Umenikumbusha mbali sana aisee.
Mwaka 2015 (14/11/2015 siku ya Ijumaa saa kumi jioni) nikiwa Form Five nikavunjika Mkono ninaotumia kuandikia.
Balaa linakuja nasoma PCB, 2016 April nafanya paper ya Robo Semster nikawa wa pili kutoka Mwisho katika combination ya PCB.
Katika Maisha yangu ni wale watu wakuchukulia mambo kimatani matani na mizaha Mingi ya Kuchekesha si unajua tena ukimkuta msukuma comedian.
Baada ya kuwa wa pili kutoka Mwisho nilijiapia sitokuwa wa mwisho tena bali nitakuwa wa Juu.
Napiga Paper ya ACSEE May/2017 nafanikiwa kutoka na ufaulu mzuri kabisa hadi namshangazaa Mwalimu mkuu wa ile shule.
Mwaka ule ule mwezi Novemba/2017 naingia Chuo na Course ya Computer Science, Medicine sikufanikiwa kupata Nafasi UDOM na Mhimbili.
Ndoto za MD zikaishia pale pale, nikaenda kupiga course ya Computer Science, kwa kweli course hiyo sikuipenda hadi nafika mwaka wa 3 do sasa inakuja imani nipambane nimalize chuo nirudi home nikawe mkulima.
Kipindi niko chuo mwaka 2019 nikapataga nafasi ya Kujitolea katika Hospitali fulani ya Rufaa, ikajaga kutokea wizi wa Desktops nikaachiwa msalaa kwamba mimi do nimeiba nikafukuzwa April/2019.
Mei/2019 natapeliwa Na Mkinga fedha ya Ada, Bumu. Kama kawaida yangu sikuwa na pressure niliamini ipo siku mambo yataenda sawa.
Mwaka 2020 na graduate chuo kimiujiza miujiza, Mungu huyu acha aitwe Mungu.
Mwaka 2021 Januari nikapataga kazi Serikalini, Daaaaaaah.
Fani niliyosoma niliamini sitokuja kupata kazi, unapanga na Mungu naye anapanga lake.
Hakuna kukata tamaa, tupambane hadi tone la Mwisho.