Umewahi kukutana ana kwa ana na mnyama gani mkali?

Siku Uje Huku Nachingwea kijiji cha Kilimarondo uone Tembo wanacheza na wanakijiji bila Shida
 
Mwaka 1959 niko machungani kijijini Ng'waukoli nikasikia mbuzi wanapiga makelele sana na mikikimikiki mingi wakizunguka jiwe fulani hivi. Kwenda kuangalia nikakutana uso kwa uso na chui. Niliganda pale pale maana ningepiga hatua tatu nne hivi ningemfikia. Basi tulibaki tumetazamana pale tu mara huyo akanyanyuka na kwenda zake pole pole bila shari yo yote. Inavyoonekana alikuwa ni jike na alikuwa na mimba karibu kabisa ya kujifungua.

Ni miaka zaidi ya 60 imepita lakini sijasahau tukio lile maana huyu mwamba akikuamria kukutoboa koo ni sekunde tu. Mungu ni mwema!

 
Vifutu hao, wana tabia ya kuwa wawili wawili.. Shamba nishaua mara kadhaa
 
Siku niko selous ndani huko mahenge balaa kwanza jamaaa.
 
Meatu au bariadi?
 
Hivi ukiganda tu hakufanyi chochote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…