Ulimwengu wa majini na mambo niliyoshuhudia na kujifunza kwao

TUNAENDELEA:
Basi yule bibi nilimpiga Kofi zito sana alishika uso wake nami nikaondoka kurudi pale alipokuwa baba , kaka na watu wengine kwenye jamvi . Muda wote huu Rauhiyah nilikuwa nae na nilikuwa na hasira nyingi sana nafikiri mpaka sasa hivi hajasahau hasira yangu ya siku ile.

Yule bibi alikuwa akilia kimya kimya huku akisema nishaumia eee nishaumia mtoto keshanitia ubovu huyu na ukilema. Mimi sikujali wala kuzingatia muda wote nilikuwa nikiangaza macho huku na kule nikijionea uchafu wa matendo ya waenda usiku .
Sijui kwanini walijazana msibani na katikati ya watu wenye huzuni kubwa ya kuondokewa na kijana mdogo tena swahiba yangu kwelikweli.
Muda sio mrefu sana wakina mama walitoa lalamiko kuwa upande wao kumeibuka wadudu chungu (sisimizi) wengi sana na kadiri muda unavyosonga walikuwa wakiongezeka sana na kuna kila dalili huwenda wangeingia barazani kwenye nyumba ya msiba.
Watu wazima waupande wa mwanaume walisimama nakwenda kuangalia, lakini kabla ya kurudi waliokuwa ndani ya chumba cha maiti walitoa taarifa kuwa kuna kundi la wadudu wengine weusi wameibuka na kuzunguka kwenye kitanda cha maiti tena upande wa kichwani.

Watu walihamaki sana lakini binafsi nilishajua ni kitu gani kinaendelea na kuwepo kwangu pale msibani kulisababisha mivutano mikubwa sana na kuna namna nilikuwa nikisababisha watu kuchelewa kukamilisha dhamira yao mbaya na ovu.
Wazee watatu walisimama tena kwenda ndani ya chumba cha marehemu , mimi, baba , kaka na watu wengine tulibaki pale kwenye jamvi lakini kiukweli kabisa macho yangu yalikuwa hayatulii kabisa muda wote nilikuwa naangalia huku na kule mpaka pale nilipoona kundi la mbwa wakilia kwa kupokezana sauti nilipoangalia vizuri hawakuwa mbwa bali walikuwa ni fisi hapo nikajua kweli wachawi walikuwa wameamua.

Kule ndani mambo hayakuwa vizuri walioenda walifanya jitihada zao niseme ukweli, lakini walizidiwa uwezo mzee mmoja alitoka na kumfata baba na kumwambia kwa sauti ya chini chini lakini nilijuwa kuwa mzee yule alikuwa akimuulizia sheikh Yusuf rafiki wa baba , lakini sheikh Yusuf kwa muda ule hakuwepo msibani yeye msibani angefika siku ya pili kwaajili ya mazishi (kuzika) . Nia ya wao kumuulizia sheikh Yusuf walitaka aingie mule ndani ya chumba cha marehemu afanye dua, kutokuwepo kwake ilibidi baba yangu ndio afanye zoezi lile.
Baba kabla ya kusimama kwenda aliniangalia sana machoni, narudia tena baba aliniangalia sana machoni na mimi nikamuangalia sana baba yangu , nilimuangalia baba yangu hadi mapigo yangu ya moyo yakawa yanapiga mbio sana nikaanza kutoka jasho jembamba. Nilitaka kusema kitu lakini Rauhiyah alinizuia na kiukweli kama sio Rauhiyah kunizuia basi nahisi mambo yangeharibika sana .

Baba alisimama na kunishika mkono nisimame, nikasimama na tukaanza kwenda wote kuelekea kwenye chumba cha maiti, Rauhiyah muda huu hakunifata yeye alibaki nje na sababu kubwa ni kubaki na kaka yangu, kaka yangu ambae yeye bado walikuwa hawajamfungua. Mazingira yalikuwa mabaya sana wachawi wengi hivyo jicho lote lazima libaki kwake.
Tuliingia pale ndani lakini tulipofika mlangoni utosi wangu ukawa unavuta sana na kuniuma nikamwambia baba asimame asiingie ndani asimame palepale nikaangalia pale juu ya kizingiti cha mlango nikaona chupa ndogo nyeusi imefungwa uzi mwekundu inabembea, bila kupoteza muda nikajua kinachoendelea hivyo nikafanya utajo wa haraka sana kumuita mzee Ruhaby lakini muda huu kumbe yeye alikuwa kwenye misafara ya kiilmu hivyo akatumwa mwingine wakuja.
Alikuja wakiume na alipofika nikamwambia ashushe ile chupa, aliishusha na kuiangusha pale chini na akaamua kutangulia mbele kusafisha njia sisi tupite.

Kuja kwa Saadiq Rihaan pale msibani kulikuwa ni pigo zito kwa wachawi, tuliingia ndani kweli kulikuwa na wadudu weusi wengi kwelikweli, nilimwambia baba amwambie yule mzee tulieenda nae awaeleze watu wengine watoke, watu walitoka tukabaki mimi, baba , yule mzee na mwingine ni Rihaan ambae yeye watu walikuwa hawamuoni. Sasa hapo nilisogea pembeni kidogo na kumwambia rihaan namuamuru ampe baba yangu taarifa moja kwa moja kupitia sauti sikioni mwake.
Jambo la kwanza rihaan kumwambia baba ni kumfunua maiti ile shuka nyeupe aliyofunikwa na kisha asogee sikioni mwa marehemu asome na kufanya utajo wa maneno fulani hivi ( sitayataja tafadhalini) kisha asome suratul yaasin yote .

Baba alifanya kama alivyoambiwa na mara baada ya kumaliza akaambiwa aagaize maji yaletwe, maji yalipoletwa kwenye bakuli nilimuona Rihaan akisogea kwenye lile bakuli na kupuliza pumzi mle na kumwambia baba asome kuna utajo fulani na kisha suratul Baynnah na suratul fily kisha maji yale arashie rashie kwenye wale wadudu.
Haikupita muda mrefu wale wadudu wakawa wanajikusanya sehemu moja wao wenyewe mara wakawa wamekufa.

Rihaan akatoa maelezo mengine kuwa chini ya mvungu wa kitanda cha maiti kuna chungu kitolewe, hivyo baba alimwambia yule mzee tusogeze kitanda, tulivuta kitanda kiukweli chungu kwa macho yakawaida mtu huwezi kukiona hata kidogo, lakini palikuwa na chungu na kulikuwa na viwembe, sindano, na kichupa kingine. Pia kulikuwa na unga unga mweusi.
Kilivyotolewa yule mzee alikuwa na hofu sana na woga ni hivyo hakukuwa na namna ila alitamani atoke nje .
Nakumbuka tulikiacha kitanda cha maiti pale kando bila kurudisha kilipokuwa mwanzo.

Rihaan alitoa maelezo kuwa shuka za kumfunika marehemu zibadilishwe na kuwashwe mshumaa ndani ya chumba cha maiti taa ya kibatari ile itolewe. Yule mzee baba alimpa maelezo na tukawa tunatoka nje .
Tulipokuwa tunatoka nje rihaan hatukuongozana nae yeye tulimkuta amesimama uwanjani lakini mkononi mwake alishika mchanga ni kama alikuwa akiongea nao ule mchanga na kisha aliuachia ukaenda na upepo mchanga ule .

Haukupita muda mrefu kuliibuka upepo mkali sana na ghafla kukatimuka vumbi jingi sana kukaanza kusikika kelele za vilio kwa baadhi ya watu.
Nakumbuka kuna bibi mmoja alikuwa amevaa khanga zake za njano hakuwa mbali sana na niliposimama alikuwa akilia sana kuwa macho yanawasha, haoni mbele na alikuwa akiongea sijui maneno ya lugha gani ile ni kama alikuwa anaropoka. "Yote ameyataka mama fulani ( alitaja jina la mama mmoja maarufu sana pale mtaani) kisha alianguka chini.

Rihaan sijui aliusemea maneno gani ule mchanga lakini baadae alinambia kuwa miongoni mwa alivyosoma ilikuwepo suratul buruj, zilzal na nyingine mbili . Na hapo makhudam na maburuhani na malaikat ruhaniya wakafanya kazi yao ya kufurumusha upepo mkali uliomlenga kila mchawi akiyekuwepo pale msibani.

Baada ya hekaheka ya kuwadhibiti wachawi na nia yao mbaya tuliaga na kuondoka kurudi nyumbani tukisubiri siku ya kesho yake yaani ile siku ya mazishi. Rihaan na Rauhiyah hatukuongozana nao kurudi nyumbani wao waliondoka wenyewe.
Bwana ndugu zanguni sitasahau vita iliyoendelea usiku wa siku ile ya Alhamis ni kama wachawi waliitana kumaliza hasira baada ya kuvuruga mpango wao .
 
( Nimeruka kuna yasiyo muhimu sana twende na muda )
Usiku mkubwa ulipoingia uwanjani kulisikika kishindo kizito sana nahisi mimi ndio nilikuwa wa kwanza kusikia kisha akafatia dada Aisha maana nilimsikia akiguna akiwa chumbani mwake na alikuwa anataka atoke nje kuangalia lakini niliwahi kutoka chumbani kwangu na kusimama Karibu na chumba chake .
Nilifungua mlango kidogo tuuu nikachungulia kule kwenye mkuyu nikamuona kiumbe kimoja (huyu simtaji jina hajataka jina lake litajwe nisimnyime uhuru wake) alikuwa yuko peke yake tuu , na huyu ni swahiba mkubwa wa dada Aisha kuliko mimi .
Nilifunga mlango tukawa tunaulizana na dada Aisha ni kishindo cha nini? tulikosa jawabu kila mtu aliingia chumbani mwake, kumbe wakati narudi chumbani dada yeye alijiwa na yule swahiba wake ambae jina lake sitataja. Na alipofika swahiba wake yule alimwambia dada Aisha kuwa asilale abaki macho muda sio mrefu kuna kitu kitatokea.
Nikiwa chumbani kwangu nikaanza kuhisi kuna kiumbe amekuja pale nyumbani lakini kwakuwa hakuja kwaajili yangu sikutaka kufatilia sana hivyo nikawa nimejilaza nasubiri saa tisa usiku ifike nifanye visimamo vya usiku.
Lakini ghafla nikaskia mlango mkubwa umefunguliwa na hatua zikawa zinatoka kuelekea nje kisha huko nje nikaskia kelele za paka akilia kwa uchungu sana. Kulifatia mburuzo kama mtu anaburuzwa ardhini huku analia na kuugulia, hapo nilishindwa kuvumilia nilifungua mlango tena na muda huo dada mlango wake ulikuwa wazi nikachungulia kule uwanjani nilimuona dada yupo na mtu huku anaongea mama fulani umefata nini hapa? Na wewe ni mchawi pia ? kabla sijatoka nje dada aliingia ndani huku mikono yote imejaa damu hapo nikajua wazi kuwa yeye na yule swahiba wake kuna mchawi wametoka kumpa stahiki yake.
Dada akaanza kunambia kuwa kulikuja kundi la wachawi pale uwanjani na walikuwa wanapiga ngoma na walikuwa wamebeba fuvu la kichwa cha mtu , walikuwa wamekaa juu ya mgongo wa mtu na walikuwa wakiimba nyimbo zao huku wakitaja jina langu kuwa lazima nikomeshwe kuwaharibia mpango wao . Sasa wale wachawi wenyewe walikuwa wakinitafuta mimi ila walikuwa hawaioni nyumba yetu wala kuniona mimi hivyo waliishia uwanjani kwenye miembe. Lakini mmoja kati yao anatujua vizuri pale nyumbani hivyo alitumwa aje kufungua njia na hapo yule swahiba wa dada alitoka kwenye mkuyu na kuja kumpa pigo baya ndio kile kishindo kizito.
Wengine walikimbia yeye alishindwa na kujigeuza paka hivyo dada na swahiba yake walitoka kumsulubu.

Baada ya maongezi yale nilirudi chumbani kwaajili ya kufanya visimamo vyangu vya usiku na kumuacha dada Aisha akigomba kwelikweli kuwa asubuhi anamfata mchawi mmoja kwake , aligomba huku ananawa mikono kuondoa damu .
Kabla sijaanza kuswali nikaambiwa sikioni kuwa mchawi aliyejigeuza paka na kujeruhiwa ni mama fulani kweli na haitafika asubuhi atakuwa marehemu mimi nikaachana na kuzingatia ile habari nikawa naswali. Baada ya rakaa zangu kumalizika nikawa nawaza yaliyoendelea mchana kwenye msiba wa abushiri na kwenye mazishi nini kitatokea na hapo nikawa nasoma dua Mwenyezi aepushe shari.
ITAENDELEA HII:
Lakini tafadhali sana sehemu ambazo sikutaja majina ya watu au kiumbe huyu swahiba wa dada msijiskie vibaya na wala msiulize sana kwanini hakutaka jina lake litajwe pamoja na kuwa ameruhusu mambo haya kusimuliwa.
 
Nilikuwa natafuta kuhusu Cassiel nikasema ngoja nije kuchungulia mara moja pengine mkuu buraq atakuwepo na kweli imekuwa🤠
 
Daah mkuu kama waweza nisaidia kuhusu hilo usisite kunisaidia tafadhali. Huwa najua mambo ya rohoni machache sana tena juu juu, inshort mimi ni kama mwanafunzi wa chekechea na unaniagiza kufanya mambo ya chuo kikuu ambayo sina hata uelewa nayo😂😂

Kiukweli mbele naona jangwa
Hamna neno, utauliza hapa maswali juu ya unayotaka kufahamu nitakwambia
 
Nilikuwa natafuta kuhusu Cassiel nikasema ngoja nije kuchungulia mara moja pengine mkuu buraq atakuwepo na kweli imekuwa🤠
Anhaa, hulali mapema.
Huyu cassiel au kayfail yenyewe ni malaika mpole tuu na ukiwa ndani ya utawala wake wa kinyota huwa na kawaida ya kukuondoshea sana hofu juu ya huzuni au yanayokupa huzuni.
Unaweza kuwa unalia kwa huzuni lakini ghafla ukajiona ni mwenye furaha ya ghafla na matumaini.
Allah mjuzi zaidi na ndio mwenye ilmu ya siri kuhusu ulimwengu mengine yapo katika himaya yake binaadamu, malaika na majini hatuyajui ila yeye tuu.
 
Hamna neno, utauliza hapa maswali juu ya unayotaka kufahamu nitakwambia
Sawa mkuu, sasa kuhusu kujua ufalme wa nyota ya mbuzi nimeanza kutafuta kujijua vizuri

Nimeanza kutafuta mbili tatu kumhusu cassiel inasemekana ni yupo(mtawala) mbingu ya saba, na bado nahangaika

Sema daah hizi mambo ni sawa na kunionea kutafuta mwenyewe😂 ilihali ndio kwanza naanza safari
Chukulia kama mtoto wa chekechea kufanya mambo ya chuo kikuu
 
Anhaa, hulali mapema.
Huyu cassiel au kayfail yenyewe ni malaika mpole tuu na ukiwa ndani ya utawala wake wa kinyota huwa na kawaida ya kukuondoshea sana hofu juu ya huzuni au yanayokupa huzuni.
Unaweza kuwa unalia kwa huzuni lakini ghafla ukajiona ni mwenye furaha ya ghafla na matumaini.
Allah mjuzi zaidi na ndio mwenye ilmu ya siri kuhusu ulimwengu mengine yapo katika himaya yake binaadamu, malaika na majini hatuyajui ila yeye tuu.
Amin mkuu,
 
Sawa mkuu, sasa kuhusu kujua ufalme wa nyota ya mbuzi nimeanza kutafuta kujijua vizuri

Nimeanza kutafuta mbili tatu kumhusu cassiel inasemekana ni yupo(mtawala) mbingu ya saba, na bado nahangaika

Sema daah hizi mambo ni sawa na kunionea kutafuta mwenyewe😂 ilihali ndio kwanza naanza safari
Chukulia kama mtoto wa chekechea kufanya mambo ya chuo kikuu
Mashallah sema hongera sana jitihada unayo na huku ndio njia bora ya kujifunza unapata wingi wa mambo
 
Pia nina swali kuhusu willpower? Kama unafahamu naomba unielezee kwa undani kama hutojali tafadhali

Na nini kifanyike ili kuwa na willpower kubwa zaidi?
 
Mashallah sema hongera sana jitihada unayo na huku ndio njia bora ya kujifunza unapata wingi wa mambo
Yeah naweka nia kabisa. Penye nia pana njia mkuu

Zamani nilikuwa nikiwaza sana pesa, yaani nilitaka kuwa na mali inshort ndio kilikuwa kipaumbele changuila sasa ni tofauti, yaani katika vitu vikuu navyotafuta sana siku hizi ni Hekima, maarifa na nguvu za kiroho....
 
TUNAENDELEA:
Basi yule bibi nilimpiga Kofi zito sana alishika uso wake nami nikaondoka kurudi pale alipokuwa baba , kaka na watu wengine kwenye jamvi . Muda wote huu Rauhiyah nilikuwa nae na nilikuwa na hasira nyingi sana nafikiri mpaka sasa hivi hajasahau hasira yangu ya siku ile.

Yule bibi alikuwa akilia kimya kimya huku akisema nishaumia eee nishaumia mtoto keshanitia ubovu huyu na ukilema. Mimi sikujali wala kuzingatia muda wote nilikuwa nikiangaza macho huku na kule nikijionea uchafu wa matendo ya waenda usiku .
Sijui kwanini walijazana msibani na katikati ya watu wenye huzuni kubwa ya kuondokewa na kijana mdogo tena swahiba yangu kwelikweli.
Muda sio mrefu sana wakina mama walitoa lalamiko kuwa upande wao kumeibuka wadudu chungu (sisimizi) wengi sana na kadiri muda unavyosonga walikuwa wakiongezeka sana na kuna kila dalili huwenda wangeingia barazani kwenye nyumba ya msiba.
Watu wazima waupande wa mwanaume walisimama nakwenda kuangalia, lakini kabla ya kurudi waliokuwa ndani ya chumba cha maiti walitoa taarifa kuwa kuna kundi la wadudu wengine weusi wameibuka na kuzunguka kwenye kitanda cha maiti tena upande wa kichwani.

Watu walihamaki sana lakini binafsi nilishajua ni kitu gani kinaendelea na kuwepo kwangu pale msibani kulisababisha mivutano mikubwa sana na kuna namna nilikuwa nikisababisha watu kuchelewa kukamilisha dhamira yao mbaya na ovu.
Wazee watatu walisimama tena kwenda ndani ya chumba cha marehemu , mimi, baba , kaka na watu wengine tulibaki pale kwenye jamvi lakini kiukweli kabisa macho yangu yalikuwa hayatulii kabisa muda wote nilikuwa naangalia huku na kule mpaka pale nilipoona kundi la mbwa wakilia kwa kupokezana sauti nilipoangalia vizuri hawakuwa mbwa bali walikuwa ni fisi hapo nikajua kweli wachawi walikuwa wameamua.

Kule ndani mambo hayakuwa vizuri walioenda walifanya jitihada zao niseme ukweli, lakini walizidiwa uwezo mzee mmoja alitoka na kumfata baba na kumwambia kwa sauti ya chini chini lakini nilijuwa kuwa mzee yule alikuwa akimuulizia sheikh Yusuf rafiki wa baba , lakini sheikh Yusuf kwa muda ule hakuwepo msibani yeye msibani angefika siku ya pili kwaajili ya mazishi (kuzika) . Nia ya wao kumuulizia sheikh Yusuf walitaka aingie mule ndani ya chumba cha marehemu afanye dua, kutokuwepo kwake ilibidi baba yangu ndio afanye zoezi lile.
Baba kabla ya kusimama kwenda aliniangalia sana machoni, narudia tena baba aliniangalia sana machoni na mimi nikamuangalia sana baba yangu , nilimuangalia baba yangu hadi mapigo yangu ya moyo yakawa yanapiga mbio sana nikaanza kutoka jasho jembamba. Nilitaka kusema kitu lakini Rauhiyah alinizuia na kiukweli kama sio Rauhiyah kunizuia basi nahisi mambo yangeharibika sana .

Baba alisimama na kunishika mkono nisimame, nikasimama na tukaanza kwenda wote kuelekea kwenye chumba cha maiti, Rauhiyah muda huu hakunifata yeye alibaki nje na sababu kubwa ni kubaki na kaka yangu, kaka yangu ambae yeye bado walikuwa hawajamfungua. Mazingira yalikuwa mabaya sana wachawi wengi hivyo jicho lote lazima libaki kwake.
Tuliingia pale ndani lakini tulipofika mlangoni utosi wangu ukawa unavuta sana na kuniuma nikamwambia baba asimame asiingie ndani asimame palepale nikaangalia pale juu ya kizingiti cha mlango nikaona chupa ndogo nyeusi imefungwa uzi mwekundu inabembea, bila kupoteza muda nikajua kinachoendelea hivyo nikafanya utajo wa haraka sana kumuita mzee Ruhaby lakini muda huu kumbe yeye alikuwa kwenye misafara ya kiilmu hivyo akatumwa mwingine wakuja.
Alikuja wakiume na alipofika nikamwambia ashushe ile chupa, aliishusha na kuiangusha pale chini na akaamua kutangulia mbele kusafisha njia sisi tupite.

Kuja kwa Saadiq Rihaan pale msibani kulikuwa ni pigo zito kwa wachawi, tuliingia ndani kweli kulikuwa na wadudu weusi wengi kwelikweli, nilimwambia baba amwambie yule mzee tulieenda nae awaeleze watu wengine watoke, watu walitoka tukabaki mimi, baba , yule mzee na mwingine ni Rihaan ambae yeye watu walikuwa hawamuoni. Sasa hapo nilisogea pembeni kidogo na kumwambia rihaan namuamuru ampe baba yangu taarifa moja kwa moja kupitia sauti sikioni mwake.
Jambo la kwanza rihaan kumwambia baba ni kumfunua maiti ile shuka nyeupe aliyofunikwa na kisha asogee sikioni mwa marehemu asome na kufanya utajo wa maneno fulani hivi ( sitayataja tafadhalini) kisha asome suratul yaasin yote .

Baba alifanya kama alivyoambiwa na mara baada ya kumaliza akaambiwa aagaize maji yaletwe, maji yalipoletwa kwenye bakuli nilimuona Rihaan akisogea kwenye lile bakuli na kupuliza pumzi mle na kumwambia baba asome kuna utajo fulani na kisha suratul Baynnah na suratul fily kisha maji yale arashie rashie kwenye wale wadudu.
Haikupita muda mrefu wale wadudu wakawa wanajikusanya sehemu moja wao wenyewe mara wakawa wamekufa.

Rihaan akatoa maelezo mengine kuwa chini ya mvungu wa kitanda cha maiti kuna chungu kitolewe, hivyo baba alimwambia yule mzee tusogeze kitanda, tulivuta kitanda kiukweli chungu kwa macho yakawaida mtu huwezi kukiona hata kidogo, lakini palikuwa na chungu na kulikuwa na viwembe, sindano, na kichupa kingine. Pia kulikuwa na unga unga mweusi.
Kilivyotolewa yule mzee alikuwa na hofu sana na woga ni hivyo hakukuwa na namna ila alitamani atoke nje .
Nakumbuka tulikiacha kitanda cha maiti pale kando bila kurudisha kilipokuwa mwanzo.

Rihaan alitoa maelezo kuwa shuka za kumfunika marehemu zibadilishwe na kuwashwe mshumaa ndani ya chumba cha maiti taa ya kibatari ile itolewe. Yule mzee baba alimpa maelezo na tukawa tunatoka nje .
Tulipokuwa tunatoka nje rihaan hatukuongozana nae yeye tulimkuta amesimama uwanjani lakini mkononi mwake alishika mchanga ni kama alikuwa akiongea nao ule mchanga na kisha aliuachia ukaenda na upepo mchanga ule .

Haukupita muda mrefu kuliibuka upepo mkali sana na ghafla kukatimuka vumbi jingi sana kukaanza kusikika kelele za vilio kwa baadhi ya watu.
Nakumbuka kuna bibi mmoja alikuwa amevaa khanga zake za njano hakuwa mbali sana na niliposimama alikuwa akilia sana kuwa macho yanawasha, haoni mbele na alikuwa akiongea sijui maneno ya lugha gani ile ni kama alikuwa anaropoka. "Yote ameyataka mama fulani ( alitaja jina la mama mmoja maarufu sana pale mtaani) kisha alianguka chini.

Rihaan sijui aliusemea maneno gani ule mchanga lakini baadae alinambia kuwa miongoni mwa alivyosoma ilikuwepo suratul buruj, zilzal na nyingine mbili . Na hapo makhudam na maburuhani na malaikat ruhaniya wakafanya kazi yao ya kufurumusha upepo mkali uliomlenga kila mchawi akiyekuwepo pale msibani.

Baada ya hekaheka ya kuwadhibiti wachawi na nia yao mbaya tuliaga na kuondoka kurudi nyumbani tukisubiri siku ya kesho yake yaani ile siku ya mazishi. Rihaan na Rauhiyah hatukuongozana nao kurudi nyumbani wao waliondoka wenyewe.
Bwana ndugu zanguni sitasahau vita iliyoendelea usiku wa siku ile ya Alhamis ni kama wachawi waliitana kumaliza hasira baada ya kuvuruga mpango wao .
😂😂 Bila shika huyu Saadiq Rihaan ni komandoo la vita ulimwengu wa majini.
 
Yeah naweka nia kabisa. Penye nia pana njia mkuu

Zamani nilikuwa nikiwaza sana pesa, yaani nilitaka kuwa na mali inshort ndio kilikuwa kipaumbele changuila sasa ni tofauti, yaani katika vitu vikuu navyotafuta sana siku hizi ni Hekima, maarifa na nguvu za kiroho....
Mashallah hii safi kabisa
 
Back
Top Bottom