Mkubwa
Grahams na
Shadow7,
Madame B semeni Jambo.
Ilikuwa ni moment nzuri sana Kwa kweli
Baada ya kupima na kujua mwenzangu alikuwa Mjamzito Kwa mara ya kwanza, nilihakikisha natumia resources zote kumtunza na kuhakikisha anakula mlo kamili Kila Siku
Nilihakikisha namtunza vizuri Mama Kijacho pamoja na mtoto mwenyewe iwapo atazaliwa salama
Ilikuwa sitaki apate tatizo lolote wakati wote wa ujauzito wake, na yeye alikuwa anadeka hadi basi (unaweza kuwa Kazini, mwenzio anakupigia simu eti mtoto(mimba) amemisi kusikia sauti yako hivyo anaomba niongee naye)
Ujauzito huwa unakuja na mabadiriko ya mwili wakati mwingine na tabia Kwa Mwanamke ama Kwa Baba husika (Baba Kijacho)
Binafsi nilikuwa nahisi kichefuchefu wakati wote Waifu alipokuwa Mjamzito hadi kilipokoma baada ya yeye kujifungua 🙌
Mama Kija wangu, yeye alikuwa Mpenzi sana wa Kitimoto na Soda ya Pepsi
Kwahiyo nilimwekea Bili Kwa Mangi kwaajili ya kula Kila Siku
Soda nilikuwa nanua Kreti la Pepsi Kila baada ya Siku 4 maana alikuwa na wastani wa kunywa Chupa 5 hadi 6 Kwa Siku 🙌
Baada ya miezi 9 alijifungua mtoto wa Kiume mwenye Afya tele
Ilikuwa ni kama naota kupewa taarifa zile na Daktari, maana kusema kweli Wanaume wengi hupenda kupata Watoto wa Kiume kwenye Uzao wetu
Kutokea hapo nikawa nawahi kutoka Kazini Kila Siku hata kama ni Kwa kutoroka ili niweze kwenda kucheza na mtoto nyumbani 🤗
Mtu asikudanganye, being a Dad for the first time unaweza kuchizika.
Unaweza kumchukua mwanao uzunguke naye mitaani just for the funny 🤗