Ulijisikiaje baada ya kugundua unaenda kuwa mzazi kwa Mara ya kwanza?

Ulijisikiaje baada ya kugundua unaenda kuwa mzazi kwa Mara ya kwanza?

Nilikuwa na mixed feelings, shauku na uoga.

Nilipata bahati ya kuwepo mtoto alipokuwa anazaliwa na kupata fursa ya kumbeba alipofutwa tu. Kwa mara ya kwanza nadhani nilitokwa na machozi ya furaha, yani nilijikuta machozi tu yananitoka.

Ilikuwa ni hisia nzuri mno.


Hakuna mtu yeyote anaeweza kukufundisha jinsi ya kuwa mzazi bora, just be the best you can be kwa kuwepo katika kila hatua ya ujauzito mpaka kujifungua kwa mzazi mwenzio. Kumbuka kila kitu kwako ni kipya hivyo ni sawa kuwa na hofu na uoga.

Funzo pekee ambalo nahisi ni muhimu ni kupanga na mwenzi wako kupata mtoto, nahisi hapo utaenjoy zaidi process yote mpaka mtoto kuzaliwa.
 
Ilikuwa ni moment nzuri sana Kwa kweli

Baada ya kupima na kujua mwenzangu alikuwa Mjamzito Kwa mara ya kwanza, nilihakikisha natumia resources zote kumtunza na kuhakikisha anakula mlo kamili Kila Siku

Nilihakikisha namtunza vizuri Mama Kijacho pamoja na mtoto mwenyewe iwapo atazaliwa salama

Ilikuwa sitaki apate tatizo lolote wakati wote wa ujauzito wake, na yeye alikuwa anadeka hadi basi (unaweza kuwa Kazini, mwenzio anakupigia simu eti mtoto(mimba) amemisi kusikia sauti yako hivyo anaomba niongee naye)

Ujauzito huwa unakuja na mabadiriko ya mwili wakati mwingine na tabia Kwa Mwanamke ama Kwa Baba husika (Baba Kijacho)

Binafsi nilikuwa nahisi kichefuchefu wakati wote Waifu alipokuwa Mjamzito hadi kilipokoma baada ya yeye kujifungua 🙌

Mama Kija wangu, yeye alikuwa Mpenzi sana wa Kitimoto na Soda ya Pepsi

Kwahiyo nilimwekea Bili Kwa Mangi kwaajili ya kula Kila Siku

Soda nilikuwa nanua Kreti la Pepsi Kila baada ya Siku 4 maana alikuwa na wastani wa kunywa Chupa 5 hadi 6 Kwa Siku 🙌

Baada ya miezi 9 alijifungua mtoto wa Kiume mwenye Afya tele

Ilikuwa ni kama naota kupewa taarifa zile na Daktari, maana kusema kweli Wanaume wengi hupenda kupata Watoto wa Kiume kwenye Uzao wetu

Kutokea hapo nikawa nawahi kutoka Kazini Kila Siku hata kama ni Kwa kutoroka ili niweze kwenda kucheza na mtoto nyumbani 🤗

Mtu asikudanganye, being a Dad for the first time unaweza kuchizika.

Unaweza kumchukua mwanao uzunguke naye mitaani just for the funny 🤗
Hahaha, hongera kwako mkuu. Hop e mli tengeneza wengine😁.
Vipi Kuhusu changamoto Mlizo kumbana nazo mkubwa??.

una ushauri upi kwa vijana kuhusu suala Zina la uzazi, hasa Kwa sisi wanaume!?.

vipi kuhusu kubambikiziwa, Kuna precaution gani za kuchukua 😁
 
Narudia.Sitaki kukumbuka na kusimulia sipendi.Uzuri ni kwamba miaka hiyo hakukuwa na miaka "salasini lupango"!Ilikuwa sekondari i.e,mimi A-level na yeye O-level.
Mkuu Moisemusajiografii, for the sake ya sisi vijana.
Simulia hata kidogo basi 🤣, itakuwa uli kimbizwa na panga ehh😂
 
Nilitawaliwa na wasiwasi Je nitazaa salama , mwanangu atakuwa Hai , atafananaje na nitakuwa mama Kweli, nitaweza hekaheka za Leba kila siku zikisonga mawazo yalizidi

Mwishowe 😅😅 nikatoboa Raha sanaa.
 
Habari wakuu, najua wengine humu tayari mmesha oa au ni wazazi tayari.

Ningependa mtupe uzoefu wenu, kuwa uli jisikia vipi kwa Mara ya kwanza baada ya kugundua wewe ni mzazi mtarajiwa.

Kuna kipi Cha kuji funza zaidi , ili kuwa mzazi bora?
1. Changamoto mlizo kumbana nazo, kabla na baada ya kuwa mzazi. (Hii kwa wanaume na Wanawake, ita pendeza mki elezea kwa kina zaidi).

2. Una ushauri upi kwa vijana kuhusu suala hilo la kuwa mzazi.

3. Kwa mwanaume ni Mambo yapi ya kuzingatia zaidi, hasa Baada ya kupata taarifa hizo.

I mean no malice to nobody.
View attachment 2967184View attachment 2967185
Mm sipendi matoto matundu of course siyapendagi matoto tundu😊
 
Back
Top Bottom