Uliwezaje kuukubali ukweli kuwa sasa wewe ni mtu mzima? Bado sijui nimefikaje gorofa ya 30!

Uliwezaje kuukubali ukweli kuwa sasa wewe ni mtu mzima? Bado sijui nimefikaje gorofa ya 30!

Ukubwa majukumu. Kuzeeka lazina, kuchakaa uamuzi
Ronaldo ni mdogo kwa Rooney
Masudi kipanya ana miaka 52, Dully sykes 42, Kikwete 73, mzee. Ruksa 98, Magufuli alikufa na 62, Skudu ana 30, Onyango 25. Umri ni namba tu usiogope
Ulitaka kumaanisha Rooney ni mdogo kwa Ronaldo?
 
Wakati Nina kama miaka 20 hivi Kuna brother mmoja alikuwa na miaka 26 na alikuwa hajaoa basi nikawa namshangaa sana kwann jamaa age imesogea alafu hata mke Hana.???????

Lahaulla kumbe nlikuwa najiongopea Bure Mimi nilikuja kupitia hiyo miaka na nikawa hata wazo la kuoa Sina na maisha hayajakaa sawa.!

Nimekuja kubutua na miaka 30 ndio huyo kuchukua jiko

Uzee Huwa unakuja ghafla sana !

Usishangae kumuona mwanaume na miaka 40 anatongoza bint WA miaka 16 ukamuona WA ajabu ni kuwa hata yeye anahisi hiyo 40 Hana na bado anajiona kama yupo 25.

Uzee haukubaliki wanangu
Uko sahihi kuna ile sense unahisi bado ya kukataa ukweli kwamba sasa umekua mtu mzima, hata mimi na fewl hii kitu
 
Mi zilianza shikamoo za watoto mtaani, nilishtuka kisha nikazoea, zilipoanza za mabinti na vijana duh ndio nikajua umri unasogea

Nilivyoanza tu kuungwa kwenye magroup ya michango ya harusi na mwenyewe kutamani kuoa nikajua ndio nishakua sasa

Nashukuru Ujana nimeutumia vizuri tena sana.
 
Back
Top Bottom