Umewahi kukuta watu wanakula chakula gani ukakishangaa?

Umewahi kukuta watu wanakula chakula gani ukakishangaa?

Mie niliona Lushoto wanakula majani ambayo huwa tunalisha sungura (wao wanaitwa mbwembwe ama kavovo)
MAJANI MACHANGA YA MASHONA NGUO NI MBOGA PIA BILA KUSAHAU MAJANI YA MPILIPILI
 
Zambia wanakula yale mawashawasha yenye manyoya yanayowasha Yana rangi rangi halafu yanatisha na tukuyu wanakula panya buku.
Kwetu songea tunaita "mangatungu" ni upupu ule.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna wamakonde nilikuta wanakula, zile korosha ambazo hazijakomaa (za rangi ya kijani ) wanapasua ganda la juu na kutoa kiini cha ndani, then wanaviunga na nyanya na vitunguu then wanakula na ugali
 
Panya kuliwa kama msosi huko kusini, na wanapitishwa wakiuzwa kabisa barabarani.

Yule sijui ni Nyani/ngedere Kule Upareni,wanawawinda&kuwachuna vzr na kuwala.Wenyewe wanasema kaharufu kake tu ndio kanaakera kiaina lkn nje ya hapo hana shida yoyote.
 
Upupu uko kwa wamakonde wanatembeza kibakuli 500 na chumvi yao ipo kama mchanga sio nyeupe

Uzaramoni niliona wanakula kenge ila wenyew wanasema mbulu
 
Kuna wakati niliishi kijiji cha Matombo Morogoro,nilishangaa sana kukuta supu ya utumbo wa nguruwe
 
Back
Top Bottom