Umaskini wa nchi yetu nani alaumiwe?

China ni magiant kwa umri wake hata wazungu hawafikii, amefanya mambo makubwa huko kale,
Ukienda huko kale waafrica ndo tulitisha sana tuliwatoa tongo tongo wazungu

Soma ancient egpyt utajua mwafrica alichofanya tena leo moja ya kazi zetu inaittwa maajabu ya dunian.

Piramidi ya misri inayoitwa Giza piramidi. Sisi siyo watu wadogo huko nyuma.

Ushahidi mwingine Soma biblia isaya 18. Utaona sifa ya mwafrica biblia inasema taifa wakagao watu tangu mwanzo wao
 
Hadi unaandika uzi huu, umeifanyia nini nchi yako?
Usimshambulie,we umeifanyia nini nchi.Hata hivyo wenye nyadhifa hawajaifanyia kitu aje kuwa yeye mwanaJEIEFU!
 
kwanza kabisa sie kama taifa sio maskini KABISA, tatizo lipo sehemu nyingi tofauti tofauti mfano wale tuliowapa mamlaka kuwa na tamaa,elimu,siasa na sera ambazo haziendani na uhalisia. Ipo siku nasi tutakua kiuchumi kama nchi nyingine zilivyo sasa lakini tukubali kulipa gharama ya kufika huko kama jamii tuwe na mtazamo wa kuhitaji kweli kufika huko, hawa viongozi wasio waaminifu **** zao naumia kinoma jinsi wanavyotumbua TUNU za taifa hili na kiama kitafika! pale unapokaa na kutafakari siku tukishinda ukiritimba huu hakika Africa nzima kwa rasilimali tulizona hakuna wa kutuweza.
 
Mimi naona viongozi hasa ndo wanatuangusha!
Haiwezekani kila kiongozi ni tajiri!
 
 
Tuanzie hapa kuufuta umaskini.
Naomba wanajukwaa tufanye mpango wa kuunda timu yetu ya mpira au benki ili tununue na kuuza hisa ama tutege kitega uchumi kingine kikubwa maana wanaJF tupo wengi na naamini wengi vijipesa vya mboga tunavyo!
Yaani sisi tumebahatika kujadili hali ya uchumi wa nchi yetu,basi CHANGE IS IN US!
 
Katiba ibadilishwe ili mamlaka na nguvu irudi mikononi mwa wananchi na sio kakikundi ka watu wachache ambao wamejimilikisha kila kitu kuanzia maamuzi,madaraka na rasilimali mfano mzuri ni kikokotoo cha wastaafu ambao wanalipwa 33% ya jumla ya mafao yao na uamuzi huo umefanywa na watu wajinga,wabinafsi wachache ambao wenyewe hayo makato hayawahusu pindi wakistaafu“UBINAFSI WA HALI YA JUU”.watendaji serikalini wapunguzwe mfano hakuna haja ya kuwa na vyeo vya kisiasa ambavyo havina manufaa kwa mwananchi wa kawaida mfano wakuu wa wilaya,makatibu tawala wa wilaya,wakuu wa mikoa na badala yake wabaki katibu tawala mkoa na wakurugenzi,tutaokoa pesa nyingi sana.mishahara ya wabunge ipunguzwe maana watu wanakimbilia kwenye ubunge kufanya biashara ya kisiasa na sio kumsemea na kumtetea mwananchi .kuwe na tume huru ya uchaguzi ili kisiwepo kikundi cha watu wachache wenye hati miliki na hii nchi maana wanafanya ushenzi na wizi wanaotaka kwa kuwa wanajua kwa vyovyote vile watarudi madarakani hata kama hakuna walichokifanya kwa miaka 5.MZIGO MKUBWA WA NCHI HII WAMETWISHWA WANANCHI WA KAWAIDA WANAOKAMULIWA KODI ZA OVYO NA PESA HIYO INAYOTUMIKA KUWALIPA WANASIASA WA OVYO NA WASIOKUWA NA FAIDA NA NCHI ZAIDI YA KUTUSABABISHIA MAISHA MAGUMU
 
Mkuu mtoa mada kaongelea umasikini at National level,wewe unatoa mawazo yako at family level-na hayo mawazo yako nayo sio sahihi China policy wa kuzaa watoto 2 ni kutokana na Idadi kubwa ya watu.
Western countries wanazaa watoto wachache kutokana na rasilimali chache walizonazo tofauti na sisi.
Changia kutokana na hoja iliyotolewa sio unatengeneza hoja yako kisha inaichangia.
 
Tatizo ni mfumo mbovu wa Ujamaa. Ujamaa ndiyo uliharibu viwanda, uliharibu biashara za watu, uliharibu kilimo na ndiyo chanzo kikubwa cha ufisadi.

Kwa sababu western wameandika hivyo basi nawe unaona ni kweli.western walipoanzisha mfumo wa kibepari ilikuwa ni lazima wauponde mfumo wa ujamaa ili kuhakikisha mfumo huo unasambaa duniani,lakini sio kweli kwamba ndio chanzo cha umaskini.
Haya viwanda vyote tulivyokuwa navyo wakati wa ujamaa-vimepelekwa wapi ulipoanza ubepari??
 
Umaskini wa nchi = umaskini wa wananchi.
Hivi unaweza kusema shule inafaulisha wakati wanafunzi wote wamefeli?
 
Ioo pyramid mbona washajimilikisha, sisi wametuachia ngome ya washona na ya ghana kule.

Labda niseme kwa nchi ambazo mipaka yake ipo tokea longi. Kwamba watu washajiongoza sana na sio malimbukeni tena wa kuongoza.

Shida hawa viongozi wetu wanajisikia sana kutuongoza, wanadhani kama wanastahili, ni haki yao kumbe nguvu yao inatoka kwetu.
 
na kingine cha muhimu ni raia,popote duniani kuna nchi ni visiwa tu lakini wako vyema sasa rasilimali kuu ni sie raia (intelligence level)
 
Sisi wenyewe wananchi wa nchi hii 🤔
 
Afrika Kama isipo fanya mageuzi ya akili kwa watu wake hakika tutakuwa third class citizens katika ulimwengu huu for our rest of life
 
Toka mwinyi hadi Leo ni miaka mingapi?

CCM bado inafuata mfumo wa Ujamaa. Soma ilani yao ya uchaguzi

 

Viwanda na mashirika ya umma viliendeshwa kwa hasara vikawa vikawa vinafilisi nchi.
 
Lakini Rais Samia amekuja kuleta mapinduzi ya maendeleo mpaka vijijini miundombinu imeboleshwa maji mpaka vijijini umeme unapatikana mpaka vijijini kwaiyo tutegee makubwa zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…