Uliwezaje kuukubali ukweli kuwa sasa wewe ni mtu mzima? Bado sijui nimefikaje gorofa ya 30!

Ukubwa majukumu. Kuzeeka lazina, kuchakaa uamuzi
Ronaldo ni mdogo kwa Rooney
Masudi kipanya ana miaka 52, Dully sykes 42, Kikwete 73, mzee. Ruksa 98, Magufuli alikufa na 62, Skudu ana 30, Onyango 25. Umri ni namba tu usiogope
Ulitaka kumaanisha Rooney ni mdogo kwa Ronaldo?
 
Uko sahihi kuna ile sense unahisi bado ya kukataa ukweli kwamba sasa umekua mtu mzima, hata mimi na fewl hii kitu
 
Mi zilianza shikamoo za watoto mtaani, nilishtuka kisha nikazoea, zilipoanza za mabinti na vijana duh ndio nikajua umri unasogea

Nilivyoanza tu kuungwa kwenye magroup ya michango ya harusi na mwenyewe kutamani kuoa nikajua ndio nishakua sasa

Nashukuru Ujana nimeutumia vizuri tena sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…