UN kupinga mradi wa Steigler's Gorge ni uhujumu


Ukiona Shetani anakupiga vita ujue uko sahihi, kaza mwendo! Ukiona Shetani anakuchekea ujiulize umekosea wapi! Pia ukiona UN na US wanakupiga vita ujue uko sahihi, kaza mwendo!

Ukiona hao watu wanakusifia ujue kuna mahali umekosea, tafuta hilo kosa jirekebishe, songa mbele!

Walianza na TAZARA, sasa hivi wamegeukia Umeme wetu wa SG!

Hivi na sisi tunaweza kuwapinga katika project zao zozote, km vita vya Iraq na Libya, hivyo vita haviharibu mazingira ukiachilia mbali vifo vya watu wasio na hatia?

Dr John P. J. Magufuli, usiwasikilize, sio watu wazuri hawa, wana uchungu wa makinikia uliyoyazuia Bandarini. Kaza mwendo baba!
 
Afadhali UN mmetufanya tupumue hata hivyo bajeti ya ujenzi haipo tukimaliza kununua wapinzani tutajenga

Lukwafya
 
Magufuli Magufuli Magufuli Dr.JPM
Mbona unachelewa kujenga....kuanza Mradi wa Stiegliers gorge Baba Agggrrr....wazungu Wengi hawapendi huu Mradi....wanataka tuendelee kuwakopa hela....

Makampuni ya Ulaya ya Aggreko,Songas,Moore&Prom inawezekana kabisa Wakatumia nguvu zooooote Mradi huu Ushindwe...coz Maslahi yao ya Gas,jaman Pitia JF baba usome
Kamwe USIRUDI NYUMA,UKIUACHA TUU HUU MRADI JUA UCHUMI WA VIWANDA KWISHNEY NA MITAJI YA HELA TUTAWATEGEMEA WAZUNGU MPAKA TUFE...
STIEGLIERS GORGE NDO ITALETA KITU TUNAITA "MULTIPLIERS EFFECTS" KATIKA UCHUMI.
 
Magu piga kazi achana na kelele za hawa manyumbu wa humu na hao wenzao wa huko nje
Na kwa huyu jamaa wakaanga sumu dhidi ya nchi yao wameshapoteza. Hii miradi jamaa lazima atakamilisha.
 
Wakitugomea kabisa turudi kwenye Umeme wa gesi maana walisema ndio suluhisho na tunazo cubic meters matrilioni mengi.

Bomba lilishajengwa hadi Dsm na Kinyerezi 1 & 2 zina tumia gesi. Au kuna shida gani kwenye gesi?
 
Mkuu UNASEMA....TULISEMA.......maana yake haya masuala hayakuhusu!
Hivyo basi maelezo yoyote hayatakukidhi!
Endelea na msimamo wako wa kukaa kando kwenye masuala ya msingi.
 
Sasa hilo la study linahusianaje na UN? Hao wanajiita conservationist linawahusu nini? Wao wanaangalia madhala ya kimazingira na siyo hasara ya kiuchumi.

UN wanahangaika na mambo ya kisiasa, sasa leo mtu analeta mambo ya bwana!
 
Acha woga, aiseee.
 
Sitakudadavulia kwa pesa yangu, kanunue na wewe usome uelewe!
 
Utadhani wana hela kumbe za kuomba. Ushamba tu. UN kazia
 
Sitakudadavulia kwa pesa yangu, kanunue na wewe usome uelewe!
Unadhani wote tunaishi msimbazi! Au umeona aibu ya kuamini heading ya gazeti. Jilazimishe kuwa msomi. Kwangu mimi nikiona heading kama hiyo, brain inajiongeza yenyewe mara moja!
 
Unadhani wote tunaishi msimbazi! Au umeona aibu ya kuamini heading ya gazeti. Jilazimishe kuwa msomi.

Mkuu mi si msomi lakini bahati mbaya nina akili kama punje ya dalahari.
Sasa hapo hapo ulipo, google hilo gazeti ulisome.
 
Yaani wewe BRAMO UMEFILISIKA KIMAWAZO ! Hivi mpaka sasa hujaelewa mradi Wa Stiegler's Gorge ukikamilika utakuwa na manufaa gani kwa Taifa ? Pole sana!!
 
Mkuu UNASEMA....TULISEMA.......maana yake haya masuala hayakuhusu!
Hivyo basi maelezo yoyote hayatakukidhi!
Endelea na msimamo wako wa kukaa kando kwenye masuala ya msingi.
Yeah MLISEMA maana nachukulia wwe mtoa taarifa umechukua upande wa serikali kwenye kutetea mradi wa Stiegler's.... Hivyo serikali hiyo hiyo ambayo leo inasema SG ndio habari ya mujini ilisema miaka 4 iliopita kwamba Gesi ndio suluhu la nishati ya umeme hapa TZ hivyo nashangaa badala nyie wasomi mhoji hizo ahadi za gesi kama zimefikia malengo ndio kwanza mnatuminisha tena kwamba SG ndio mradi wa kumaliza shida ya umeme.... Hivi hizi ahadi mpaka lini?? Wasomi tunawategemea muhoji ndio kwanza mnasupport huu ujinga wa SG

Huoni tuna miradi mingi inahitaji funding hasa ya maji vijijini ama ya kilimo cha umwagiliaji au hata kuongeza ndege kwa ajili ya ATCL..... We have a way lot than switching lanes every now on then be it from hydro to coal to gas.... And then guess what!! We are talkin about hydro again???

Duh kazi ipo
 
Hapa nafuatilia comment za wale wapenda Wazungu. Nione .
Nani anayependa wazungu kuliko serikali ambayo ndio moja ya wakopaji na wafutiwa madeni wakubwa na wazungu afterall waliingia mikataba mibovu kuanzia gesi hadi madini na kusababisha hasara ya trillion zaidi ya 400 kwa mujibu wa ripoti za kamati zote 4!!!! Nani mpenda wazungu hapo
 
Yaani wewe BRAMO UMEFILISIKA KIMAWAZO ! Hivi mpaka sasa hujaelewa mradi Wa Stiegler's Gorge ukikamilika utakuwa na manufaa gani kwa Taifa ? Pole sana!!
Hapana hajapinga anashangaa tu serikali ilisema gesi ndio suluhu ghafla tena tunarudi kwenye umeme wa kutegemea maji!!!!

Yaani kwa kuwa umeme wa gesi tulishaanza kufua basi pesa hyo ya stiegler ielekezwe kwingine mfano kilimo au uvuvi n.k ili nchi isonge mbele maadam alternative ipo kuliko miradi miwili target moja wakati kuna watu wanategemea kilimo cha mvua bado na wapo karne ya 21.... Kwanni msiwekeze huko kila siku umeme umeme wakati gesi ipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…