Umeshawahi kutana na koboko(black mamba), uliescape vipi maana huyu sio wa mchezo

Umeshawahi kutana na koboko(black mamba), uliescape vipi maana huyu sio wa mchezo

Hata nyegere/honeybadger nae sumu ya nyoka inamlaza kidogo tu kisha anazinduka
black mamba anauwezo wa kumdondosha tembo, akini hyu nyoka hodari analiwa na nyegere (honey badger), ambaye anakiga ya kuzaliwa dhidi ya sumu ya nyoka yeyote
 
Ana mbio balaa mkali sana na ni mpole pia
Anauwezo wa kugonga ng'ombe 20 kwa wkt Moja wakafa wote
Ukikutana naye tulia tulia maana yupo shap .ukijaribu hata kuokota jiwe au silaha umekufa
Sumu yake Ina protin ya hali ya juu sana ikinywewa . tatizo uwe na uhakika huna mchubuko wowote tumboni
 
kwa upande wangu sikawahi kutana nae ila nisikia ni hatare sana na wanasema sana sana anptkn Tabora, kanda ya ziwa ,Dodoma na Mbeya
Kama ushawahi kutana nae share nasi tujifunze😁
Sisi huko kijijini tulikua hatuescape bali tunamuua pindi akionekana.
 
Nimewahi kukutana nae huko ngara mbili, sikonge tabora, japo hakuwa fully grown up ila alipita kwa speed kubwa mbele yangu.

Huyu nyoka mara nyingi anaepusha shari anakukwepa, ila ukiyataka mwenyewe uwe tayari kuimbiwa ule wimbo wa parapanda, wasukuma humuua kwa kumzunguka na kumkera kwa makelele halafu wanamrushia vipande vya miti anavigonga mpaka anachoka kisha ndo wanamuambush kwa pamoja.
IMG_20190909_105721.jpg
Huyu koboko wetu ameshushwa hadhi tu kwasababu hayupo kwa wazungu, ndo maana utasikia yule Taipan wa Australia ndo anaongoza wakati fujo za koboko wetu kuwa aggressive kuliko huyo Inland Taipan ziko wazi amewaua sana wajerumani wakati wanafanya survey uchwara huku enzi hizo, karibu na ngara mbili ni hapo.
 
Nimekutana nae mara mbili. Mara ya kwanza alikuwa anakatisha barabara ambapo nami nilikuwa napita, nilivyomuona ametulia tuli na kuinua kichwa kiasi, aisee nikajisemea hapa si pa kusimama, kuhoa wala kurusha jiwe. Ni hatari mwanangu, mwamba ni mkubwa na mweusi. Urefu na kichwa chake jumlisha unene wake karibia tairi ya mbele ya TVS/Boxer.

Mara ya pili ilikuwa uso kwa uso akikatisha kwenda kichuguu na nilimtambua ndani ya mita 5, eee buana ngoja niishie hapa.
Huyo sio koboko, yule jamaa rangi yake ni ya kijivu na huwa hanenepi saaana anakuwa mwembamba akikua sana ndo anaongezeka kidogo unene ila ni mrefu sana na huwa hasimamii kichwa anasimama karibu mwili mzima hasimami kama cobra hapana, huyo mweusi uliyemuona ni swila huyo.
 
Nilimuona akiwa amekufa, alikua anavuka barabara akagongwa na gari aisee yule mdudu ni mkubwa na anatisha tulimpima urefu alikua na futi 5 na point aisee, ukikutana nae mzima kimbia tuu kwa jinsi nilivyomuona mtu mbili hutoboi qmmk.
Huyu pia sio koboko, huyu jamaa ana akili sana mpaka umpate kwa tairi umefanya kazi ya ziada na ukimgonga anatulia tuli kwenye chassis kisha mkifika mwisho wa safari yenu ana nyie, mtamueleza sheria za wanyamapori wakati zinafundishwa mlikuwa wapi.

By the way koboko ndiye miongoni mwa nyoka wenye akili zaidi duniani, na hiyo size unayoisema si hata mimi nimemzidi urefu? hawa koboko wanafika mpaka futi 14 na wanazaliwa na roughly kama futi mbili kwa urefu, so nasema huyo sio koboko.
 
Mimi nilikutana Naye mbugani akawa anainua kichwa chake.Nikambana na mti kichwa chake na nikamshika mkia wake nikaanza kumzungusha juu Hadi akalegea na kumng'oa meno yake.Nilifanya Hivyo Kwa kutomjua kuwa alikuwa ni black mamba Hadi pale watu wanaojua nyoka wakaja wakamtambua Kwa jina na wanasema nilikuwa nacheza na moto
Nyie wakuu acheni kutufunga kamba, koboko yupi umfanyie huo mchezo? kwanza koboko meno yake ni kama meno ya mbuzi umtoe kirahisi hivyo?! maana koboko akiuma huwa haachi meno anachoma kama sindano anashusha venom mls kadhaa anakuacha hapo, kisha miaka ya nyuma enzi ya Samuel sitta kule urambo walipeleka kikosi kazi kwaajili ya kuwapunguza hawa wakuu.

Wadau wa mazingira tukashauri kuwa waachane na huo mpango maana koboko kwa risasi kumpata ni nadra sana, inatokea ila ni nadra sana kutokana na speed yake ya kukwepa na intelligence yake, sasa wewe umshike koboko kwa mkono eti umzungushe juu mpaka alegee, huyu nachelea kusema labda ilikuwa ni fimbo kavu ukaifananisha na nyoka bila kujua.
 
Ndio huyu mnaemzunguzia au sio yeye?
 

Attachments

  • FB_IMG_1735916186288.jpg
    FB_IMG_1735916186288.jpg
    76.5 KB · Views: 22
Nilikutana nae mboka nikiwa 13yrs mzee wangu alikua anamashamba ya tambuku chimbo moja hivi lakuitwa igombe ,
Kabla sijamuona tulikua tumeenda kufua kisiman na vijana wa mzee jamaa akaona alama tairi la baiskel lisilo na kashata aka kipara limakatiza barabarani jamaa akaniambia muda simrefu hapa kapita koboko nikauliza umejuaje? Mwamba akaniambia huyo mwamba hatembeagi kwa kujinyonganyonga kama vinyoka vyakipumbavu yeye hujivuta tu kwa mstar mnyoofu ,bas nikapata hio knowledge moja ya mwituni
Sasa tuko zetu kisiman mwamba anafua mimi nimejilaza kwenye mchanga mweupe pee uliopatikana baada kuchimba kisima mbele yangu nikaona nyaka yuko rangi ya khaki nmemkodolea macho kama nimepigwa na butwaa akapita mbele yangu akaja mpaka usawa nilipo akatokomea mgongon huko ata kugeuka nyuma sikuweza alivyopotea kabisa ndio akili ikaja nikamwambia mwamba kapita koboko hapa jamaa akacheka sana akasema angekua koboko saiv ungekua ushabadilika rangi jamaa alikua na haki yakutokuniamin maana nilikua na reputation ya uongo uongo sana kipindi hicho sasa mwamba alivonisogelea siakaona ile alama ya unyayo alioacha chief wa pori akaniambia baba #niyeye hapa tuchape mwendo
Kilichoniokoa mimi adrenalin yangu hakuditekt hatar so sikutoa kijasho cha kujihami wala,sikuleta wenge mwamba akaniona koboko mwenzie tu
Nilivorudi kambini nikamwambia mzee huku uonge mimi nirudishe tu town
Hapa nasadiki, huyu sasa ndio the man himself, the great koboko of kusini mwa jangwa la Sahara, koboko huwa hana neno anaepusha shari mara nyingi, sema ujinga wake ni territorial snake hahami hami kutafuta makazi anashika eneo moja muda mrefu na ana mipaka yake anakata kabisa kuwa miguu kadhaa hapa mpaka hapa.
 
Tofauti na nyoka wengine ukiacha chatu , nyoka wengine wakikuona wanachimba au wana hibernate wao wanashambulia tu wakitishwa
Au chatu anashambulia tu ili ale
Ila koboko master yeye anashambulia for funny tu anaweza kuingia zizini akaruka na ng'ombe kumi halaf akapita hivi au anaweza akakuona kwa mbali akaanza kukulia timing akufanyie unyoka
Hahaha koboko hana cha kukulia timing, anakufuata live bila chenga, yeye ana mchezo mchana wa jua kali anakaa sehemu wanapopita watu wengi, anafunga njia mpaka atakapoamua mwenyewe.

SA wamejaa wengi sana, zimeripotiwa kesi kadhaa anakuja kugonga mlango af anakaa pembeni, ukifungua anakutambaliza.
 
Nyoka karibu wote wana hulka mmoja..... Huwa wanajitahidi sana ku avoid kukutana ana kwa ana na viumbe ambao ni wakubwa kuliko wao, ni hatari kwao na ambao sio chakula chao.

Nyoka wana sense ya hali yajuu kupitia ulimi na macho yao kubaini kiumbe kinacho wakaribia....... Hivyo akikuhisi/ona kwa mbali kabla hujamuona huwa anajificha na kutulia tuli hadi upite

Na iwapo mtakutana ghafla ana kwa ana Kwenye open space au ukambananisha labda ukatani kwakawaida Koboko huwa kwanza lazima asimamishe kichwa na kutoa onyo kwa mlio mkali wa kupuliza, na ukizidi kumsogelea anaweza kukurushia sumu usoni ili kukupa upofu wa muda ili apate nafasi ya kusepa zake

Koboko huwa hashambulii bila warning labda umkanyage ghafla hapo ata attack bila warning

Kumekua na uongo mwingi kwamba ukikutana naye anakufukuzia hadi akung'ate au anaweza kuua hata mifugo mingi zizini just for fun........ Hii sio kweli
Mkuu koboko hawapendi kelele, sasa ng'ombe huwa wana fujo za fuuffffufffff wakiwa wanakula sasa wakikumbana nae huwa anasimama mbele yao kuwapa onyo wakikaidi wanakuja tu, analala nao mbele kama 10 hivi halafu anaondoka zake.
 
z

Hapa nasadiki, huyu sasa ndio the man himself, the great koboko of kusini mwa jangwa la Sahara, koboko huwa hana neno anaepusha shari mara nyingi, sema ujinga wake ni territorial snake hahami hami kutafuta makazi anashika eneo moja muda mrefu na ana mipaka yake anakata kabisa kuwa miguu kadhaa hapa mpaka hapa.
Ukileta ujanjaujanja wa migogoro ya aridhi anaruka na wewe mzimamzima, kuna mwamba ameamin wazingu wa kwenye tv kwamba king koboko akivurugwa hawagi miyeyusho , akiwa ndan ya himaya yake tena awe jike anaetaga jiandae kukimbia 60km/h mixer kuruka meter kadha wa kadha
 
Sio kweli

Sio kweli huyo nyoka ni mtukutu kupindukia angekumaliza mapema tu
Kuna yule jamaa na mke wake kule south Africa wale watu ni binadamu kweli? wale wana matatoo mwili mzima na mabangili bangili, mke sijui ana nywele za orange, wanawashika koboko kama nyoka wa bandia aisee.
 
Ukileta ujanjaujanja wa migogoro ya aridhi anaruka na wewe mzimamzima, kuna mwamba ameamin wazingu wa kwenye tv kwamba king koboko akivurugwa hawagi miyeyusho , akiwa ndan ya himaya yake tena awe jike anaetaga jiandae kukimbia 60km/h mixer kuruka meter kadha wa kadha
Koboko yupi mwenye hizo busara? kwanza ameanza lini kuwa na hizo hekma? halafu akikukimbiza anakupita kwanza halafu mkishakuwa sawa anakuteremshia makwenzi kadhaa ya sumu, unang'olewa makangarii.
 
Huyo ilikuwa nikimuona najihami kwa kukimbia huwa hataki mpishane mara mbili, huwa sio mkali kama watu wanavyosema kwamba akikuona tu anaanza kukuwinda., bali ukimchokoza au mtu alimchokoza wewe ukapita hapo. Au amekuona na bado ukaendelea kubaki eneo lake hapo ndipo huanza kuliamsha labda kama umejiandaa kupambana
Wewe nahisi unazungumzia Tom and Jerry, eti unajihami kwa kufanyaje?.
 
Back
Top Bottom