Umewahi kukutana ana kwa ana na mnyama gani mkali?

Umewahi kukutana ana kwa ana na mnyama gani mkali?

Sitasahau tulilala na nyoka aina ya Cobra ukubwa mita 1.5 za mraba kwakua alishiba panya yule nyoka alishindwa kutembea hivyo alipita upande tulioelekeza vichwa vyetu wakati tumelala kwenye majamvi, kwa wale tuliokulia vjijini tunaelewa haya maisha ya kulala chini

Basi kwakua yule nyoka alishiba panya hivyo aliishia kukaa kwenye kona karibia na mlango ambapo kulikuwa na pipa la kupikia pombe ya mahindi

Majira ya Hasubuhi alikuja mke wa Baba mdogo ambae tulikua tunakaa jirani yaani nyumba ya Bibi na yao zilikua zinatizamana alikuja kuomba chanuo ili awahi Hospitari kumpeleka mtoto alikua anaumwa

Alipokuja alianza kumuamsha Sister ili ampe hilo chanuo, sister alipoamka akaanza kulitafuta cha kushangaza wakati anatafuta lile Chanuo ghafla alisikia sauti kama Bata kwenye kona akaanza kujiuliza ikiwa sisi hatufugi mabata hili bata linalopiga kelele la nani akawa anazidi kusogelea ule upande kwakua kulikua na kigiza Basi yule nyoka alimtemea mate hali iliyopelekea aangue kilio kama mtoto mdogo...

Basi tukaamshwa ili tutoke nje ile tunatoka nnje me braza na aliyekuja kutuamsha ni sister mwingine" amkeni kuna kuna nyoka mkubwa yupo hapo kwenye kona ya mlango na mpite haraka"

Ile tunatoka nje tulikuta nyomi la watu na hiyo yote ilisababishwa na sister aliyetemewa mate kulia kwa maumivu ya kutemewa mate na yule nyoka.

Itaendelea.....
 
Mimi kuna siku niko na Pikipiki nimetoka site huko nyengedi napanda Milima ya rondo mida ya saa 2 usiku aisee Mara simba huyu hapa nilianguka na Pikipiki nikainyanyua sikugeuka nyuma nilipofika kijijini palepale nilizimia.

Kuna siku tena natoka makangaka naelekea kiranjeranje kupanda basi saa 12 Asbh niko na miguu aisee ghafla naona simba dume na jike huwez amini simba Walikuwa hawana njaa walinisindikiza ila Mimi begi nilitupa na Viatu nilikimbia baadae akaja jamaa wa baiskeli aliokota viatu na begi kauliza nani mwenye begi nikamtajia vitu vilivyopo ndani kitambulisho na nguo akanipa begi.

Kuna siku tena niko speed natoka kinyope nakuja Rutamba pale katikati chui huyu hapa kainua miguu aisee nilinyosha wanguwangu akaruka pembeni.

Siku nyingine tuko na gari Tukaona tembo wanne ruangwa wanapita.

Kiboko ashanikosa kwenye mtumbwi mto ruvuma daraja la mkenda.hakuwa na mtoto alikuwa anaibuka nasikia akiwa na mtoto ndo anakuwa mkali.

Nyoka ndo sana barabarani nishkutana nao zaidi ya Mara tatu ila wadogo wadogo sijawahi kukutana na joka kubwa na kuna siku tumekaa kwenye mti ghafla nyoka kadondoka.

Aisee tunaoishi huku lindi tumepakana karibu sana na pori kubwa la selous yaani tunapocheza Cheza huku njiani tunakutana na viumbe machachari hapa ninahamu tu kuja kukutana na mamba live ndo sijawahi kumuona.
Mi kila siku simba na fisi nawakimbizaga na mwiko ule wa kusongea ugali...
Wanakujaga kumendea mbuzi wangu
 
Nilikoswa koswa na nyoka nimeenda Kwa jirani kama saa moja hiv wakat naingia nasikia kitu kinafoka sikuwa na toch na umeme ulikuwa hakuna nikasimama bahat nzuri walikuwa na tochi wakamulika aisee bonge la joka wakamuua hatujakaa vizuri mwingine anakuja wakamuua nae nafikir ni wale wanatembeaga wawili wawil
Vifutu hao. Wapo sana Iringa na alininusuru nikiwa mdogo huko Moro. Nilimkanyaga ni Mungu tu aliniepusha kwani yule kifutu(Viper) ndio nyoka mwenye sumu zaidi duniani.
 
Nilikoswa koswa na nyoka nimeenda Kwa jirani kama saa moja hiv wakat naingia nasikia kitu kinafoka sikuwa na toch na umeme ulikuwa hakuna nikasimama bahat nzuri walikuwa na tochi wakamulika aisee bonge la joka wakamuua hatujakaa vizuri mwingine anakuja wakamuua nae nafikir ni wale wanatembeaga wawili wawil
Pole😆
 
Back
Top Bottom