Ulipokea vipi Msiba wa Hayati Magufuli?

Ulipokea vipi Msiba wa Hayati Magufuli?

Alikuwa ni kiongozi mbaya kupindukia. Japo alikuwa muuaji na katili, kiasi cha kila mpenda haki kupendelea kutokuwa na kiongozi wa namna ile, lakini nilisikitika kupokea taarifa za kifo chake. Ni jambo jema mwovu aendelee kuishi, ajutie uovu wake au abadilike na kuuchukia uovu wake wa kale. Nilipoisikia habari ile, nilishtuka, nikaamka. Nilikaa kimya kwa dakika, nikajawa na simanzi. Maana kwa kweli pamoja na kuwaaumiza watu wengi, haikuwahi kutokea akilini mwangu kufikiria kuwa, aheri afe. Ningependelea aondoke kwenye uongozi lakini siyo kufa. Lakini basi kwa kuwa ilitokea, mapenzi ya Bwana yalitimia kwa kipimo cha hekima yake Mungu.

Vyovyote iwavyo, kifo chake ni fundisho kubwa kwetu tulio hai. Cha kujiuliza, sisi tunafanya nini tofauti na uovu wake? Tunafanya nini sambamba na mazuri yake, hata kama yakiwa machache? Kuna wengine ni fundisho kubwa kwao mara mbili zaidi maana wakati wa utawala wake, walitenda uovu mwingi wakiamini yupo wa kuwalinda kwenye uovu wao.

Wapo waliomkufuru Mungu, hata wakamwita Magufuli ni Mungu, wengine wakasema ni zaidi ya Yesu, na wengine wakasema eti Mungu amshukuru Magufuli. Na wote sasa hivi wamebakia kama kondoo wasio na mchungaji.

Hii ilikuwa ni kufuru kubwa. Mbaya zaidi hata marehemu mwenyewe hakuwakemea. Mwalimu Nyerere alipopambwa kupita kiasi, alimaka na kusema, 'mmeniita mchongameno nimenyamaza, mmeniita Haambiliki nimenyamaza, lakini hili la Musa, kuniita Musa, hapana, sitaki kusikia'. Yaani Mwalimu aliona kuwa yeye hafanani wala kumkaribia kwa chochote nabii Musa aliyewaongoza wana wa Israel toka utumwani Misri. Nabii Musa alikuwa mwanadamu, lakini mwalimu aliona bado Nabii Musa ni mkubwa mno kuweza kufananishwa naye. Marehemu alilinganishwa na Mungu, yeye akakaa kimya. Lilikuwa kosa kubwa.

Kifo chake ni fundisho kwetu kuwa Mungu hana ushirika na mwanadamu yeyote katika Umungu wake. Tunafundishwa kuwa Mungu hana mwanzo wala mwisho. Kifo hiki kilitufundisha kuwa hata uwe na nini, wewe bado ni mwanadamu, unafanana na wanadamu wenzako katika kuzaliwa na kufa.

Tuendelee kuomba, Mungu atujalie hekima ya kujifunza kupitia kifo hiki, na wala kifo hiki kisitufanye kuzidi kumkosea yeye Mungu au wanadamu wenzetu.
 
Wakati tukiwa kwenye kipindi cha Kumbu kumbu cha musiba wa hayati Dr John Pombe Magufuli Rais wa JMT awamu ya tano tuambizane wewe ndugu yangu huko uliko taarifa za musiba ulizipataje na ulipokea vipi msiba mzito wa kuondokewa na rais wa Tanzania?

Ilikuwa ni habari ya kusikitisha kwa Watanzania kwa mara ya kwanza kumpoteza Rais Kipenzi akiwa madarakani na pengine Afrika mashariki nzima.
Ujinga hauishimiaka miwili sasa bado kujadili mtu hamna mambo mengine ya kufanya?
 
Wakati tukiwa kwenye kipindi cha Kumbu kumbu cha musiba wa hayati Dr John Pombe Magufuli Rais wa JMT awamu ya tano tuambizane wewe ndugu yangu huko uliko taarifa za musiba ulizipataje na ulipokea vipi msiba mzito wa kuondokewa na rais wa Tanzania?

Ilikuwa ni habari ya kusikitisha kwa Watanzania kwa mara ya kwanza kumpoteza Rais Kipenzi akiwa madarakani na pengine Afrika mashariki nzima.
Nilikuwa nimelala, ghafla nastuka usiku nakuta sms ya mtu ananiuliza "ETI JIWE KAFA" fasta nikakimbilia jf nakuta Uzi uko page ya 200+. Kimoyomoyo nikajisemea "MWAMBA KADED"
 
Nakumbuka usiku ule nilimwombea kwa Mungu, kwamba Mungu amponye (kama anaumwa) maana kulikuwa na minong'ono na tetesi kwamba anaumwa sana na huenda amekufa kwa corona (sijui kwanini akina Kassim walituficha hivi hata maombi tukaomba ya kubahatisha tu).

Nikalala. Ile naamka asubuhi, naskia kuna mtu anasema "raisi wenu amekufa". Kwangu mimi hazikuwa habari njema, kwa kuwa hata Mungu hafurahii kufa kwake mwenye dhambi. Ila mtaa ninaoishi, kuna jamaa walikesha pub kwa kunywa mapombe nadhani waliomboleza kwa namna hiyo, ingawa baadhi yao (wafanyakazi serikalini) waliitwa kwenye mamlaka na kuulizwa kwanini wameshangilia kifo...
 
Ilikuwa ni habari ya kusikitisha kwa Watanzania kwa mara ya kwanza kumpoteza Rais Kipenzi akiwa madarakani na pengine Afrika mashariki nzima.

Usitake kuwapangia watu hisia!Sio watu wote walisikitika.Sitaki kuwa mnafiki katika hili :Mimi sikusikitika!
 
Nilipokea kwa Masikitiko makubwa.
Nilienda pale St. Peters, nikarandaranda sana pale. Kwani sio kitu rahisi, kama raia, kuondokana na mtu mwenye matazamio kama yako. Kiongozi wako. Ila....

Nilikubali, nikamwombea.

Amani ikutawale
 
Fact must told!
IMG_20230313_170725_768.jpg
 
Wakati tukiwa kwenye kipindi cha Kumbu kumbu cha musiba wa hayati Dr John Pombe Magufuli Rais wa JMT awamu ya tano tuambizane wewe ndugu yangu huko uliko taarifa za musiba ulizipataje na ulipokea vipi msiba mzito wa kuondokewa na rais wa Tanzania?

Ilikuwa ni habari ya kusikitisha kwa Watanzania kwa mara ya kwanza kumpoteza Rais Kipenzi akiwa madarakani na pengine Afrika mashariki nzima.
Kwanza nilijua ashafariki tokea tarehe 09 march baada ya Corona kumfyeka fyeeeee[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Siku anatangazwa nilifurahi sana tulifanya bonge ya party mwenge tukalewa hadi asubuhi tukisherehekea kuwa kambare amekata moto

Nchi yetu ilipata uhuru baada ya miaka 6 ya yule shetani katili wa kuzimu

Kwa kweli Asante Mungu, asante sana Corona kwa kumfyeka yule mwehu kambare mkuu
 
Back
Top Bottom