Uliwahi kuonesha jeuri ya pesa hata kama huna, ili kulinda heshima?

Mie nimejiwekea ka utaratibu kakuuliza bei Kwanza sikurupuki aisee,


Nilijichanganyaga siku moja nilikuwa na wenge,

Nilikuwaga Safari nikanunua korosho nilitoa buku ten,akanirudishia buku moja,nikatulia Kwanza nikajua kafuata chenji,. Nikatulia kwenye benchi nikaona kimya hatokei,nikamfuata nikamuuliza hizi ni buku Tisa?? Akasema ndio
Nikamwambia hatukuelewena nahitaji za buku,hahahaha nashukuru alinielewa akanirudishia pesa yangu,

Japo niliumia pia hizo za buku hata kumi hazikufika,
 

[emoji23][emoji23][emoji23]
 

[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Dah mlitisha Sana mabaharia 😁😁
 
We uko kama Mimi Tu,unajua wakati mwingine ili kuondoa aibu ndogo ndogo ni Bora ujue bei mapema kuliko kuja kutukanwa baadae,kuna sehemu soda 1,000 kwengine 6,000 na 8,000 haya ndo umejichanganya kwenye buku 8 hlf huna hiyo hela si aibu hiyo?

Na hii nilijifunza hata Kwa wazungu huwa wanauliza bei Sana,siku moja tulitoka nao out Yani wanauliza bei fresh Tu, kwahiyo ndio nikazidi kupata hamasa ya kuuliza kabla ya huduma
 
Kabisa nikitu kizur sema watu wanaona aibu.
 
Nilikua na 2000 tu alaf dem wa chuo nlietoka kumtongoza siku km 3 nyuma akaniambia hana vocha, nikasema mmh uyu nikimuonyesha unyonge mapema itakua jau, nikamuungisha bando la 1500 uku m nikabaki nawaza ntakulaje iyo siku.
[emoji23][emoji23]
 
Mie nijue bei Kwanza,habari za kujutia siwezi,
 
Kuna pisi moja nilionana nayo kiwanja kimoja usiku mida ikawa imeenda sana tukapeana number nikawa naitafuta mara moja moja.

Ijumaa ikanitafuta mapema kuwa usiku tuonane, mida ilivyowadia ikawa wote tumefika mahali tulipokuwa tumeahidiana. Akawa amekuja na rafiki zake wawili na mimi pia niliongozana na mshikaji wangu tunayefanya wote kazi naye alikuwa anakutana na jamaa zake hapo. Sasa bata likaanza pasipo kuwekeana limit.

Mida imefika watoto washachangamka wanataka tusepe kiwanja kingine. Nikamuita mhudumu ili anipe bill, mhudumu akaniletea receipt ya efd machine inasoma 498,000/= basi nikajipindua Atm chaap nikachanja nikarudi nikalipia.

Watoto wakasuggest kiwanja kingine tukachoma ndani ya mchuma washkaji wawili mademu watatu, tukiwa njiani wakasema huko tunapoenda show ni ya kwao sisi tumemaliza show yetu. Sasa huko ndiyo nikajua nipo na aina gani ya pisi huko watoto wa kike walichoma hela mpaka tukawa tunasema na mwanangu hawa mademu wanataka roho zetu nini? Baada ya hapo wakasema tuwapeleke maskani yao kuwafikisha bado tulikuwa tunaona ni ndoto apartment wanayokaa si mchezo. Show ikaendelea tena maghetoni kwao the rest is history.

Kwa kifupi wale watoto walikuwa wapo njema kuliko mimi.
 
Et ki Bob Marley😅😅😅
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…