Umeshawahi kutana na koboko(black mamba), uliescape vipi maana huyu sio wa mchezo

Mbona inasemekana kuwa huyu Nyoka akikuona yeye hata kama hujamuona na huna mpango naye yeye ndo anakuja kukushambulia? Au ni maneno ya mtandaoni tuu?
 
Black mamba siyo mnene
 
Huyo cobra..
 
Kuna aina mbili za koboko.
Koboko mweusi na koboko wa kijani. Wote wana simu sawa na ni nadra kupona kama akiku bite(wote hawang'oi au kuacha meno kama wafanyavyo nyoka wengne kama wakibite)
Koboko wa kijani ni mpole kupitiliza hata mkiwa sehemu mmekaa kama yupo juu ya mwembe au mti aweza fika karbu kama vile stori zinamhusu, yeye akibaini mmemuona ana tabia ya kukimbia juu sana, sasa mdeshi kama unataka kupga au ukamrushia chochote..naomba nisiendelee kwa kinachoweza kutokea..
Koboko mweusi ana tabia ya kujificha kwa kukuzoom tu lakn si kukimbia, ukileta nyoko anakuletea unyoko..koboko mweusi kuua watu zaidi kwa mkupuo siyo shida (timbwili hili nmelishuhudia) amewatesa sana wakurya wa serengeti na nyumba zao za nyasi.
Hukimbia angalau nusu ya mwili ukiwa umesimama(wakati wa mapambano) hi ni tofauti na koboko kijani.

NB: PAMOJA NA SIFA ZOTE HZO HAWATOBOI KWA NYANI, VICHECHE, TAI NA HONEY BURGER(NYEGERE)

SITAKI MAZOEA NA KOBOKO, NILICHOKIONA SITAKI TENA NIKIONE.
 
Kwa msiemjua maana uzi unaenda bila picha
 

Attachments

  • images-1.jpg
    31.2 KB · Views: 16
  • images-3.jpg
    12.2 KB · Views: 21
  • images-2.jpg
    23.8 KB · Views: 20
NatGeo wamekubrainwash sana mkuu anaye rusha mate ni swila koboko ni miyeyusho naongea kwa uzoefu mkuu nimemuona live na baadhi ya ndugu zangu ni victim wa huyo kiumbe kwa maelezo zaid unaweza kuuliza game rangers waliopo mbuga za tabora achana na hao makamera man wa natgeo ambao most of their documentaries zinakuaga staged unaweza kufuatilia pia kuhusu hili
 
Huyu mwamba hapana..
Hata ungenihadithia na almas pembeni sitaki kujua upole wake..
Nafahamu timbwili lake, nilisha mshuhudia ujinga wake mbashara siyo kupitia gugo, yutyubu wa ei ai!
🤣🤣🤣🤣 nimecheka ,ilikuajekuaje mkuu
 
Hapa unaongelea cobra na sio black mamba mazee, cobra ndo huwa ana aibu na anasimisha kichwa na kuvimba, black mamba ni jeuri na mkorofi na pia ni m deadly.
 
Mnavyosimulia visanga vya huyu nyoka namtafakari bado ila sitaki nikute nae nasikia south Afrika wako wengi,wale jamaa wa snake in the city wanawakamata black mamba kama anadaka panzi hawana hofu inakuaje hii
 

Attachments

  • images-5.jpg
    28.1 KB · Views: 19
  • images-4.jpg
    23.9 KB · Views: 20
Mnavyosimulia visanga vya huyu nyoka namtafakari bado ila sitaki nikute nae nasikia south Afrika wako wengi,wale jamaa wa snake in the city wanawakamata black mamba kama anadaka panzi hawana hofu inakuaje hii
Wale koboko wa Nat Geo watakuwa wanaugua mshipa wa ngiri, si kwa udhaifu ule.

Koboko tulionao huku si mafala, hata wanakijiji wanaochunga mifugo na kufanya shughuli zao maporini tu wanawaheshimu, na ikitokea wanamuwinda basi kuna process za kijadi wanazifanya kwanza na wanakuwa serious nazo kweli. Leo hii watu wapo huko Mbezi na Manzese darajani anasema ni wepesi kisa kaona Nat Geo. Nakataa kabisa kuwa koboko ni nyoka mpole.

Nyoka ninayefahamu ana sumu hatari lakini ana uboya mwingi ni cobra. Hao nimewaua wengi na wakubwa kirahisi tu nikiwa dogo. Wao silaha yao kuu ni kurusha mate. Ukiwa makini tu kwenye kukwepa mate yake unammaliza kirahisi maana ana ubonge fulani hivyo ni mzito. Lakini black mamba kinachomfanya kuwa hatari zaidi ni mwili wake wa mazoezi na speed yake kali sana (ndiye nyoka mwenye speed zaidi kwa mujibu wa tafiti). Kwahiyo wapuuzeni tu hao wanaosema ni rahisi kumuua maana uwezo wa kukwepa na kushambulia kwa haraka anao wa kutosha. Huyo hutoki tu mtu mmoja na kushika fimbo kindezi eti unaenda kumuua akiwa mkubwa kama unavyomuua cobra, lazima mjadili na majirani kadhaa kama si ubalozi mzima, mikakati ipangwe na tahadhari zichukuliwe, la sivyo maturubai yanaweza kutundikwa kama utani tu.
 
Basi sawa.

Japo katika posts zako kadhaa humu umeshindwa hata kutofautisha kati ya koboko na swila kiasi kwamba tunakosa uhakika ni nyoka yupi unayemzungumzia, ila ngoja tuvumilie.

Huko kwenu mmeishi na koboko sana ndani wakati moja ya sifa kuu za koboko ni kuishi mbali na binadamu na ndio maana ni nadra sana kukutana naye, hutokea kwenye makazi ya watu kama ajali tu na haweki kambi ya kudumu kama cobra na nyoka wengineo.
 
Wengi mnachanganya mafaili hapa. Mmeishi mkiua cobra (ambaye hata bibi kizee mmoja akitia bidii kidogo tu anamuua)huku mkiamini mliwaua black mamba. Koboko havimbi taya na hauawi kirahisi namna hiyo.

NB: Usiwachukulie poa wanyama jamii ya paka kwenye mishe zao ukasema tu "...aaah kaweza paka nishindwe miee?". Wewe hapo ukijifungia ndani upambane na paka mwenye afya yake ya mwili na akili hutoamini balaa lake pamoja na fimbo yako😁. Njia salama kumuua mnyama wa jamii hiyo ni kumnyemelea akiwa hana habari.
 
Kwahiyo ukimuona anaingia getoni kwako na penyewe umuache
 
Akikugonga tu na meno yake unageuka kuwa kama rangi yake, unapewa tu dakika 10 za kujuta dhambi zako, unafutika katika uso wa dunia.
 
Hakuna black mamba mweusi kwa taarifa yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…