Ulikuwa Bingwa wa Michezo ipi Utotoni?

Ulikuwa Bingwa wa Michezo ipi Utotoni?

Ifahamu michezo asilia ya watoto inayotambulika katika Lugha adhimu ya Kiswahili

1) Kombolela
2) Mdako/nakwa
3) Rede
4) Nage
5) Tobo
6) Saga koboa
7) Ukuti ukuti
8) Kinyulinyuli
9) Visoda
10) Kula mbakishie baba

Itaendelea...

Utoto wangu nilidhulumiwa sana , majukumu yalio kuwa nje ya umri wangu yaligharimu.
Hata hivyo kombolela nilikua vizuri kwayo, nikijificha sehemi sionekani kamwe.
 
Hadi sasa unacheza games ?
adi sasa nacheza pale nikikutana na wale tulio cheza udogoni yan ni kama muunganiko flani usiofutika kwenye mioyo yetu wengine tupo mikoa tofaut but sometime mtu anaez kukwambia ntafunga safari nije kukusallimia pia tutapita sehem tujikumbushie vitu vyetu😁
 
Ifahamu michezo asilia ya watoto inayotambulika katika Lugha adhimu ya Kiswahili

1) Kombolela
2) Mdako/nakwa
3) Rede
4) Nage
5) Tobo
6) Saga koboa
7) Ukuti ukuti
8) Kinyulinyuli
9) Visoda
10) Kula mbakishie baba

Itaendelea...

Goroli na visoda
Enzi izo naingia na goroli mbili tatu natoka mfuko wa suruali umejaa. Mtaani akija mtu anapiga goroli sana wananiita mm .
I miss the old me😌❤️
 
Sasa Kombolela mnachaguliana vipi mume na Mke wakati pale mkibutua tu lindo/kopo mnatawanyika ... Labda mkakutane huko ...Ule wa kuchaguliana Mke na mume inaitwa KIBABA NA MAMA.. WAZAZI MNAKUWA NA KANYUMBA KENU NA WATOTO KANYUMBA KAO... Nilikuwa natengeza taa Kwa vibetri na tubalbu tule tudogooo ... Tunaweka kwenye nyumba yetu na watoto mnawaambia hakuna kuuingia Kwa baba mpaka mgonge hodi ...wanabaki nje wanajipikilisha mboga na ugali kwenye vikopo vya Tanbond vya bati....aseee
Umenirudisha mbali sana 😂 😂
 
Yani, kuna dada aliitwa pendoo sita kaa nimsahau , nilifumwa nae mama alinipiga mpaka nikaingia uvunguni🤣
Kipigo chote hicho alafu sasa hv umekuwa anataka uoe wakati tayari alisha kuharibu kisaikolojia
 
Back
Top Bottom