Umoja wa Israel na Marekani uko sawa na ule wa Ujerumani na Austria 1914

Unataka USA afanyeje ili uamini kwamba ndie anayewapiga Iran, Hezzibollah, Hamas na Houthi

Hizi vita zote ukijumuisha na Ukraine Marekani ndio Injinia
 
Kuna utafiti ulifanywa na Prof Graham T Allison wa Harvard University na kuunda nadharia iitwayo The Thucydides Trap akifanyia tafiti chanzo cha vita baina ya madola ya kale ya Sparta na Athene (The Peloponessian War), iliyotokea miaka zaidi ya 2000 iliyopita.

Katika tafiti hii, alipitia vita kubwa zilizotokea miaka 500 iliyopita tokea mwaka 1500 hadi 2000 na kufahamu kwamba taifa dogo linapoanza kukua kiuchumi na kuanza kutishia mustakabali wa dola lenye nguvu duniani kwa wakati huo ni lazima vita itokee.

Tafiti yake inaonesha Case Study ya mataifa 16 makubwa, na kuangalia chanzo cha mvutano wao. Mara zote chanzo zimekuwa taifa dogo linalokuwa (Rising Power) kuanza kutishia taifa ambalo linatawala kwa wakati huo (Rulling Power). Ni mara nne tu katika hizo Case Study 16 ambapo mataifa yalikubali kukaa chini na kuelewana na kuzuia vita kubwa.

The Franco Prussian War 1871
-France (Rulling Power) vs Imperial Germany (Rising Power)

First World War 1914
- Great Britain (Rulling Power) vs Imperial Germany (Rising Power)

Second World War 1939
- Great Britain (Rulling Power) vs Nazi Germany (Rising Power)

Kiufupi sababu za vita kubwa huwa ni zilezile The Balance of Power.
 
Point of correction The Holy Roman Empire was neither Holy nor an Empire. Ila ilikuwa loose confederation of Germanic states.

Haikuwa German ilikuwa Prusia
 
Point of correction The Holy Roman Empire was neither Holy nor an Empire. Ila ilikuwa loose confederation of Germanic states.

Haikuwa German ilikuwa Prusia
That's really debatable, some scholars like Prof Roy Casagrande believe that The Holy Roman Empire was not Roman, not Holy and not an Empire. But what are the facts: It dominated a huge chunk of a land mass which was once a Western Roman Empire. And it was ruled by a single emperor who owed his pedigree to Emperor Charlemagne, king of Franks and Lombards.

This kind of debate is similar to that of saying The Byzantine Empire was not Roman Empire because it was neither Catholic nor Latin.

And by the way, Prussians and Austrians are ethnically German.
 
Naomba unifahamishe, Kwa Sasa, ni taifa gani Dogo linatishia mustakabali wa Dola kubwa ya US? Huo udogo unapimwa Kwa mambo gani?

Kiufupi sababu za vita kubwa huwa ni zilezile The Balance of Power.
Kama lengo ni "The balance of power", mara baada ya WWII, Kwa nini Dunia ilikubali US kuwa superpower? Dunia haikujua kwamba wanaokuwa vilanja wa Dunia mara nyingi ndiyo wanaokuwa chanzo Cha machafuko? Kwa nini Sasa hivi ndipo Kuna umuhimu wa kuwepo hiyo inayoitwa "The balance of power"?.

Kama balance of power itapatikana (au ipo) Kwa muktadha wa kutooneana; je, inamaana kwamba hakutakuja kupatikana superpower mwingine? Au machafuko mengine?



Superpower "the controller of world" .
 
Unataka USA afanyeje ili uamini kwamba ndie anayewapiga Iran, Hezzibollah, Hamas na Houthi

Hizi vita zote ukijumuisha na Ukraine Marekani ndio Injinia
Sijakataa kwamba US hausiki, ila siamini kama ushirika wake ni wa 100% kwenye kila angle ya vita, kwamba Marekani anafanya kila kitu yeye mwenyewe.

Nahitaji ushahidi ktk hilo, Kwa kuwa Mwaka 2007 kulikuwa na mjadala mkali sana kule US kwamba Israel hastahili kuendelea kusaidiwa ktkt sector yoyote ile, eti Kwa kuwa Sasa inajiweza kiuchumi na technology za vita.
Poll iliyopigwa iliamua kwamba Israel aendelee kusaidiwa kijeshi tu. Mwezi wa nne 2024 Marekani ilitishia kuzuia misaada Kwa Israel Kwa kuwa ilikuwa ikikiuka sheria za vita pale Gaza, Kwa kuwauwa watoto.
 
Taifa kubwa ni USA, na taifa linalokuwa ni PRC. USA kama taifa kubwa ana sehemu tano ambazo ni muhimu kwa usalama na maslahi yake (Strategic Areas):

1. Sehemu ya kwanza- The Western Hemisphere
2. Sehemu ya pili- Continental Europe
3. Sehemu ya tatu- The Persian Gulf
4. Sehemu ya nne- Asia Pacific
5. Sehemu ya tano- Central Asia/Middle East

Europe matatizo yametokea kwasababu NATO ilianza kujitanua baada ya kuona Urusi iliyotegemewa kwamba haitafika mwaka 2005 salama imeanza kukua na kuanza kujenga ushawishi wake maeneo ya Ulaya, hasahasa kwenye jamhuri za zamani za kisovieti. Marekani akaanza kutanua NATO huku akiizunguka Urusi pande zote. Urusi kang'aka na kuanza kuvamia Georgia na Ukraine mataifa ambayo ni sehemu zake kubwa za ushawishi. Ulaya Marekani anatumia NATO na EU kupambana na Urusi.

Asia Pacific, kuna taifa jingine ambalo linakuwa kwa kasi na kutishia mustakabali wa Marekani. PRC, mpaka sasa ni taifa la pili kiuchumi duniani (In terms of GDP) na la kwanza (In terms of PPP). Kiufupi, hata USSR wakati inapambana na USA, ilikuwa ina uchumi asilimia 20% tu ya ule wa Marekani. PRC, imekuwa ni tofauti kabisa kwasababu ameshampiku Marekani kama The World's Factory, The World's Leading Exporter of Merchandise and World's Largest Producer of Scientific Research.

Asia Pacific, USA anatumia makundi kama QUAD, ASEAN na AUKUS kama nyenzo za kumdhibiti (Containment) PRC asikue. USA kaenda mbali na kuanzisha alliances na nchi binafsi kama Japan na South-Korea ambazo zinamsaidia kumweka PRC kwenye kapu kwa kutumia Taiwan.

Persian Gulf, ni sehemu ambayo Marekani hakuwahi kupata mpinzani kwa miaka mingi. Lakini kuanzia 1979 mambo yake yalianza kuharibika baada ya kibaraka wake Shah kupinduliwa na serikali ya kiislamu kuingia. Iran ni taifa ambalo linakuwa mno kijeshi na haliko chini ya ushawishi wa Marekani kama ambavyo mataifa mengine kama Qatar, UAE, Israel na Saud yapo. Iran yuko na PRC na Russia.

Huku USA anaitumia Israel kuratibu mambo yake hasahasa kupiga Lebanon, Syria na Gaza. Kiufupi mataifa yaliyokuwa yanataka kukua na kutishia maslahi yake kama Iraq yalishavamiwa, amebakia Iran ndiye anayesumbua na anatafutiwa sababu ashughulikiwe.

NB 1: Baada ya WW2 dunia haikukubali USA awe Super-Power, ila ni kwasababu yeye na USSR ndiyo mataifa yaliyoibuka na nguvu zaidi baada ya mataifa mengine kuanguka.

NB 2: The Concept of Balance of Power, ndiyo ilisaidia kudumisha amani Ulaya kwa miaka zaidi ya 100 tokea mwaka 1814 baada ya Napoleonic Wars kuisha. Mataifa yote ya Ulaya yalikubaliana kwamba ili kuzuia vita ni lazima yahakikishe kwamba hakuna taifa ambalo litajitanua kuwa kubwa kuliko jingine na kuleta matatizo. Lakini mwaka 1871, Prussia walianza kujitanua na kutengeneza taifa la Ujerumani ambalo liliharibu mzani wa nguvu barani Ulaya. Mfaransa na Mjerumani wakaanza kutandikana na kuviziana kuanzia Asia, Afrika na Amerika.

NB 3: USA ni mnufaika mkubwa wa vuruge za Ulaya na Asia.
 
So if we compare Austria-Hungary and Israel we are missing a point what the main purpose of Islamic revolution in Iran.

reasons German Reich started WWII ni Treaty of Versailles pamoja na Idea kuwa Watu wa Jamii Moja lazima waishi chini ya Dola Moja, i.e Germanic people should be under single rule.

Tuangalie hili swala kwa wakati huu.
Moja ya Sababu Putin ameivamia Ukraine ni "Russia speaking people are being oppressed by Ukraine regime" so we will invade Ukraine to protect them.

Second thing why Iran ni Adui wa nchi zote za middle East baada ya Mapinduzi ya Kiislam ya 1979.
Iran wanaamini hivi kuwa all so called slamic lands should be ruled by Muslims under Imam of Iran (Iran Supreme leader) their goal can never be achieved if America and Israel are in middle east, why? Because the Americans and Israelis are most powerful forces in the region.
To achieve their goals first they have to make sure all monarchies are overthrown, this is very big serious concern to Hashimities of Jordans, Saudis, Omanis, UAE, and almost every one in middle east.
To address hii hatari mataifa yenye wasiwasi na Iran yameziharika Israel na Marekani zifanya mashirikiano ya Kijeshi.

Kwa maoni yangu Austria-Hungary is very comparable to Iran than Israel
 
Sawa boss, nimekusoma vizuri tu. Juzi tu hapa (wiki iliyopita) Putin alisema Marekani wamechelewa kuikwamisha China kusonga mbele. Putin alisema China ya Sasa haikamatiki kiteknolojia, manufacturing industries, na sector zinginezo. Putin huyo huyo katabiri kwamba, miaka michache ijayo, makampuni ya US hayatakuwa na nguvu Tena ktk ushindani wa kibiashara dhidi ya Yale ya China.
Je, Marekani atakubali Hali hiyo iendelee Kwa makampuni ya China yaendelee kustawi? au ndiyo itakuwa WWIII uliyoizungumza Kwa lengo la "balance of power" ? Ngoja tusubiri.
 
Huo ni uoni wako hafifu unaotokana na udini na upifu uliokujaa. Hakuna mwenye akili timamu asiyeona genocide inayofanywa na Wazayuni waliyojificha kwenye koti la Uisraeli.
Unajua neno Genocide kwenye huo mgogoro lilianzia wapi?
Anyway, kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake, kama maoni yangu ni uoni hafifu ni vizuri pia.
Bora mimi mwenye uoni hafifu kuliko wewe unaebeba vitu kama dodoki na kuvitapika hivyo kisa fulani kasema.
 
kuna uwezekano Iran tayari analo bomu la nyuklia,
 
Kinachoendelea Gaza ni vita kati ya Israel na hamas kama ambavyo Israel inapambana na Hezbollah.

Je, huko Ukraine Russia inafanya Genocide?
Genocide is an international crime which can be committed against a group of people (ethnicity, religious or nationality), during both peace times and an armed conflict.

Unaposema kwamba Afrika Kusini ndiyo ametunga neno GENOCIDE ilhali kuna mkataba wa kimataifa ambao unakataza GENOCIDE, THE GENOCIDE CONVENTION 1948 unataka sisi tukueleweje labda ???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…