Ukitaka furaha ishi kama vile upo milele duniani
Ila ukitaka ukose furaha na maana ya maisha haya fikiria kifo
Nini maana ya maisha kama kuna kufa? Mtu unasoma kwa shida miaka mingi ,unahangaika na utafutaji wa mali na vitu mbalimbali
Unazurula huku na kule mara miaka 60+ hii hapa ,mara 70.Na kwa maisha ya mlala hoi mara nyingi hata hapo hutoboi .
Kama tungekuwa tunajua siku ya kila mmoja ya kuondoka humu duniani sijui ingekuwaje
Nazani amani ingepungua mana kungekuwa na baadhi ya watu wangekuwa wanafanya vitu vya ajabu kisa tu salio lao linataka kukata.
Maisha ya sasa kutoboa 80yrs ni nadra sana na huenda inaishia kwa wazee wetu tu.ila kwetu na kwa vizazi vyetu itakuwa si rahisi hata kidogo.
Tuombe mwisho mwema tu,age is just a number waswahili husema ,tufurahie uwepo wetu bila kujari tuna umri upi,just enjoy kwa kile ulicho nacho.
Ukipata mvi furahi mana kuna wengine hawakuzipata ,
Ukifika 30 furahi ,ukifika 40 furahi ,ukifika 50 furahi sana ukifika 60 ongeza furaha ,ukifika 70 aaah we furahi kabisa,ni wachache sana wanafika hapa kwa miaka hii
Mtu asikudanganye eti ujichukie kwa umri kuongezeka ,hayo ndo maisha,uwe nacho au usiwe nacho ,ni matokeo tu hayo,ila maisha halisi ni ile hali ya wewe kuwa mzima na afya njema .
Ukiweza kumudu mahitaji yako mhimu na ya wapendwa wako basi furahi sana .
We are just passing guys,ishi maisha yako ,jali afya yako,pendwa wapendwa wako ,ishi kadri ya riziki yako ilivyo,hakuna anae jali maisha yako hata kama ukiondoka leo,just be happy ,hakuna aijuaye kesho yake.