Umoja wa vyama 10 vya upinzani nchini Tanzania vimefungua kesi Mahakamani Kuu kupinga muswada wa sheria ya vyama vya siasa

Isome vizuri hiyo ibara usikopi nusu nusu, inazungumzia vyote unaweza kupinga sheria au (hatua) process.
 
Hata hiyo kupinga kila jambo huwa kuna hoja za msingi sana kwa wapingaji, mnapaswa muwe huru kifkra ili muwasikilize hao wanaopinga siyo mnashupaza shingo hamtaki mkosolewe kana kwamba kila mnalofanya liko sahihi kwa %100 kitu ambacho ni kujidanganya

2020 John Walker out
 
Wapinzani mnafanya mambo ya kutia aibu kabisa;

Mtu anaamua kwa makusudi kabisa kukiuka masharti ya dhamana; wenzake wanaamua kukutana huko hotelini na kumtangaza kuwa ni mfungwa wa kisiasa. What a shame.
Wewe unaona ni mfungwa wa ubakaji?

2020 John Walker out
 
Shukrani mkuu kwa kuweka kumbukumbu hii ili hawa vichwa maji waweze kuelewa msingi wa shauri la kupinga mswada huo kupitishwa kuwa sheria

2020 John Walker out
 
Mtanyooka tu!
Hivi kwa akili yako nani kanyooka kama sio lijiwe?
We kila anachogusa anaumbuka unadhani anasikia raha? Ni aibu tu mtu mzima kuonekana ovyo!
 
Kwenye kundi la mamba hata kenge wamo. Kwenye mahakama wamo kenge pia, kama yule Mashauri wa Kisutu au yule wa kesi ya Lema Arusha ambaye hata kwenye appeal ,Jaji alimtukana kiutu uzima yeye na ofisi ya DPP
 
Imefunguliwa Mahakama Kuu ya Tanzania, case no. 31/2018 ipo mbele ya jopo la majaji 3, Sehel, J., Maghimbi, J., na Masoud, J.
Kuna mwandishi wa pili kauliza swali zuri sana kwamba wanapinga contents au process. Katika majibu naona Bashange anajichanganya sana; mara aseme ni suala la kikatiba mara siyo la kukatiba. Kama ni suala la kikatiba basi mahakama hiyo haina nguvu ya kulisikiliza hilo suala. Watapigwa PO keshokutwa na mambo yanaishia hapo hapo. Kama hawajajiandaa vizuri basi kesho PO inawahusu. Halafu Zitto anaulizwa swali zuri badala ya kujibu anasema kesho mahakama inaweka historia!
Wanajichanganya sana na wataweka historia ya kujichanganya
 
Muda mwingi umetumika kuijenga na kuitunza AMANI tuliyonayo leo. Jambo la ajabu kuna wajinga wachache wanataka kuiharibu AMANI hii.

This is unacceptable!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona walijibu vizuri tu kuwa wanapinga vyote content na process, akatolea mfano wa content ni ku criminalise shughuli za kisiasa, process ni kutoshirikishwa kwa wadau, hata hivyo tusi predict hukumu kama alivyofanya Zitto na wewe.
 
Wapinzania wamefungua kesi na majibu yao kabisa kwa mtazamo wangu hi kesi itatupiliwa mbali kwasababu kesi imefunguliwa kwa mtazamo tu Wala si kisheria.

Lets wait and see
 
Wapinzania wamefungua kesi na majibu yao kabisa kwa mtazamo wangu hi kesi itatupiliwa mbali kwasababu kesi imefunguliwa kwa mtazamo tu Wala si kisheria.

Lets wait and see
Inatupiliwa mbali saa kumi na moja asubuhi!
 
Nijuavyo kupokelewa maombi ni hatua moja, kukubalika kusikilizwa shauri ni hatua nyingine.
 
Umefanya vema kuweka vifungu hivyo katiba. Vyote vinaxungumzia sheria zinaxokiuka misingi ya katiba, sio Mswaada ulioko bungeni unaojadiliwa na muhimili mwingine wa kutunga sheria na haujawa SHERIA bado. Kwa sasa vyama vilitakiwa kujenga ushawishi kwa wabunge wengine, muswada usipitishwe bungeni na kama ukipita na kuwa sheria ndio nafasi ya kuomba Mahakama kutafsiri ukiukwaji wa haki. Mahakama kuingilia jambo linalojadiliwa na halijaamuliwa na bunge ni chanzo cha mgogoro wa kikatiba.
 
Kwani mlikatazwa na nani kuwa na wabunge wengi. Vyama 10 mmeshindwa kuwa na wabunge kwa umoja wenu kufikia idadi sawa na CCM. Hapo ni tatizo, mjitafakari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…