Ulivyokuwa mdogo ulikuwa na ndoto ya kuja kufanya kazi gani?

Nipo upande wa Mzeee! Daktari ni bora.
 
Padri. Niachana na hayo mawazo baada ya kufukuzwa seminary.
 
Ukiwa mdogo utatamani kufanya kazi za watu waliokuzunguka.

Wakati wa ukuaji wangu watu walionizunguka walikuwa Wanajeshi wa JWT, Walimu wetu shuleni na Madaktari.

Ndoto yangu ilikuwa kuja kuwa Rubani na baadaye kuwa Banker.

Nimeishia kufanya kazi ambayo wengi huitamani ingawa ukiwa limbukeni huchelewi kufa haraka 😎
 
Kubet sio kazi
Maisha ya tz ni kubeti , unalima unabeti mvua inyeshe , unafungua biashara unabeti wateja waje , wasipo kuja mkeka wa sku unachanika , unafungua mgahawa una bahatisha wateja waje wasipo kuja chakula una mwaga , unabeti Mungu yupo na haujawahi mwona ili ukifa ubeti kwnda peponi , unabeti unaenda kulala , kesho ukiamka utafanya jambo fulani na hauna uhakika kama utaamka, maisha hauwezi yatenga na kubeti hasa nchi zetu za ulimwengu wa tatu.
 
I got your point!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…