black mamba anauwezo wa kumdondosha tembo, akini hyu nyoka hodari analiwa na nyegere (honey badger), ambaye anakiga ya kuzaliwa dhidi ya sumu ya nyoka yeyoteHata nyegere/honeybadger nae sumu ya nyoka inamlaza kidogo tu kisha anazinduka
Nini maana ya Kaboka mchizi?Nilijua ni kaboka mchizi
Sisi huko kijijini tulikua hatuescape bali tunamuua pindi akionekana.kwa upande wangu sikawahi kutana nae ila nisikia ni hatare sana na wanasema sana sana anptkn Tabora, kanda ya ziwa ,Dodoma na Mbeya
Kama ushawahi kutana nae share nasi tujifunze😁
Akiingia ndani unashauriwa ufungue milango na madirisha ili apate nafasi ya kutoka kwa haraka na urahisi.Kwahiyo ukimuona anaingia getoni kwako na penyewe umuache
Huyo sio koboko, yule jamaa rangi yake ni ya kijivu na huwa hanenepi saaana anakuwa mwembamba akikua sana ndo anaongezeka kidogo unene ila ni mrefu sana na huwa hasimamii kichwa anasimama karibu mwili mzima hasimami kama cobra hapana, huyo mweusi uliyemuona ni swila huyo.Nimekutana nae mara mbili. Mara ya kwanza alikuwa anakatisha barabara ambapo nami nilikuwa napita, nilivyomuona ametulia tuli na kuinua kichwa kiasi, aisee nikajisemea hapa si pa kusimama, kuhoa wala kurusha jiwe. Ni hatari mwanangu, mwamba ni mkubwa na mweusi. Urefu na kichwa chake jumlisha unene wake karibia tairi ya mbele ya TVS/Boxer.
Mara ya pili ilikuwa uso kwa uso akikatisha kwenda kichuguu na nilimtambua ndani ya mita 5, eee buana ngoja niishie hapa.
Huyu pia sio koboko, huyu jamaa ana akili sana mpaka umpate kwa tairi umefanya kazi ya ziada na ukimgonga anatulia tuli kwenye chassis kisha mkifika mwisho wa safari yenu ana nyie, mtamueleza sheria za wanyamapori wakati zinafundishwa mlikuwa wapi.Nilimuona akiwa amekufa, alikua anavuka barabara akagongwa na gari aisee yule mdudu ni mkubwa na anatisha tulimpima urefu alikua na futi 5 na point aisee, ukikutana nae mzima kimbia tuu kwa jinsi nilivyomuona mtu mbili hutoboi qmmk.
Nyie wakuu acheni kutufunga kamba, koboko yupi umfanyie huo mchezo? kwanza koboko meno yake ni kama meno ya mbuzi umtoe kirahisi hivyo?! maana koboko akiuma huwa haachi meno anachoma kama sindano anashusha venom mls kadhaa anakuacha hapo, kisha miaka ya nyuma enzi ya Samuel sitta kule urambo walipeleka kikosi kazi kwaajili ya kuwapunguza hawa wakuu.Mimi nilikutana Naye mbugani akawa anainua kichwa chake.Nikambana na mti kichwa chake na nikamshika mkia wake nikaanza kumzungusha juu Hadi akalegea na kumng'oa meno yake.Nilifanya Hivyo Kwa kutomjua kuwa alikuwa ni black mamba Hadi pale watu wanaojua nyoka wakaja wakamtambua Kwa jina na wanasema nilikuwa nacheza na moto
Hapa nasadiki, huyu sasa ndio the man himself, the great koboko of kusini mwa jangwa la Sahara, koboko huwa hana neno anaepusha shari mara nyingi, sema ujinga wake ni territorial snake hahami hami kutafuta makazi anashika eneo moja muda mrefu na ana mipaka yake anakata kabisa kuwa miguu kadhaa hapa mpaka hapa.Nilikutana nae mboka nikiwa 13yrs mzee wangu alikua anamashamba ya tambuku chimbo moja hivi lakuitwa igombe ,
Kabla sijamuona tulikua tumeenda kufua kisiman na vijana wa mzee jamaa akaona alama tairi la baiskel lisilo na kashata aka kipara limakatiza barabarani jamaa akaniambia muda simrefu hapa kapita koboko nikauliza umejuaje? Mwamba akaniambia huyo mwamba hatembeagi kwa kujinyonganyonga kama vinyoka vyakipumbavu yeye hujivuta tu kwa mstar mnyoofu ,bas nikapata hio knowledge moja ya mwituni
Sasa tuko zetu kisiman mwamba anafua mimi nimejilaza kwenye mchanga mweupe pee uliopatikana baada kuchimba kisima mbele yangu nikaona nyaka yuko rangi ya khaki nmemkodolea macho kama nimepigwa na butwaa akapita mbele yangu akaja mpaka usawa nilipo akatokomea mgongon huko ata kugeuka nyuma sikuweza alivyopotea kabisa ndio akili ikaja nikamwambia mwamba kapita koboko hapa jamaa akacheka sana akasema angekua koboko saiv ungekua ushabadilika rangi jamaa alikua na haki yakutokuniamin maana nilikua na reputation ya uongo uongo sana kipindi hicho sasa mwamba alivonisogelea siakaona ile alama ya unyayo alioacha chief wa pori akaniambia baba #niyeye hapa tuchape mwendo
Kilichoniokoa mimi adrenalin yangu hakuditekt hatar so sikutoa kijasho cha kujihami wala,sikuleta wenge mwamba akaniona koboko mwenzie tu
Nilivorudi kambini nikamwambia mzee huku uonge mimi nirudishe tu town
Naam huyu ndio koboko.Ndio huyu mnaemzunguzia au sio yeye?
Hahahahah.mmmmmmmmmmmmmmmmhhhhhhhhhhhhhh
Hahaha koboko hana cha kukulia timing, anakufuata live bila chenga, yeye ana mchezo mchana wa jua kali anakaa sehemu wanapopita watu wengi, anafunga njia mpaka atakapoamua mwenyewe.Tofauti na nyoka wengine ukiacha chatu , nyoka wengine wakikuona wanachimba au wana hibernate wao wanashambulia tu wakitishwa
Au chatu anashambulia tu ili ale
Ila koboko master yeye anashambulia for funny tu anaweza kuingia zizini akaruka na ng'ombe kumi halaf akapita hivi au anaweza akakuona kwa mbali akaanza kukulia timing akufanyie unyoka
Mkuu koboko hawapendi kelele, sasa ng'ombe huwa wana fujo za fuuffffufffff wakiwa wanakula sasa wakikumbana nae huwa anasimama mbele yao kuwapa onyo wakikaidi wanakuja tu, analala nao mbele kama 10 hivi halafu anaondoka zake.Nyoka karibu wote wana hulka mmoja..... Huwa wanajitahidi sana ku avoid kukutana ana kwa ana na viumbe ambao ni wakubwa kuliko wao, ni hatari kwao na ambao sio chakula chao.
Nyoka wana sense ya hali yajuu kupitia ulimi na macho yao kubaini kiumbe kinacho wakaribia....... Hivyo akikuhisi/ona kwa mbali kabla hujamuona huwa anajificha na kutulia tuli hadi upite
Na iwapo mtakutana ghafla ana kwa ana Kwenye open space au ukambananisha labda ukatani kwakawaida Koboko huwa kwanza lazima asimamishe kichwa na kutoa onyo kwa mlio mkali wa kupuliza, na ukizidi kumsogelea anaweza kukurushia sumu usoni ili kukupa upofu wa muda ili apate nafasi ya kusepa zake
Koboko huwa hashambulii bila warning labda umkanyage ghafla hapo ata attack bila warning
Kumekua na uongo mwingi kwamba ukikutana naye anakufukuzia hadi akung'ate au anaweza kuua hata mifugo mingi zizini just for fun........ Hii sio kweli
Ukileta ujanjaujanja wa migogoro ya aridhi anaruka na wewe mzimamzima, kuna mwamba ameamin wazingu wa kwenye tv kwamba king koboko akivurugwa hawagi miyeyusho , akiwa ndan ya himaya yake tena awe jike anaetaga jiandae kukimbia 60km/h mixer kuruka meter kadha wa kadhaz
Hapa nasadiki, huyu sasa ndio the man himself, the great koboko of kusini mwa jangwa la Sahara, koboko huwa hana neno anaepusha shari mara nyingi, sema ujinga wake ni territorial snake hahami hami kutafuta makazi anashika eneo moja muda mrefu na ana mipaka yake anakata kabisa kuwa miguu kadhaa hapa mpaka hapa.
Kuna yule jamaa na mke wake kule south Africa wale watu ni binadamu kweli? wale wana matatoo mwili mzima na mabangili bangili, mke sijui ana nywele za orange, wanawashika koboko kama nyoka wa bandia aisee.Sio kweli
Sio kweli huyo nyoka ni mtukutu kupindukia angekumaliza mapema tu
Koboko yupi mwenye hizo busara? kwanza ameanza lini kuwa na hizo hekma? halafu akikukimbiza anakupita kwanza halafu mkishakuwa sawa anakuteremshia makwenzi kadhaa ya sumu, unang'olewa makangarii.Ukileta ujanjaujanja wa migogoro ya aridhi anaruka na wewe mzimamzima, kuna mwamba ameamin wazingu wa kwenye tv kwamba king koboko akivurugwa hawagi miyeyusho , akiwa ndan ya himaya yake tena awe jike anaetaga jiandae kukimbia 60km/h mixer kuruka meter kadha wa kadha
Hahahaaa nyie wakuu.Sasa unabisha ulikuwepoooo ulikuwepoooo!!!!
Wewe nahisi unazungumzia Tom and Jerry, eti unajihami kwa kufanyaje?.Huyo ilikuwa nikimuona najihami kwa kukimbia huwa hataki mpishane mara mbili, huwa sio mkali kama watu wanavyosema kwamba akikuona tu anaanza kukuwinda., bali ukimchokoza au mtu alimchokoza wewe ukapita hapo. Au amekuona na bado ukaendelea kubaki eneo lake hapo ndipo huanza kuliamsha labda kama umejiandaa kupambana