Umoja wa wanawake CCM wasikitishwa na udhalilishaji wa Makonda, watoa tamko

Umoja wa wanawake CCM wasikitishwa na udhalilishaji wa Makonda, watoa tamko

Kwenye siasa vita moja ikiisha nyingine inaanza na kuama upande ni jambo la kawaida sana.

Ni kwa sababu hizo, ndio maana utakutana na kauli za hovyo walizopewa wanasiasa kama vile “tofauti ya dada poa na mwanasiasa; mwanasiasa bei yake ni kubwa zaidi” lakini wote wapo tayari kufanya kazi na yeyote mwenye dau.

Hakuna uadui wa kudumu kwenye siasa, kuna maslahi ya kudumu. Vita moja ikiisha nyingine inafuata na wachezaji wanabadili upande kwa maslahi yao mapana.

Ama ni utoto kinachoendelea huko CCM kila siku kumfanyia majungu Makonda, au wahuni wana mtu wao 2025 wanataka popular support ya ‘bi-tozo’ iendelee kubaki chini ili iwe rahisi kumvaa.

Vinginevyo hata dictatorship kama huko China serikali inajaribu kutafuta legitimacy ya uwepo wao kwa kuwafanyia kazi wananchi na kutatua shida zao. Hata wanapozuia wapinzani unakuta bado wana support ya wananchi walio wengi.

Uchaguzi mkuu sio kama chaguzi za ndani ya CCM wajumbe wananunulika kirahisi au wapiga kura wote ni watumishi wa serikali wanaopenda viongozi wazembe katika kuwasimamia wafanye yao. Wapiga kura waliowengi ni wananchi wa wakawaida na wengi ndio hao wanaojaa kwenye mikutano ya Makonda na huko anamtengenezea imani Samia anawajali.

Hata kama unajua unashinda chaguzi kwa hila, bado kuna umuhimu wa kutafuta legitimacy ya kuonekana unapendwa. Na mtu anaefanya hiyo kazi on the ground na kueleweka kwa sasa ni Makonda peke yake, wengine ni kuandaa makongamano ya kujitekenya na kucheka wenyewe hakuna wananchi wanaosikiliza upuuzi wao.

Bi Tozo aelewi somo au watu aliowaweka karibu ndio waliovuruga uraisi wake.

Ni upuuzi wa hali ya juu viongozi wa CCM kuwa na wivu na Makonda.

Ukiangalia clip wala akumdhalilisha yule dada, ye mwenyewe anaongea kwenye mkutano wa hadhara uku anatabasamu na kuchekacheka bila ya sababu za msing, ndio Makonda alipomwambia mbona unaongea kama tunatongozana mimi na wewe wakati wananchi wanataka majibu; mimi tayari nina mke mzuri (aina maana yule dada mmbaya).
 
1000195045.jpg
 
Makonda ni mwehu.

Kwenye hicho kikao, yeye kama kiongozi wa mkoa, habari ya mke wake kuwa mzuri au mbaya ilikuwa na ubusiano gani? Nadhani ana uwezo mdogo sana wa akili. Hajui aseme nini, wapi, wakati gani na kwa namna gani. Yeye muda wote ni uropokaji.
Jamani Hapo kakosea wap kijana wa watu.
 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) Marry Chatanda ameeleza kusikitishwa na kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda alichokiita unyanyasaji na udhalilishaji wa watendaji wanawake kwenye maeneo yao ya kazi.

Chatanda ameyasema hayo leo Jumamosi, Mei 25, 2024 jijini Dodoma wakati wa semina ya wabunge wa viti maalumu, manaibu waziri, mawaziri, makatibu wa jumuiya ya wazazi ngazi ya mkoa na wilaya ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania bara, Abdurahman Kinana

"Kuna 'clip' imezunguka kule Arusha, Longido haikuwa jambo jema wala sio zuri hata kidogo, kama wewe ni kiongozi mkuu wa Serikali na umemuona mtendaji wako amekosea ni vizuri ukakaa na kuzungumza nao, kwa suala la udhalilishaji wa wanawake siwezi kukubaliana nalo, tunaomba tuheshimiwe wanawake, tena sisi wanawake ni watendaji wazuri kuliko wanaume.

Chatanda amesema kuwa clip hiyo tayari ameshamtumia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Abdulrahmani Kinana.

Hatua hii ya UWT inafuatia matamshi ya Makonda katika kipande kifupi cha video kinachosambaa katika mitandao ya kijamii ambapo anasikika akisema, ...usiongee na mimi hivyo nina mke mzuri huongei na mchumba wako hapa...
Amakweli Dunia ina mambo, "KINYAGO" walicho kichonga wenyewe leo kinawatisha🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Merry chatanda amepiga kelele kumhusu makonda ,lakini pia chini chini mahali anakopita huyu kiongozi watu wanapiga kelele ambazo hazisikiki, sauti zinazomsifia ni zile ambazo zimejaa hofu. Kuogopwa! Labda anawaongoza watu kwa kuwatisha!

Moyoni hata waliomteua hawajui chakufanya! Anaweza akafanya vizuri mambo matano akaharibu mambo 20! Akipewa maiki kuhutubia watu wanashika roho mkononi kwa sababu anaweza kuongea lolote wakati wowote!

Huyu mtu ana ulemavu wa ulimi tusimhukumu ,tumuombee mungu amponye ,popote ulipo ndugu Paulo christian makonda pokea uponyaji wa ulimi katika jina la YESU kristo ,Amina
Hata kama Mimi unanibania pua nakuchana live!

Ifikie hatua tuache kubembelezana watz!ujinga ni mwingi mnonkwenye hizi halmashauri!!
 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) Marry Chatanda ameeleza kusikitishwa na kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda alichokiita unyanyasaji na udhalilishaji wa watendaji wanawake kwenye maeneo yao ya kazi.

Chatanda ameyasema hayo leo Jumamosi, Mei 25, 2024 jijini Dodoma wakati wa semina ya wabunge wa viti maalumu, manaibu waziri, mawaziri, makatibu wa jumuiya ya wazazi ngazi ya mkoa na wilaya ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania bara, Abdurahman Kinana

"Kuna 'clip' imezunguka kule Arusha, Longido haikuwa jambo jema wala sio zuri hata kidogo, kama wewe ni kiongozi mkuu wa Serikali na umemuona mtendaji wako amekosea ni vizuri ukakaa na kuzungumza nao, kwa suala la udhalilishaji wa wanawake siwezi kukubaliana nalo, tunaomba tuheshimiwe wanawake, tena sisi wanawake ni watendaji wazuri kuliko wanaume.

Chatanda amesema kuwa clip hiyo tayari ameshamtumia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Abdulrahmani Kinana.

Hatua hii ya UWT inafuatia matamshi ya Makonda katika kipande kifupi cha video kinachosambaa katika mitandao ya kijamii ambapo anasikika akisema, ...usiongee na mimi hivyo nina mke mzuri huongei na mchumba wako hapa...
Mpenda kiki ameshaharibu...
 
Ni Umoja wa wanawake CCM? Au Ni Mary chatanda ? wasikitishwa na udhalilishaji wa Makonda, watoa tamko
 
Najua Mama chatanda ni spika, yupo mwenye agenda nyuma ya hili suala.

Mungu ampiganie Makonda, ipo siku kuna watu wataaibika. Makonda chapakazi tambua wapo watu nyuma yako tunakuombea.

Mama asikubali maadui wa Magufuli wawaandame wasaidizi wake
 
Merry chatanda amepiga kelele kumhusu makonda ,lakini pia chini chini mahali anakopita huyu kiongozi watu wanapiga kelele ambazo hazisikiki, sauti zinazomsifia ni zile ambazo zimejaa hofu. Kuogopwa! Labda anawaongoza watu kwa kuwatisha!

Moyoni hata waliomteua hawajui chakufanya! Anaweza akafanya vizuri mambo matano akaharibu mambo 20! Akipewa maiki kuhutubia watu wanashika roho mkononi kwa sababu anaweza kuongea lolote wakati wowote!

Huyu mtu ana ulemavu wa ulimi tusimhukumu ,tumuombee mungu amponye ,popote ulipo ndugu Paulo christian makonda pokea uponyaji wa ulimi katika jina la YESU kristo ,Amina
Ulimi ndiyo huamua mtu azungumze nini?
 
Back
Top Bottom