Uliwahi kuonesha jeuri ya pesa hata kama huna, ili kulinda heshima?

Nakumbuka mwaka 2014 binamu yangu anatoka school yupo kituoni anasubiria gari apande na mfukoni ana nauli tu ya kufika nyumbani


Anatokea mwanafunzi wa kike anamuomba amsaidie nauli apande daladala

Bila hiyana anampa nauli demu na yeye anatembea kwa mguu, hadi home

Nikajisemea hizi sifa nyingine na kulinda heshima ili usionekane mnyonge ni za kipuuzi
 
[emoji23][emoji23][emoji23]

Dah! Mshikaji supu kaitia nazi
 
Amini kwamba [emoji119]

Yani ni temporary events tu, yanini yote hayo
 
Dharau zina umiza ila mimi kutokana na jinsi navyo jikubari ninge mwambia boda tungeuze maana na jua baada ya hapo pesa inauma kuliko hata dharau ANGALIZO usi kabiliane na maumivu kwa kutengeneza mazingira ya kuumia baadae
 
😂😂😂 mimi ningekufa, yani tako tatu wazungu shwaa alafu inajirudia
 
Nakumbukaga zile za kwenye vizibo enzi za mkapa maana kikwete ni soda tu na laki wanatoa basi ikaishiliaga hmsini nilikuwa mdogo primary .
Unafungua soda za bonite unasoma kizibo nilipataga laki na udogo wangu tukabiwa tuende ofisini kupokea hela za ushindi
 

Safii mkuu si jambo baya. Ila samaki wa hapo uliwaonaje mkuu ?
 
Mimi ndo nipo nasumbua ndugu hapa wanikopeshe walau alfu kumi.

Hii ni baada ya kulipia bili za watu wote niliowakuta mgahawani jana
Kwa tsh 86500.

Ni stori ndefu kidogo lakini tu kiufupi dharau zinaumiza sana.
Hahahaaaa nikajua ni peke angu kuona dharau inaumiza
 
Ilinitokea miaka hiyo nikiwa sekondari, siku moja asubuhi(mimi na ndugu yangu) tumetoka kwa sista. Sista alikua na safari ya nairobi kwahiyo ikatulazimu turudi nyumbani mkoani kwakua alihofia kutuacha wenyewe. Tukapewa nauli na baada ya kuona hela tukaona hatuna muda wa kupoteza tukaaga mbio mbio hata chakula hatukula tuliona kitatuchelewesha.

Tukafika town tukashauriana tuingie mahali tuchambe koo na juice plus kuku kidogo then tuamshe. Tulifika na kupokelewa na pisi moja ya kimbulu kali sana(huu ndio ugonjwa wa huyu ndugu yangu mpaka kesho alafu ni mbishi akitaka jambo lake lazima liwe). Nikamnong'oneza ndugu yangu hapa bei zao sio size yetu tumevamia kambi tutafute sehemu nyingine, mwamba akagoma akasema pesa si ipo leta vitu. Nikaagiza juice, inakuja juice naona na misahani shazi, nikauliza kiuwoga nikajibiwa huwa wanauza special package(hapa tulipigwa plus ushamba). Tukaulizwa turudishe au mtakula? Ndugu yangu akaropoka tutakula mbona ni jambo dogo sana, basi tukala tukamaliza bili inakuja hatukubaki hata na nauli, tulivyotoka hapo nilikua kama bubu kimya tulitembea hadi kwa dada tulivyofika tukamwambia asijali sisi tutabaki tu hamna shida, alituelewa 😂😂 sitosahau hiyo siku niligongwa na mvua sana.
 
Huyo mkeo ni Kama mie tu,na haya majuba watu wanatuonaga washamba,nawakomeshaga hatari,utasikia tu upo vizuri.
 
Kwakweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…