Uliwezaje kuukubali ukweli kuwa sasa wewe ni mtu mzima? Bado sijui nimefikaje gorofa ya 30!

Uliwezaje kuukubali ukweli kuwa sasa wewe ni mtu mzima? Bado sijui nimefikaje gorofa ya 30!

Ukubwa majukumu. Kuzeeka lazina, kuchakaa uamuzi
Ronaldo ni mdogo kwa Rooney
Masudi kipanya ana miaka 52, Dully sykes 42, Kikwete 73, mzee. Ruksa 98, Magufuli alikufa na 62, Skudu ana 30, Onyango 25. Umri ni namba tu usiogope
Labda Onyango wa Yombo Dovya siyo huyu ninaemjua mimi wa team Madelu
 

Attachments

  • download.jpg
    download.jpg
    11.6 KB · Views: 2
You guessed wrong.

Nenda jukwaa la ajira na tenda uone ninavyotembeza cv tangu 2017
Kwa maana hiyo Kama sijakuelewa vibaya bado unatafuta ugali (ajira) na bado hujaupata. Sasa say tokea 2017 unasambaza cv ina maana mpaka Léo ni miaka 6. Kwa hesabu ya harakaharaka muhitimu wa chuo kwa standard anamaliza akiwa na miaka 23. Kwa hiyo say ulimaliza na miaka hiyo, tukiongeza sita ya kutembeza cv maana yake una 29 kwa Sasa.

Sasa basi, naona unakaribia kutuacha maana miaka miwili ijayo tu utakuwa unafikisha hiyo 31. Ila siwezi kujua maana raia anapiga madeal makali within a month na anafanya yote hayo. Ila ndg kwa kuwa bado unatembea CV naona kama huna muda kutekeleza hazma yako ya kujinyofoa roho. Utamsalimia mwenda zake Kama utabahatika kufika aliko
 
Zipo nyingi but naion hii ndio weirdest one [emoji38][emoji38][emoji38]

Nilivyokua nikipita sehem alaf nisikie harufi nzuri ya msosi upo jikon basi nitapata hisia kali sana ya kwamba " it's mimi niko na familia yangu ( my wife and children) huku wife anarekebisha jikoni " hivyo nikaona huu utu uzima huu unaninyemelea
Yeah same to me
 
Napata wakati mgumu kupokea shikamoo barabarani, kwakweli wataki niko teenager, sijui nilikuwa nachukuliaje nikisikia mtu anamiaka 25, 30 nk.

Napata mashaka kwamba hata miaka 40 na 50 itafika kiutani utani na nitaanza kuitwa mzee bila mimi kujua nimefikaje fikaje hapo!

Uliwezaje kukubaliana na ukweli?
Whereas growing up is optional; growing older is mandatory
 
Ukitaka furaha ishi kama vile upo milele duniani
Ila ukitaka ukose furaha na maana ya maisha haya fikiria kifo
Nini maana ya maisha kama kuna kufa? Mtu unasoma kwa shida miaka mingi ,unahangaika na utafutaji wa mali na vitu mbalimbali

Unazurula huku na kule mara miaka 60+ hii hapa ,mara 70.Na kwa maisha ya mlala hoi mara nyingi hata hapo hutoboi .
Kama tungekuwa tunajua siku ya kila mmoja ya kuondoka humu duniani sijui ingekuwaje

Nazani amani ingepungua mana kungekuwa na baadhi ya watu wangekuwa wanafanya vitu vya ajabu kisa tu salio lao linataka kukata.

Maisha ya sasa kutoboa 80yrs ni nadra sana na huenda inaishia kwa wazee wetu tu.ila kwetu na kwa vizazi vyetu itakuwa si rahisi hata kidogo.
Tuombe mwisho mwema tu,age is just a number waswahili husema ,tufurahie uwepo wetu bila kujari tuna umri upi,just enjoy kwa kile ulicho nacho.
Ukipata mvi furahi mana kuna wengine hawakuzipata ,

Ukifika 30 furahi ,ukifika 40 furahi ,ukifika 50 furahi sana ukifika 60 ongeza furaha ,ukifika 70 aaah we furahi kabisa,ni wachache sana wanafika hapa kwa miaka hii
Mtu asikudanganye eti ujichukie kwa umri kuongezeka ,hayo ndo maisha,uwe nacho au usiwe nacho ,ni matokeo tu hayo,ila maisha halisi ni ile hali ya wewe kuwa mzima na afya njema .
Ukiweza kumudu mahitaji yako mhimu na ya wapendwa wako basi furahi sana .

We are just passing guys,ishi maisha yako ,jali afya yako,pendwa wapendwa wako ,ishi kadri ya riziki yako ilivyo,hakuna anae jali maisha yako hata kama ukiondoka leo,just be happy ,hakuna aijuaye kesho yake.
 
Back
Top Bottom