Ulivyokuwa mdogo ulikuwa na ndoto ya kuja kufanya kazi gani?

Ulivyokuwa mdogo ulikuwa na ndoto ya kuja kufanya kazi gani?

Mimi kusema kweli nlitaka tu kuwa dereva hasa hasa wa malori ya masafa ili nitembee niione dunia.
Nmefika class 7 nkwambia mshua mi shule staki tena nataka kuwa dereva.
Akanipeleka seminari.
Nmemaliza form 4 nkakumbushia, akaishia kunitaftia leseni na kuniambia umri wa kuendesha lori bado miaka 3 kwaio nenda advance kwanza. Nkajidanganya nkaenda. Wooi, nmemaliza nkaishia kusomea udaktari.
But one day yes, ntashika chuma yangu nianze kuitalii dunia.
Nipo upande wa Mzeee! Daktari ni bora.
 
Leo nimekumbuka kipindi nipo mdogo nilikua na ndoto ya kuja kua Miss Tanzania.

Akili yangu yote ilikua inajua Miss Tanzania ni kazi kama daktari, mwanasheria, mwalimu au kazi zingine.

Nilivyofika form 1 ndo nikajua kumbe sio kama nilivyodhani, hapo nikapata mawazo ya kua mwanauchumi mpaka sasa napambania ndoto yangu.

Mliotimiza ndoto zenu nyoosheni mikono juu tuwapigie makofi!😹
Padri. Niachana na hayo mawazo baada ya kufukuzwa seminary.
 
Ukiwa mdogo utatamani kufanya kazi za watu waliokuzunguka.

Wakati wa ukuaji wangu watu walionizunguka walikuwa Wanajeshi wa JWT, Walimu wetu shuleni na Madaktari.

Ndoto yangu ilikuwa kuja kuwa Rubani na baadaye kuwa Banker.

Nimeishia kufanya kazi ambayo wengi huitamani ingawa ukiwa limbukeni huchelewi kufa haraka 😎
 
Kubet sio kazi
Maisha ya tz ni kubeti , unalima unabeti mvua inyeshe , unafungua biashara unabeti wateja waje , wasipo kuja mkeka wa sku unachanika , unafungua mgahawa una bahatisha wateja waje wasipo kuja chakula una mwaga , unabeti Mungu yupo na haujawahi mwona ili ukifa ubeti kwnda peponi , unabeti unaenda kulala , kesho ukiamka utafanya jambo fulani na hauna uhakika kama utaamka, maisha hauwezi yatenga na kubeti hasa nchi zetu za ulimwengu wa tatu.
 
I got your point!
 
Back
Top Bottom