sana
 
Nyie Nyie binaadamu?[emoji119]

Yupo nilimfundisha kila kitu na amekua my no one Enemy!

Yeye ndo amekua anapambana na mimi kupitia migongo ya watu wengine,
Ndo maana matajiri hawataki ukaribu na maskini..
Hiyo ni wengi sana wako hivyo. Unamtoa chini baadae anakuwa adui yako namba moja. Waafrika sio kabisa
 
jamaa akanikoki ukiwa na chainsaw mizinga ya mabox ni rahisi kuchonga tena kiwepesi... Ltrs20 ya petrol inachana mbao 700. Bwn bwn nikaona utajiri si huu hapa... Kumbe bhn si kwel yule mshenz alikuwa na lengo lake maalum
Yaani kuna wakati mtu ukikaa ukikumbuka jinsi ulivyochoma pesa unaishia kucheka badala ya kuhuzunika.😀 Na kuna watu ni wataalamu kwenye kuchochea wenzao wafanye vitu ambavyo wenyewe hawavifanyi au vilishawashinda..
 
Back
Top Bottom