Umoja Party ni chama chenye mlengo upi, kinaamini katika maendeleo au katika Magufuli?

Umoja Party ni chama chenye mlengo upi, kinaamini katika maendeleo au katika Magufuli?

Kama ukiwa asset watu watakutumia tu kufikia ndoto zao na watajaribu kuishi kama wewe, unafikiri ni kwa nini PLO Lumumba alihubiri Magulification of Africa, je alikuwa anamaanisha nini?

Hiki chama kinaweza kuwa chama kizuri kama kitakuwa kinaeneza sera na sio chuki, watu wamemis sana kusikia hoja zenye nguvu.

Shida ni moja, hawa ni wale waliopewa tonge wakaelewa utamu wa tonge sasa wamenyang'anywa, wameona walitafute kwa namna yao.
 
Probably itakuwa kitu vizuri CCM, ACT, Chadema wakaungana pamoja wanakubaliana na kuunganishwa na mambo mengi kikubwa kinachowaunganisha, sera yao kubwa ni Anti- Magufuli, chuki kwa kanda flani, kuangalia nyuma awamu ya tano na kutukana na kubeza kila kitu kilichofanywa wakati huo mazuri na mabaya.

Watanzania wote waliobaki ni vizuri wakaungana pamoja waanzishe chama kipya kitakachosimamia maslahi mapana ya Watanzania wote, kuangalia mbele, bila kuendekeza ukabila, udini, ukanda, matabaka, matusi, kejeli, mipasho.

Tanzania tuwe na vyama viwili tu imara.
Hivi kuna kiongozi mdini, mkabila, muuaji, mwizi na muongo zaidi ya Jiwe? Mama ushahidi upo wazi kabisa
 
Duh, hii Safi Sana. Baadae wanaungana na chadema, halafu CCM ya Samia chali.

Hii nimeipenda Sana, najua kushinda hawawezi, Ila wakishamiri CCM itabidi 2025 wa rethink watuletee Chuma Kama mzee baba mwenda zake.
Hivi watu huwa mnawaza nini! Yaani unamtaka mtu kama yule tena?
 
Hiki chama kilikuwa kianzishwe na system toka enzi za Magufuli, ila upepo haukukaa sawa. Lengo la chama hiki ni kuipa ccm ahueni wakati wa uchaguzi. Mpango ilikuwa kujitokeze wanaccm watakaojifanya wana mgogoro ndani nya ccm, kisha wavute watu, ila kifanye upinzani unaotakiwa na ccm. Naona sasa hawa sukuma gang ndio wamekabidhiwa huu usanii wa kuanzisha hicho chama. Ila hizi ni mbinu za kizee ile mbaya.

Cc: Msemaji ukweli
Muda haudanganyi. Itafahamika tu. Kinachonipa WASIWASI ni kuwa, wanaomtukana uncle M, hawana chembe ya utani usoni.
 
Kwanini bado ni siri kubwa kina nani hao watu wawili ambao waliwasilisha maombi kwa Msajili wa Vyama Vya Siasa.

OFISI YA VYAMA VINGI VYA SIASA :

Utaratibu wa kusajili chama kipya kipate hati ya muda ni huu hapa chini kutoka website ya msajili wa vyama vingi :

Chama cha siasa ni nini?

Kwa mujibu wa kifungu cha 3 cha Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992, Chama cha siasa ni kundi wa watu wenye lengo la kuunda Serikali kupitia uchaguzi halali.

2. Je kuna hatua ngapi katika kusajili chama?

3. Je ni nini kinahitajika ili kupata usajili wa muda?

  • • Wanzilishi wawili watawasilisha maombi ya usajili wa muda kwa kujaza fomu maalumu wakiambatanisha na katiba na kanuni za chama kitarajiwa.
  • Chama tarajiwa kinatakiwa kutoa uhuru wa mtanzania yoyote kuweza kujiunga bila kuwa na ubaguzi wowote wa kijinsia,kidini, kiitikadi n.k
  • • Kulipa ada ya maombi ya usajili ya shilingi 25,000.
  • • Usajili wa muda utadumu kwa muda wa siku 180, ndani ya muda huo, chama kitatakiwa kutafuta wanachama wasiopungua 2000 ( 200 kwa kila mkoa) katika mikoa 10, mikoa miwili kati ya hiyo ni lazima iwe Tanzania Zanzibar na mkoa mmoja kati ya hiyo miwili, uwe Pemba.
  • • Kutimiza masharti ya usajili wa muda yaliyopo kwenye sheria

4. Je ni nini kinahitajika ili kupata usajili wa kudumu?

  • • Baada ya kupata wanachama 2000 ndani ya siku 180, Waanzilishi watawasilisha maombi ya usajili wa kudumu kwa kujaza fomu maalumu.
  • • Kulipa ada ya usajili wa kudumu ya shilingi 50,000. • Chama kiwe kimepata Ofisi ya Makao makuu na anuani ya posta kwa ajili ya mawasiliano rasmi na kuchagua viongozi wa kitaifa.
  • • Chama kiwe kimetimiza masharti yote ya kupata usajili wa kudumu yaliyopo kwenye sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho 2015

Source : ORPP Website
 
Hiki chama kilikuwa kianzishwe na system toka enzi za Magufuli, ila upepo haukukaa sawa. Lengo la chama hiki ni kuipa ccm ahueni wakati wa uchaguzi. Mpango ilikuwa kujitokeze wanaccm watakaojifanya wana mgogoro ndani nya ccm, kisha wavute watu, ila kifanye upinzani unaotakiwa na ccm. Naona sasa hawa sukuma gang ndio wamekabidhiwa huu usanii wa kuanzisha hicho chama. Ila hizi ni mbinu za kizee ile mbaya.

Cc: Msemaji ukweli
CCM imwogope nani mpaka ifanye hivyo maana hilo li chama lenu la kaskazini lilikufa mwaka 2015 wakati mwenyekiti wenu alipobadili gia angani
 
CCM kimekuwa mchumia belly aka tumbo kinara na kwa hili kimeungana kabisa na chadema zitto nae akipiga gitaa matakoni kwa chama mboga. Leteni sera kabla ya 2025 dadeki tuwakomeshe

Kwanini Zitto anakiita ACT Wazalendo? jina sahihi ni ACT Zanzibar / maslahi.

Hi chama ACT kina-act kuleta ulaji kwa maslahi binafsi ya Zitto, hana la zaidi. ACT kingekuwa chama makini cha kitaifa sera zinazowekwa Zanzibar angesisitiza na kupiga kelele ziwekwe na huku Bara pia.

Mfano bei ya vyakula, mafuta, umeme, maji, kodi, tozo wanavyowasaidia Machinga, wafanyabiashara wadogo wangefanya hivyohivyo na huku bara n.k.

Tanzania hatuna chama chochote makini cha upinzani kwa sasa. Angalia mfumuko wa bei, bei za mbolea vifaa vya ujenzi, chakula mafuta, nafaka, usafiri, ajira, mikopo ya hovyo, teuzi, tenguzi huduma za umeme, maji, tozo, kodi zisizo na tija.

Yote hayo vyama vyote viko vya upinzani kimya. Wanasimamia nini kama hivi vitu, majanga haya yote hayawahusu?
 
Kama kinajihusisha na mawazo machafu ya jiwe basi hakinifai
Wakijitofautisha na jiwe naweza kuwasikiliza hata kwa dakika moja.
Hata ukiacha sawa tu, sasa hivi kina mamilioni ya wanachama. Subiri muda utaongea.
 
Kwanini bado ni siri kina nani waliwasilisha maombi


Chama cha siasa ni nini?

Kwa mujibu wa kifungu cha 3 cha Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992, Chama cha siasa ni kundi wa watu wenye lengo la kuunda Serikali kupitia uchaguzi halali.

2. Je kuna hatua ngapi katika kusajili chama?

3. Je ni nini kinahitajika ili kupata usajili wa muda?

• Wanzilishi wawili watawasilisha maombi ya usajili wa muda kwa kujaza fomu maalumu wakiambatanisha na katiba na kanuni za chama kitarajiwa. • Chama tarajiwa kinatakiwa kutoa uhuru wa mtanzania yoyote kuweza kujiunga bila kuwa na ubaguzi wowote wa kijinsia,kidini, kiitikadi n.k • Kulipa ada ya maombi ya usajili ya shilingi 25,000. • Usajili wa muda utadumu kwa muda wa siku 180, ndani ya muda huo, chama kitatakiwa kutafuta wanachama wasiopungua 2000 ( 200 kwa kila mkoa) katika mikoa 10, mikoa miwili kati ya hiyo ni lazima iwe Tanzania Zanzibar na mkoa mmoja kati ya hiyo miwili, uwe Pemba. • Kutimiza masharti ya usajili wa muda yaliyopo kwenye sheria


Source : ORPP Website
Walishindwa kina Samuel Sitta na CCJ ndo sembuse hizi takataka zinazoanzisha chama cha kikabila?

Tatizo la Sukuma gang bado hawataki kuamini kwamba zama zao zimekwisha rasmi na utawala wao wa kifashisti ni Mungu mwenyewe ndio ameingiliabkati ili kuwaokoa Watanzania.
 
Hivi watu huwa mnawaza nini! Yaani unamtaka mtu kama yule tena?
Watu wengi ambao walikuwa sana wanaunga mkono upuuzi wa bwana yule ni watu wajinga wajinga, wenye roho mbaya, mtu yeyote mwenye akili timamu alikuwa anaweza kung'amua ujinga na uongo ule. Leo wanalalamika ripoti ya CAG, tujiulize kwanini CAG Assad alifukuzwa kazi na taarifa zilikuwa zinafanywa siri? Kwa akili ndogo tu unaona ni kwakuwa, kulikuwa na ufisadi unafichwa.
 
Back
Top Bottom