Ulishawahi kununua asali kwenye duka la serikali? Uliwezaje?

unaweza nipa nmba ya yule dada pale
 
Ni kweli unayoyasema ila punguza kidogo mzee baba, kwakweli hadi nahisi furaha yako imepunguzwa na siasa sio yule Behaviorist mzee wa vyura
 
Ukiona hivyo ujue asali hawana
 
Mm mbona napata kila nikienda. Tena kwa wingi mnooo. Uclipie kwao wakisema ipo chukua control namba nenda kwa wakala fasta mbona. Bila kupepesa macho hii ni bznes nzr mno kwa sisi baazi tuna uza nje ya nchi asali yenye lebo ya Tanzania yani serikali inauzika kirahisi nje. Ndio maana wanazidiwa na soko. Uzalishaji wao nazani mdogo
 
Acha uongo, mbona watu wananunua kila siku? Ni kweli kuna wakati stock huisha kwa sababu Asali inayouzwa hapo ni ile iliyozalishwa na Serikali tu.
Kwanini wasiwe na wakala wao sehemu kama Mbezi beach, Masaki, Oyster bay pale mororo store, Bagala kwenye barabara kuu pale, Temeke hospitali pale ni mahali pazuri kuweka, Kimara stend na mbezi mwisho wasafiri wanaoenda mikoani wanwaweza nunua. Ukiribimba wa
Yule mdada bonge ndiyo rafik yako??
Mimi asali ya Pinda naikuta soko kuu majengo mabanda ya nje kuna kibanda kinauza asali ndo humo naipata. Muuzaji ni kijana manamme.
 
Nyuki wa Tabora wanapata chakula kutoka kwenye maua ya Tumbaku ndo maana soko lake kimataifa limeshuka.
Kwa hiyo ukiila Asali unakuwa kama umevuta Sigara?
 
Una bahati waeleze wenzio mbinu unazotumia ile asali kuuziwa ni kazi san
Huwa naenda kati ya saa nne asubuhi na saa sita mchana.
Mara zote nulizoenda ni zaidi mara kumi napewa control no nalipa kwa simu au kwa wakala hapo nje.
Hata kesho nitapita ,nikishindwa kupewa control no itakuwa kwa mara ya kwanza
 
Hao wana hujumu haiwezekani kila siku mtandao uwe hakuna kwao tu
 
Kwa hiyo ukiila Asali unakuwa kama umevuta Sigara?
Hapana lakini wataalamu wanasema ukiila ni kama vile umevutishwa sigara sawa na wavutaji wanapovuta ukikaa karibu nao wewe ndo unavuta zaidi maana wewe ni recipient ambaye hutaki ila unavutishwa.
 
Maduka ya serikali?
Ndio nasikia leo.
Pale darajani kuelekea kariakoo ambako ilikuwa wizara ya maliasili na utalii lile jengo la wizara [Mpingo House]limeachwa chini ya usimamizi wa idara ya maliaasili na utalii wapo mpaka wakala wa misitu Tfs sasa pale kwa mbele barabarani kuna vifremu kimoja ni atm ya Nmb na kingine ndo idara ya mali asili wamefanya kama duka sio asali tu vitu vingi vya utalii na misitu wanauza ila ndo mchakato wake kama anavolalamikia mdau apo juu.
 
Hivi serikali bado ina maduka?
Nilijua haya mambo yalikua enzi za ujima huko?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…