Ulimwengu wa majini na mambo niliyoshuhudia na kujifunza kwao

Basi baba alipokea ile pesa na kuiweka mfukoni mwake lakini nilimwambia kuwa pesa ile asiitumie wala kwenda maduka ya kubadilisha fedha aiache hadi baada ya siku saba na sikumwambia sababu.

Swala ya alaasiri nakumbuka tuliswali pale nyumbani na baada ya swalat tukabaki wote chumbani kwangu pale, na hapo nilimwambia baba asome suratul yaasin na suratul jinn kuweka sawa mwili baada ya nafsi yake kutoka muda mrefu kwenda kushuhudia mambo na alienambia nimwambie ni mzee Ruhaby japo kwa muda ule pale chumbani hakuja lakini sauti yake niliisikia.
Na hata kuhusu ile pesa kuwa asiitumie hadi baada ya siku saba ni yeye mzee Ruhaby ndio alinambia nimwambie na mara hii alinambia kuwa anataka afanye kitu kwaajili ya baba yangu mimi sikujua ni kitu gani na sikumuuliza sababu nisingeweza kuongea na yeye huku naongea na baba .
Lakini alinipa maelekezo ya kumfanyia baba baada ya swalat magharibi kuna kiasi chake cha pesa kingi tuu kwa watu wake anaodai atalipwa na atapata safari nyingine ya dar es salaam kuchukua pesa nyingi tuu.

Hapo sikuwa najua kama baba kuna watu anawadai pesa nyingi na hawataki kumlipa au wanamzungusha kumpa, hivyo ilibidi nimuulize baba vizuri na kisha alikiri kusema anakaribia hadi kukata tamaa juu ya kupata pesa hizo . Na kuhusu dar es salaam nako alisema hana matumaini maana keshaahidiwa sana .

Baaada ya maongezi mengi na mengi magharibi ilifika na baada ya swalat kumalizika mzee Ruhaby alinambia kuwa nichukue bakuli la maji, niweke ile pesa niweke ubani na udi na matone ya asali na niende kule kwenye mkuyu kuna kitu kitadondoshwa kutoka juu niokote niweke, sasa kwakuwa muda ulienda sana ikabidi nimwambie dada Aisha aende kukileta.
dada alienda kilianguka kitu kinawaka sana dada aliokota na kuja nacho kabla ya kuona ni nini nilifahamu kuwa ni ua la mkuyu.
Basi nilichanganya vizuri vile vitu huku nikipata maelekezo muhimu kwa mfumo wa sauti yake mzee Ruhaby.
Kuna maneno kadhaa alinambia nifatishe kusema, nilisema maneno na kisha akanambia nimpe baba yake maji anawe mikono na kuosha uso yaani afanye kama mwenye kuweka udhu ila abakishe mengine ataoga kidogo na mengine asubuhi atatumia muda sio mrefu ataitwa akachukue pesa .

Baada ya zoezi kukamilika tuliingia ndani muda wote baba yupo kimya tuu ni kama mtu anaeshangaa kuona nafanya mambo ambayo yeye mwenyewe hayajui wala hajawahi kuyaona sehemu.
Lakini tulipoingia ndani mama alikuwa akisema kuwa karibu na jikoni amepishana na mtu amevaa kanzu lakini hana uhakika kuwa ni kweli au ni macho tuu yamemdanganya.

Nakumbuka baada ya zoezi lile baba alitoka na kile kitabu kuingia chumbani huku yale maji akiondoka nayo nikamwambia ayaweke mvunguni mwa kitanda .
Mimi nilibaki chumbani kwangu tuu pale na haikuchukua muda mrefu kaka zangu waliingia wakitokea kwenye biashara na kuniuliza baba yuko wapi .
Walimpatia salamu kuwa wamekutana na mzee Othman kesho aende wakaongee na huyu mzee Othman ni mzee ambae anadaiwa na baba pesa nyingi tuu . Nilishangaa na sikutaka kuamini kuwa kile tulichofanya tayari kimetoa jawabu kabla ya usiku kumalizika.
Asubuhi kuamka kulikuwa na mvua sana ikawa vigumu kutoka kwenda masjid badala yake tulikaa sebleni na ibada ya alfajir tulifanya pale pale nyumbani.
Kisha nikamuacha baba akifanya nyiradi mimi sikuweza nilirudi chumbani kulala sababu usiku sikulala vizuri sababu ya mawazo ya rafiki yangu abushiri alikuwa akiumwa sana .
Nililala sana hadi nilipokuja kuamshwa kwaajili ya kifungua kinywa, baada ya kula nikarudi tena chumbani na haikuchukua muda nilimsikia baba akisalimiana na mtu pale sebleni, nilitoka nilijuwa rafiki yake sheikh Yusuf.

Ni yule mzee Othman alikuwa na amekuja yeye mwenyewe kumpa baba fedha zake na alisema kuwa usiku mzima hakulala na alitamani asubuhi ifike haraka aonane na baba ampe pesa zake moyo ulikuwa ukimuuma na kujiskia vibaya kukaa na pesa za mtu muda mrefu.
Baba alipokea tuu pesa na kuzihesabu na mzee yule hakukaa sana aliondoka.

"Deni lilikuwa la muda mrefu sana lakini sasa limelipwa lote kikamilifu mola wangu nakushukuru " baba alisema na kuondoka kuingia chumbani na ule mfuko wa pesa .
 
Muda ule nilitoka na kaka zangu kwenda kwa kina abushiri msambweni lakini tulipokuwa njiani nilikuwa nakijiskia vibaya sana kwenye nafsi , nilijikuta nikiskia kulia tuu nilipata hisia kuwa abushiri hospital hatarudi atafariki na kweli haikuchukua muda wakati tunafika pale kwao haikuchukua muda zililetwa taarifa kuwa amekufa na hivyo watu waandae mazingira marehemu aletwe kwa taratibu za mazishi.
Niliumia sana ile siku niliumia sitaki kukumbuka, yeye abushiri alikuwa ndio rafiki yangu peke yake ninaempenda sana . Baba yangu na baba yake abushiri pamoja na kiongozi fulani katika serikali ya Tanzania walisoma pamoja hivyo watu walipigiana simu kupeana taarifa za msiba.

Tulirudi nyumbani bila kuongea na mtu niliingia chumbani na kujitupa kitandani nililia sana hata mzee Ruhaby alipokuja mimi sikuangalia pale ukutani nae alinifariji kwa maneno hadi aliondoka mimi sikuongea kitu .
Baba mama na kaka waliondoka kwenda msibani mimi nilibaki na dada .
SEHEMU YA TANO: mambo yaliyoibuka kwenye msiba wa abushiri, safari ya baba dar es salaam na kuimarika kwa uchumi wa nyumbani, kupewa chumba maalum cha kufikia viumbe
 
Yanatolewa kwa Sala za Toba na utakaso kwa Baba Yah El'Elyon hamna kisichotoka. Kama yupo tayari tuanze safari Mimi na yeye litatoka hilo takataka
sio kila jini ni jini m-baya kuna wengne wanakuw umezaliwa nao ila kama wa huyo jamaa ni wakuwekwa kama mwenyew anavyodai anauwezo pia wa kutolewa ila ni kwa higher vibration of energy yani mweny nguvu kuliko alie muwek au mwenyew alie muwek ndo anawez kumtoa...
 
Hii ni sehemu ya ilmu waliyojaaliwa kuwa nayo
Assalam aleykum!!naomba msaada kidogo.Kuna jini wa kike alinitokea ndotoni aliletwa na babu zangu waliokufa miaka mingi iliyopita.Alijitambulisha kwa jina la AISHA BINT AFRIT,then akavua nguo tukafanya mapenzi then kesho yake akanipa pete nikiwa chooni,akawa na desturi ya kuja ndotoni nafanya naye mapenzi.Siku moja alikuja na katoto ka kike kama ka miaka minne hivi akawa analalamika kwamba nimemtelekeza maana ile pete niliitupa,,JE UNAWEZA KUMFAHAMU HUYU JINI ALIKO KWA SASA?
 
Waalaykumusalam warahmatullah wabarakatu, alikuwa katika mavazi ya rangi gani? Na alikupa pete ya rangi gani? na siku gani alikuwa anakujia zaidi?
 
Ndicho nachozungumzia maana hiyo higher vibration ndio mwili wa Nuru wa asili yetu. Jini si kiumbe wa Nuru hivyo hupaswi kukaa naye wala kumtumikia. Anapaswa kutufuzwa haraka
 
Waalaykumusalam warahmatullah wabarakatu, alikuwa katika mavazi ya rangi gani? Na alikupa pete ya rangi gani? na siku gani alikuwa anakujia zaidi?
Pete ilikuwa gold,mavazi meupe na sura yake kama mwarabu hivi siku ya kuja kwake kwa kweli sikumbuki
 
Ndicho nachozungumzia maana hiyo higher vibration ndio mwili wa Nuru wa asili yetu. Jini si kiumbe wa Nuru hivyo hupaswi kukaa naye wala kumtumikia. Anapaswa kutufuzwa haraka

Ndicho nachozungumzia maana hiyo higher vibration ndio mwili wa Nuru wa asili yetu. Jini si kiumbe wa Nuru hivyo hupaswi kukaa naye wala kumtumikia. Anapaswa kutufuzwa haraka
Unaweza kuwaambia watu tofauti kati ya jini , shetani na ifrit? Hapo nafikiri utajua vizuri jini ni nani na nuru anayo au hana ?
 
Unaweza kuwaambia watu tofauti kati ya jini , shetani na ifrit? Hapo nafikiri utajua vizuri jini ni nani na nuru anayo au hana ?
Ndugu, kwa kuheshimu nakuambia jini si dhambi wala giza kwa msingi wa asili yake, lakini nguvu za jini zina mwelekeo mbili: mwanga au giza.

Jini wa mwanga ni viumbe vya Baba, vinavyotii sheria za Nuru, vinavyosaidia wanadamu kwa rehema na uponyaji.

Shetani na ifrit ni viumbe wa giza waliotoka mbali na nuru, wakiwa wakiishi giza na kueneza hofu na maovu.

Mtu anayeungana na Baba El’Elyon na kupokea moto wa Yah’Ur anaweza kutambua na kuamuru jini wa giza kuondoka, akitumia nuru kama silaha.

Kwa hiyo, elimu ya kweli ya majini ni ile inayojumuisha nuru na upatanisho na Baba, si elimu inayotawanya watu kwa giza na hofu
 
. nakushaur mkuu fanya astral plojection ili uende ukapat kufahamu kuhusiana na mamb yote amby unayaon kweny ulimweng wa kimwili huyaelew mana itakusaidia kit kuptia huko utakuw unaelew kila kit kinachokuzungka hata ukitaku kuongea na mnyama yoyot na mukaelewan bila shida yoyot hat mimea pia kwa ujumla utaelew mengi
 
Asalaam alykm...

Napenda na nimevutiwa na unavyojibu maswali yetu kwa unyenyekevu mkubwa na kwa busara kabisa... Nahisi anayetujibu ni huyu jin mwema! Au la kama ni wewe basi sishangai watu wanaokutembelea na ukatatua shida zao.

SWALI LANGU

Je mwenyezi Mungu, ameruhusu tushirikiane na hawa majini wema? Kama ndivyo kwa nini tumeaminishwa kwenye baadhi ya dini hizi za kizungu kuwa majini ni mashetani na pepo wachafu, kiasi kwamba tukisikia jini unajua ni jitu haribifu tu?

Asante mengi nitakuja inbox.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…