Nilifika kwenye bar mojaa kijiweni 2022 mwanzoni
Kufika kutoa salamu kwa jirani zangu hawakuniitikia salamu kutokana na kuonekana mlugaluga tu
Sasa nilienda na bodaboda sikuhiyo
Nikala msosi wa 4,000 kwa kutoa 2000 mfuko wa nyuma na iliobaki mfuko wa mbele
Wadau na warembo wananiangalia marakwa mara nikitabasamu wananicheka kuona sio level zao
Kilichofuata
Kesho yake jumapili nikawakuta wanakunywa kijiwe kile kile
Kwanza kutokana na gari kuwa gerage, fundi alinipa gari nyingine nitumie kama siku tatu,
Kufika bar kwanza kuanzia mbali wanaangalia nani atakaeshuka
Nikashuka kilugaluga kama kawaida
Nikakaa karibu yao ,
NILIPEWA SALAMU NA WAO , wahudumu wakawa wanapishana kwangu ,
ILI KULINDA HESHIMA NISIONEKANE NABAHATISHA NIKATOA OFA KWA WAHUDUMU WANNE BIA 20 , kitimoto kilo 3
na wadau wangu walipokuja nikanunua hia meza za jirani walioonesha dharau
Nilichafua meza zote za karibu pale
Nilinunua bia zaidi ya 70
Nilispend karibu 360,000 wakati ni hela ya fundi na nilikuw na matatizo ya cash wiki hio,nikajitoa ufahamu tu
Baada ya hapo boss wangu akaja nae kuunga mkono juhudi
Bos wangu alimwaga bia na rafiki zake. Bill ikafika 680,000 zaidi
Jumla ya bill tulilipa mil 1.3 plus hadi kunakucha
Baada ya hapo NASHANGAA BAADHI YA WAHUDUMU NA KUNDI LA WANYWAJI WALIOKUW WANADHARAU VIJANA NIKIKUTANA NAO WANANIAMKIA
MTU MNARINGANA UMRI ANAKUAMKIA SERIOUS????????
Dharau ni mbaya sana, zitakuaibisha siku moja, nimekutana na mikasa kedekede na uzuri mimi ni raia wa wakawaida kwahiyo sioni taabu kuchukuliwa poa