Hayo ya Nat Geo Wild nashauri uyaache huko, lile onyo la WWE hapa linafit vizuri kabisa "don't try this at home, at school or anywhere". Usije kujaribu kumkamata nawe umweke kwenye mfuko na utarajie kumwacchia akimbilie porini, atakushangaza.
Achana na hao black mamba wa huko kwenye TV wanakuwa kama pets, hawa wa huku Kagera, Tabora, Kigoma nk kwanza wanatumia bangi kama chakula chao cha mara kwa mara.
Ninafahamu matukio kibao yaliyofanywa na koboko. Jambo ninalofikiri hao nyoka kadri wanavyokua wanaingiwa na kichaa, maana matukio yote ninayoyafahamu ni koboko wakubwa (wazee).