Umoja wa wanawake CCM wasikitishwa na udhalilishaji wa Makonda, watoa tamko

Kwa uzoefu wa CCM hasa hii ya sasa tayari Makonda kayakanyaga. Wakuu wa CCM wakishavalia njuga suala ni lazima uvune ulichopanda. Hata angekuwa mwenyekiti wa UVCCM ndo katoa kauli ya kuchukizwa na hicho kitendo lazima Konda Boy yangemkuta tu. Tusubiri tuone.
Makonda yupo na ataendelea kuwepo labda mama aondoke.
 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) Marry Chatanda ameeleza kusikitishwa na kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda alichokiita unyanyasaji na udhalilishaji wa watendaji wanawake kwenye maeneo yao ya kazi.

Chatanda ameyasema hayo leo Jumamosi, Mei 25, 2024 jijini Dodoma wakati wa semina ya wabunge wa viti maalumu, manaibu waziri, mawaziri, makatibu wa jumuiya ya wazazi ngazi ya mkoa na wilaya ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania bara, Abdurahman Kinana

"Kuna 'clip' imezunguka kule Arusha, Longido haikuwa jambo jema wala sio zuri hata kidogo, kama wewe ni kiongozi mkuu wa Serikali na umemuona mtendaji wako amekosea ni vizuri ukakaa na kuzungumza nao, kwa suala la udhalilishaji wa wanawake siwezi kukubaliana nalo, tunaomba tuheshimiwe wanawake, tena sisi wanawake ni watendaji wazuri kuliko wanaume.

Chatanda amesema kuwa clip hiyo tayari ameshamtumia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Abdulrahmani Kinana.

Hatua hii ya UWT inafuatia matamshi ya Makonda katika kipande kifupi cha video kinachosambaa katika mitandao ya kijamii ambapo anasikika akisema, ...usiongee na mimi hivyo nina mke mzuri huongei na mchumba wako hapa...
Hatelezi ulimi bali anatatizo la ulevi wa madaraka na analo toka muda sana nashangaa wateuaji sijui huwa wanatumia tumbo kufanya vetting mbona hatukuwahi kuwa na takataka za aina hii kwenye uongozi wa miaka ya nyuma
 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) Marry Chatanda ameeleza kusikitishwa na kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda alichokiita unyanyasaji na udhalilishaji wa watendaji wanawake kwenye maeneo yao ya kazi.

Chatanda ameyasema hayo leo Jumamosi, Mei 25, 2024 jijini Dodoma wakati wa semina ya wabunge wa viti maalumu, manaibu waziri, mawaziri, makatibu wa jumuiya ya wazazi ngazi ya mkoa na wilaya ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania bara, Abdurahman Kinana

"Kuna 'clip' imezunguka kule Arusha, Longido haikuwa jambo jema wala sio zuri hata kidogo, kama wewe ni kiongozi mkuu wa Serikali na umemuona mtendaji wako amekosea ni vizuri ukakaa na kuzungumza nao, kwa suala la udhalilishaji wa wanawake siwezi kukubaliana nalo, tunaomba tuheshimiwe wanawake, tena sisi wanawake ni watendaji wazuri kuliko wanaume.

Chatanda amesema kuwa clip hiyo tayari ameshamtumia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Abdulrahmani Kinana.

Hatua hii ya UWT inafuatia matamshi ya Makonda katika kipande kifupi cha video kinachosambaa katika mitandao ya kijamii ambapo anasikika akisema, ...usiongee na mimi hivyo nina mke mzuri huongei na mchumba wako hapa...
Hiki ni kikao cha kimetengenezwa,ili kimjengea makonda ajali ya kisiasa.

Kinana hamtaki makonda, na ccm ni ya wote.

Mkimgusa makonda sasa mtajua CCM Ina watu wachache.

Watu wanateseka na kero za kimaisha mnasema UWT?

WANAWAKE WANAOTESEKA NA WENYE KERO NI WENGI KULIKO WANAWAKE WALIOKO UWT.
 
Back
Top Bottom