Umewahi kuwaza nani atashika simu yako ukifa?

Umewahi kuwaza nani atashika simu yako ukifa?

Hadaa hizo huendelea kupumbaza roho kama liwazo na wakati wa kukata kabisa roho, huja raha kubwa sana
Mbona umeongea kinyume na ninavyojua. Ukiachana na wale wanaokufa usingizini, aliyekuwa macho naona Huwa anaumia sana wakati anakata roho. Au walikuwa na masambi mengi? 😅
 
Mimi binafsi nakuelewa kwa kuwa natumia app pia. Watu wengine huwa wanapenda kulazimisha wanachojua wao ndio uwe ukweli. Umeshasema app ila mtu anakomalia iwe browser [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Umeona hii maana hawajui reality sensitive app ka JF unaanzaje kuweka remember password na username maana mi mzoefu wakutumia mitandao na siwezi allow hyo kitu kabisa
 
Wewe ulijuaje kama hizo picha ni kutoka selfika tu??
Ondoka neno "tu" hakuna sehemu nimelitumia, ila nafahamu picha nyingi huwekwa selfika kuliko sehemu zingine.
 
Miaka imebadilika labda uwe unatumia private browsing.
Kuhifadhi data za utafutaji na uingizaji (inputs) kama vile fomu na maelezo mengine kwenye kivinjari cha mtandao (browser) kuna lengo la kuboresha uzoefu wa mtumiaji. Hii inamwezesha mtumiaji kujaza fomu kwa urahisi na haraka bila kuandika upya kila wakati. Pia, kuhifadhi data hii inaweza kusaidia kupunguza kasi ya matumizi ya data, kwa sababu kivinjari cha mtandao kinaweza kutumia data iliyohifadhiwa badala ya kupakua tena kutoka kwa tovuti.
Nasemea hyo kugoma ku log in mbona jibu Hali relate kabisa ndio umecopy huko chatgpt bila ku edit
 
Kuwa huru. hata ukifuta utabadilisha ukweli kuwa ww ni nani na kama ni mchafu utakuwa mchafu mpka utakapo amua kubadilika lkn sio kwa kufuta vitu ulivyonavyo kwenye simu.
 
Amani kwenu wana jukwaa
Direct kwenye mada…

Wewe kama member Umewahi kujiuliza siku ukifariki nani ataishika simu yako?

Wiki hii kuna taarifa zimetokea hapa jukwaani, zimenifanya nitafakari sana kuhusu usalama na usiri wa JamiiForums members. Kuna thread humu baadhi ya watu wali-challenge kwamba imewezekana vipi mtoto wa marehemu akatumia Account ya mzazi wake? Je alikuwa na username? Je alikuwa na password?

Hizi kauli zikanifanya niwaze kama kweli members tuna uelewa wa privacy zetu hapa JamiiForums? Nijuavyo mimi uki-log in kwenye account yako, inabaki kuwa hivyo mpaka wewe mwenyewe uamue ku- log out au ku-clear data. Hii ni kwa yoyote anaetumia App au browser (aki - install ile app ya kwenye browser). Hivyo basi, mtu yoyote anaeweza kuipata simu ya mhusika, anauwezo wa kuitumia account yake unless awe ana log out kila akitoka.

Kutokana na technology kuwa kubwa, nafikiri ni wakati sasa wa uongozi wa JamiiForums (Moderator) ,kufanya mabadiliko kwenye systems zao kuendana na uhitaji. Waweke 'one time password system' ili kutulinda members wao. Hii ni system salama zaidi kwa vile hautalazimika ku-log aut kila mara ili uwe salama, system itafanya hiyo kazi na wewe utakapotaka ku log-in itakutumia password ya kutumia kwa wakati huo.

Hik ni muhimu kwa vile simu na computer tunazotumia kuingia hapa JamiiForums zaweza kuibiwa. Waza kwamba wewe ni baba umefariki, simu ikachukuliwa na binti yako (sio wote wanaweka password ), binti anaingia kwenye PM yako anakuta uliwahi mtongoza maana ID zetu hazijulikani. Au mama amefariki kijana wake anaingi PM anakuta mtu aliekuwa anamtongoza na kumsumbua kila mara ni mama yake. Je mhusika atakuwa kwenye hali gani?

Siku moja kuna bro aliniomba nimsaidie pc yake ime corrupt windows, baada ya repair nikiwa naweka mambo sawa nikakutana na folder imeandikwa JamiiForums, ikanivutia sana nikafungua. Ndani nilikuta sub-folders kama 40 zikiwa na majina ya members ninaowajua hapa Jamii Forums. Kufungua nakuta picha mbali mbali ambazo anazikusanya kwenye uzi wa selfika😅. Kumbe kila mdada akiweka picha, jamaa ana-icopy na kuhifadhi. Kwa kweli sikujua lengo na kwa vile ni boss wangu sikuweza kumuuliza. Ila namfatilia kwa karibu sana maana id yake nimeijua na huwa hapendi ku-comment.

Jamani kuna watu wana ma-file yetu hapa JamiiForums, wanasubiri tujichanganye tu wakiwashe😅. Guys stay safe out there.

Jukumula kujilinda lipo mikononi mwa mhusika.

Nikifa, kila kitu changu lazim kiwe deleted ndo mtu yeyote atumie
 
Ondoka neno "tu" hakuna sehemu nimelitumia, ila nafahamu pocha nyingi huwekwa selfika kuliko sehemu zingine.
Kwamba Bossi hatumii social networks nyingine zaidi ya jf ??? Kwanini umeanza na habari za kifo mkuu mtu kuingia kwenye akaunti yako si mpaka ufe mwingine anaeza azima simu yako ili atumie intanet akakuta upo jf na umesave password akiclick imoooo!!
 
Back
Top Bottom